Quantcast
Channel: Michezo na Burudani – Tanzania Habari | Jamii | Michezo | Mahusiano | Kazi | Thehabari.com
Viewing all 521 articles
Browse latest View live

Warembo Redd’s Miss Kinondoni 2013 Wakutana na Kamati ya Miss Tanzania

$
0
0

Mkurugenzi wa Kamati ya Miss Tanzania, Hashim Lundega akizungumza na warembo wa Redds Miss Kinondoni 2013.

Mkuu wa Itifaki wa Kamati ya Miss Tanzania, Albert Makoye akiongea machache wakati kamati hiyo ilipotembelea Kambi ya Mazoezi ya Redds Miss Kinondoni 2013 iliyopo katika hoteli ya JB Belmont hoteli jijini Dar es Salaam. Kutoka upande wa mkuu wa Itifaki ni katibu Bosco Majaliwa, Mkurugenzi wa kamati ya Miss Tanzania Hashim Lundega, mjumbe wa kamati hiyo, Lucas Rutta wakiwa pamoja muandaaji wa mashindano hayo Dennis Ssebo.
Mkurugenzi wa kamati ya Miss Tanzania Hashim Lundega, akiongea na warembo wanaowania taji la Redds Miss Kinondoni 2013 mara baada ya kuwatembelea kambini kwao na kujua wanaendeleaje. Lundenga aliwaasa washiriki hao kuongeza bidii katika mazoezi yao ili waweze kufanya vyema katika fainali yao.

Warembo wa Redds Miss Kinondoni wakiwa wamejipanga mara baada ya kumaliza mazoezi.
Na Cathbert Angelo, Kajunason Blog

KAMATI ya Miss Tanzania ikiongozwa na Mkurugenzi Hashimu Lundenga imetembelea kambi ya Redds Miss Kinondoni 2013 wanaotarajiwa  kumenyana Alhamisi ya Juni 20 katika shindano Redd’s Miss Kinondoni Talent 2013 Ukumbi wa Shekinah Garden, Mbezi Beach jijini Dar es Salaam.

Akizungumza mratibu wa shindano hilo mara baada ya kuwakaribisha wageni, Dennis Ssebo alisema maandalizi ya kuelekea shindano hilo yanaendelea vizuri na kueleza mshindi atakabidhiwa zawadi zake kwenye fainali ya shindano hilo ambalo litafanyika Juni 21 mwaka huu katika uwanja wa hoteli ya Golden Tulip.

Alisema kwamba shindano la mwaka huu litaandika historia mpya ya urembo kwa wilaya ya Kinondoni maana wamejipanga na kupata sapoti ya kutosha, hivyo mashabiki wa mashindano ya urembo wakae mkao wa kupata raha.

Mashindano ya Redd’s Miss Kinondoni yamedhaminiwa na Redd’s Original, Chilly Willy Energy Drink, Oriflame Natural Beauty Products, Kiota cha Maraha WANTASH, Virago, Times Fm, JB Belmonte Hotel, Michuzi Media Group, Michuzijr Blog, Mtaa Kwa Mtaa Blog, Fullshangwe Blog, HandeniKwetu Blog, Mrokim Blog, TheHabari.com, Jestina George Blog, SufianMafoto Blog, Global Publisher, Mdimuz Blog, Lukaza Blog, MO Blog na Kajunason Blog.

EAC Yashiriki Tamasha la Filamu Zanzibar

$
0
0

Tamasha la Filamu Zanzibar-2013

Na Mtua Salira, EANA-Arusha

KWA mara ya kwanza katika historia ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Sekretarieti ya jumuiya hiyo inashiriki katika Tamasha la Kimataifa la Filamu Zanzibar (ZIFF) kuongeza uelewa zaidi wa jumuia kwa watengenezaji wa filamu na wasanii juu ya masuala ya mtangamano.

Tamasha hilo la 16 litakalochukua wiki zima na ambalo ni moja ya matamasha makubwa kabisa Kusini mwa jangwa la Sahara, lilifunguliwa Jumapili na litaendelea hadi Julai 6.

EAC kwa kushirikiana na Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Ujerumani (GIZ) limeandaa warsha ya uandishi wa skripti za filamu juu ya matangamano wa kikanda na kuwezeshwa na Mtengenezaji wa filamu na mwandishi wa skripti mashuhuri wa kutoka Nigeria, Femi Kayode.
Skripti itakayokuwa bora zaidi itatengezwa katika makala maalum.

Akifungua warsha hiyo Juzi, Mkuu wa Mawasiliano na Masuala ya Umma wa EAC, Richard Owora Othieno alisema Sekretarieti ina mpango wa kutengeneza makala maalum ya elimu huhusu mwenendo mzima wa EAC kwa lengo kuwafanya wana Afrika Mashariki kuwa na uelewa wa kutosha juu ya EAC.

“Tutatengeneza makala maalum yatakayoeleza kinagaubaga juu ya masuala ya mtangamano na kuongeza kasi juu ya ajenda ya uelewa zaidi kuhusu shughuli za EAC na mipango yake,” aliwaambia washiriki wa warsha hiyo.

Alifafanua kwamba hapo baadaye EAC itafanya maonyeha ya filamu juu ya mtangamano wa EAC katika tamasha hilo la ZIFF. Meneja wa GIZ anayeshughulikia Mtangamano wa EAC, Miriam Heidtmann alisema taasisi yake itaendelea kuunga mkono juhudi za ushirikiano wa jumuiya hiyo.

“Tuko tayari kuunga mkono mafunzo kwa waandishi wa habari na masuala yanayoendana nayo ili kuongeza uelewa wa wana Afrika Mashariki kuhusu EAC,” alisema.

Mrembo Sylona Atwaa Taji la Redd’s Miss Temeke 2013

$
0
0

Mshindi wa Redds Miss Temeke 2013, Sviona Nyameyo (katikati), ambaye ni mwanafunzi wa mwaka wa kwanza wa Sheria Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), akiwa na mshindi wa pili,  Narietha  Boniface, mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Sayansi ya Tiba Muhimbili (MUHAS), na mshindi wa tatu, Latifa Mohamed ambaye ni muhitimu wa kidato cha sita baada ya kutangazwa washindi katika shindano hilo lililofanyika viwanja vya Sigara Chang’ombe Dar es Salaam juzi

Na Mwandishi Wetu

MREMBO Sylona Nyameyo jana usiku alifanikiwa kutwaa taji la Redd’s Miss Temeke lililofanyika katika Ukumbi wa TCC Changombe, jijini Dar es Salaam.

Sylona aliye mwanafunzi wa mwaka wa kwanza katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), akisomea mambo ya sheria alifanikiwa kuwashinda warembo wengine na kufanikiwa kujitwalia taji hilo.

Katika shindano hilo lililokuwa na upinzani mkali, ulioambatana na burudani za kumwaga, ilishuhudiwa nafasi ya pili ikienda kwa Marietha Boniface, ambaye naye ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Tiba Muhimbili (MUCHS).

Nafasi ya tatu ilikwenda kwa Latifa Mohammed ambaye amemaliza kidato cha sita mwaka huu, hivyo warembo hao kujihakikishia nafasi ya kuingia katika fainali za Redd’s Miss Tanzania.

Ushindani ulionekana dhahiri katika shindano hilo, ambapo warembo walikuwa wakichuana mno, huku mashabiki waliojitokeza hapo wakijikuta wakishangilia muda wote.

Akizungumza mara baada ya kuvikwa taji hilo, Sylona alisema amefurahishwa mno na matokeo hayo na atahakikisha hawaangushi wakazi wa Temeke katika shindano la Redd’s Miss Tanzania.

“Nilijua toka mwanzo lazima niwashinde, maana nilijiamini na niliona nina vigezo vyote, sasa ni wakati wa kwenda kupambana katika Redd’s Miss Tanzania ili kurudisha heshima ya Temeke,” alisema.

Shindano la Redd’s Miss Tanzania kwa sasa linadhaminiwa na kinywaji cha Redd’s Original kinachozalishwa na kusambazwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL).

Mtanzania Aibuka Bingwa Kuruka Kamba Duniani

$
0
0

>

Na Jennifer Chamila-MAELEZO

KIJANA wa Kitanzania Hamisi Kondo ameibuka mshindi wa dunia katika mashindano ya kuruka kamba yaliyofanyika nchini Marekani Julia 5 hadi Julai 13 mwaka huu. Mashindano hayo yalihusisha nchi 14 zikiwa na wachezaji 480, huku Bara la Afrika likiwakilishwa na Tanzania, Kenya na Afrika ya Kusini ambapo kijana Hamisi mwenye umri wa miaka 14 Mtanzania aliweza kujinyakulia ushindi huo.

Kijana huyo ambaye ni yatima aliyelelewa na kituo cha kulelea watoto yatima cha Dogodogo Center kilichopo jijini Dar es Salaam na kupata mafunzo ya mchezo wa kuruka kamba kituoni hapo na baadae kupata ufadhili kutoka kwa Bwana na Bibi Amy Canady nchini Marekani ambako aliweza kusoma na kuendeleza kipaji chake.

Akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Hamisi amezungumzia mafanikio yake na kuwaasa vijana wenzake kutokata tamaa ya maisha kwa kuwa na juhudi ya kupambana ili waweze kufikia malengo waliyojiwekea.
“Nawaomba watoto wa mtaani na yatima kutokata tamaa ya maisha kwani hata mimi nilikuwa kama wao na nimeweza kufanya juhudi na kufanikiwa,” alisema Hamisi.

Naye Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo, kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Juliana Yassoda aliwaomba vijana kutong’ang’ania michezo mikubwa kama mpira wa miguu kwani kuna michezo midogo midogo ambayo wanaweza kucheza na kufanikiwa kama ilivyo kuwa kwa Hamisi.

Pia Mwenyekiti wa Kituo cha Kufundisha Michezo Tanzania (TSTC), Bw. Dennis Makoi ambaye alishirikiana na kituo cha dogodogo kumtafutia ufadhili Hamisi nchini Marekani, ametoa shukrani zake za dhati kwa familia ya Bw. na Bi. Amy Canady wa huko Marekana kwa ufadhili  na kusaidia kufanikisha ushindi huo. Hivi sasa Hamisi anaendelea na masomo nchini Marekani.

Msajili wa Michezo Aisajili Katiba ya TFF

$
0
0

Leodger Tenga

RAIS wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Leodegar Tenga amemshukuru Msajili wa Klabu na Vyama vya Michezo nchini kwa kusajili Katiba ya TFF toleo la 2013 kutokana na marekebisho yaliyofanywa na Mkutano Mkuu Maalumu uliofanyika Julai 13 mwaka huu.

Akizungumza na Waandishi wa Habari, Dar es Salaam leo (Agosti 5 mwaka huu), Rais Tenga ameishukuru Serikali, Msajili, Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara, Naibu wake Amos Makala na Baraza la Michezo la Taifa (BMT) kwa ushirikiano ambao wametoa kwa TFF katika kufanikisha suala hilo.

Amesema baada ya kupokea usajili huo, kinachofuata ni Katibu Mkuu wa TFF kumwandikia rasmi Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ili aanzishe mchakato wa uchaguzi wa viongozi wa TFF.

Kuhusu kauli ya Naibu Waziri Makala kuwa marekebisho hayo yasingeweza kusajiliwa kwa sababu hayakufuata Katiba ya TFF, Rais Tenga amesema alikuwa ana haki ya kusema hivyo kwa sababu hakuwepo kwenye Mkutano huo, na kuongeza:

“Makala hakuwepo kwenye mkutano ndiyo maana alisema hivyo. Ana haki ya kuuliza, nina hakika sasa atakuwa ameeleweshwa na ameelewa kwa sababu ni msikivu. Kuhusu marekebisho hayo kupigiwa kura, hilo lisingewefanyika kwa sababu hakukuwa na mjumbe aliyepinga marekebisho,” amesema.

Rais Tenga amesema marekebisho hayo yalipitishwa kwa kauli moja (unanimous) hivyo hakukuwa na sababu ya kuanza kunyoosha mikono kupiga kura, kwa maana hiyo mkutano ulipitisha marekebisho kwa asilimia 100 wakati Katiba ilikuwa ikihitaji theluthi mbili tu.

“Hakukuwa na dispute (mabishano) kuhusu marekebisho, isipokuwa wajumbe walitumia muda mwingi kuboresha kanuni na kutoa ushauri wa aina ya watu ambao wangeingia kwenye kamati mbalimbali zikiwemo zile mpya za Maadili,” amesema.

Ameongeza kuwa kwa vile wote walioingia kwenye Mkutano Mkuu huo Maalumu ni watu wa mpira wa miguu wasingeweza kupinga marekebisho kwa vile yametokana na maagizo ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA).

“Labda itokee aliyeingia kwenye mkutano alikosea njia. Mtu yeyote wa mpira wa miguu ni lazima afahamu kuwa maagizo ya FIFA ni lazima yatekelezwe, na Katiba ya TFF inasema hivyo,” amesema Rais Tenga.

Pia Rais Tenga amewataka wapenzi wa mpira wa miguu kushawishi watu wenye sifa na uwezo wa kuongoza kujitokeza kwa wingi wakati Kamati ya Uchaguzi itakapotangaza mchakato na tarehe ya uchaguzi huo.

AZAM YAANZA ZIARA KWA KUIKABILI KAISER CHIEFS
Makamu bingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), Azam wanaanza rasmi ziara ya mechi za kirafiki nchini Afrika Kusini leo kwa kuikabili timu ya Kaiser Chiefs ambayo inacheza Ligi Kuu ya nchi hiyo (PSL).

Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Azam, Jaffer Idd aliyefutana na timu hiyo, mechi hiyo inachezwa jijini Johannesburg. Idd anapatikana kwa namba +27788847399.

*Imeandaliwa na Boniface Wambura, Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

Redds’s Miss Ilala Talent Kufanyika Leo

$
0
0

Redds’s Miss Ilala Talent Kufanyika Leo


Na Mwandishi Wetu

KATIKA Kuelekea Redds Miss Ilala Ijumaa, leo kutakuwa na shindano la kumtafuta mrembo mwenye kipaji (Talent) itakayofanyika katika mgahawa wa City Sports and Lounge uliopo katikati ya jiji.
Mratibu wa shindano hilo, Juma Mabakila alisema kuwa maandalizi ya kuelekea shindano hilo yanaendelea vizuri na kueleza kuwa warembo wote 14 wamejipanga kuonesha vipaji vyao ipasavyo.
Mabakila alisema mshindi wa talent atakabidhiwa zawadi zake kwenye fainali ya shindano hilo ambalo litafanyika Ijumaa ijayo katika ukumbi wa Golden Jubilee Tower ulipo katikati ya jiji.

Mratibu huyo wa Ilala alisema mbali ya burudani hiyo, pia watatumia nafasi hiyo kuuza ticket za VIP ambazo ni chache kwa watu maalum, lakini kutakuwa na bahati nasibu itakayotoa pasi za bure za kusingia katika onesho la Ijumaa.

Alisema kwamba shindano la mwaka huu litaandika historia mpya ya urembo kwa wilaya ya Ilala maana wamejipanga na kupata sapoti ya kutosha, hivyo mashabiki wa mashindano ya urembo wakae mkao wa kupata raha.

“Tumejipanga vizuri kuonesha shoo nzuri kuanzia hii ya telent na ile kubwa Ijumaa, kutakuwa na vitu tofauti na ilivyokuwa mwaka jana, kweli mambo yanakwenda vizuri,” alisema Mabakila.
Mashindano ya Redd’s Miss Ilala yamedhaminiwa na Redd’s Original, magazeti ya Jambo Leo, Tanzania Daima, Smile, CXC Safaris, Blog ya wananchi, Fredito na Dodoma wine.

Yajue Matukio Tamasha la Serengeti Fiesta Mjini Kigoma

$
0
0

Mwananmuziki mkongwe wa bongo flava Ambwene Yesaya akitumbuiza wakazi wa mji wa kigoma katika tamasha la Serengeti Fiesta mjini Kigoma katika uwanja wa Lake Tanganyika. Tamasha hilo linadhaminiwa na kampuni ya bia ya Serengeti Kupitia bia yake ya Serengeti Premium Lager.

Wanamuziki wa kutoka TMK Family Chege (kulia) na Temba (kushoto) wakitumbuiza wakazi wa mji wa kigoma katika tamasha la Serengeti Fiesta mjini Kigoma katika uwanja wa Lake Tanganyika. Tamasha hilo linadhaminiwa na kampuni ya bia ya Serengeti Kupitia bia yake ya Serengeti Premium Lager.

Mwananmuziki mahiri wa miziki ya pwani Shilole akitumbuiza wakazi wa mji wa kigoma katika tamasha la Serengeti Fiesta mjini Kigoma katika uwanja wa Lake Tanganyika. Tamasha hilo linadhaminiwa na kampuni ya bia ya Serengeti Kupitia bia yake ya Serengeti Premium Lager.

Mwananmuziki mkongwe wa bongo flava Mwana FA akitumbuiza wakazi wa mji wa kigoma katika tamasha la Serengeti Fiesta mjini Kigoma katika uwanja wa Lake Tanganyika. Tamasha hilo linadhaminiwa na kampuni ya bia ya Serengeti Kupitia bia yake ya Serengeti Premium Lager.

Baadhi ya madada ‘warembo’ wa Mjini Kigoma katika wakiwa kwenye Tamasha la Serengeti Fiesta katika uwanja wa Lake Tanganyika. Tamasha hilo linadhaminiwa na kampuni ya bia ya Serengeti Kupitia bia yake ya Serengeti Premium Lager.

Ushauri wa Bure Kwa Msanii Dully Sykes na Watanzania Wenzangu!

$
0
0

20130826-124153.jpg

Mwanamuziki mkongwe wa Bongo Fleva, Dully Sykes

Jana nilitembelea mtandao wa Ankal Michuzi (ndio wana Blogu huwa tunatembeleana kubadilishana uzoefu -:))na baada ya kupita hapa na pale, nikakumbana na habari, iliyoambatana na video tatu kutoka Tanzania Film Critics Association (TFCA). Video hizi http://issamichuzi.blogspot.de/search?updated-max=2013-08-25T12:49:00%2B03:00 zilikuwa za mahojiano ya wasanii watutu, yaani John Kitime, Dr. vicensia Shule, na Dully Skyes. Sikuwa na muda mwingi kutokana na majukumu ya kazi, hivyo niliweza kuangalia video mbili tu mpaka mwisho, nazo ni ile ya John Kitime na Dully Sykes. Baada ya kuangalia video za mahojiano hayo yaliyohusu sheria ya ushuru wa bidhaa, sura 147, nilishindwa kujizuia na hivyo kulazimika kuandika maoni yafuatayo (chini) kwenye blog ya michuzi kwa maslahi ya Msanii wetu mahiri Dully Sykes na Watanzania wenzangu:

Maoni haya nimeyaongeza kidogo, ili kukidhi mahitaji ya mtandao wetu na wasomaji wake.
…………………………………………..

Dully Sykes, kwanza napenda kuanza kwa kusema kwamba nakuheshimu kama miongoni mwa wanamuziki wa mwanzo wa Bongo Flava, ambao mmechangia sana kuukuza mziki wetu huu tuupendao, na hongera sana kwa kuendeleza mapambano mpaka sasa, kwani miaka 17 ya muziki si haba!

Baada ya hayo, ni muhimu nikaweka wazi kwamba maelezo yako katika mahojiano haya, yamenisikitisha sana, yaani unaonekana ni mtu wa lawama na kutaka kusaidiwa tu, bila kuwa tayari kubeba majukumu yako binafsi katika kuhakikisha maslahi yako yanalindwa.

Nazungumzia ‘responsibility’, ambayo hauonyeshi kuwa nayo, kwa mfano, haujui hata alama zinazotumika kulinda kazi zenu, na wala haujui kazi za wasanii zinalindwa vipi (wakati wewe ni msanii)???? Ukiulizwa kwanini, unasema “Mimi sijapata elimu yeyote na wala sikuitwa” sasa kwanini usifuatilie mwenyewe na kuweza kujielimisha na kujilinda? Maana mwisho wa siku, ni wewe ndio unayeibiwa na si BASATA wala COSOTA. Au ina maana ukongwe wako katika muziki huu na jina lako kubwa vina kuzuia kuwa fuata watu, mpaka ufuatwe au uitwe?

Amka Dully na wasanii wengine kwa kujielimisha wenyewe kwa kufuata hizo elimu zilipo na si kusubiri tu “kuelimishwa” na kusaidiwa na serikali na maadvocate!

Natambua kwamba mnafanya kazi katika mazingira magumu sana, maana wasanii wanashindwa kunufaika na kazi zao ipasavyo kutokana na wizi uliokithiri. Lakini, ufumbuzi wa tatizo hili hauwezi kupatikana bila wasanii wenyewe kuchukua jukumu la kujielimisha na kufuatilia mambo yote yanayohusiana na ulindaji wa kazi zao, kwani mhusika wa kwanza ni msanii mwenyewe. Kama msanii upo busy kiasi cha kushindwa kufuatilia masuala haya, basi bila shaka upo busy unatengeneza pesa.

Kwahiyo basi, hakikisha kwamba una Meneja makini, ambaye atafuatilia masuala haya kwa niaba yako na baadae fursa ikipatikana mnakutana ili akuelimishe na wewe pia. Ni jitihada hizi tu ndio zitakazo tunasua katika janga hili.

Huu ni ushauri kwa Watanzania wenzangu wengine wengi tu katika nyanja mbalimbali, ambao tumezoea kulalamika, bila kuchukua hatua zipasazo kumaliza matatizo yetu. Kwa mfano, Ndg. John kitime katika mahojiano yaleyale, ambayo alifanyiwa Dully Sykes pia. Yeye alisisitiza suala la umoja, yaani kuanzisha vitu kama vyama vya wafanyakazi, wasanii, na kadhalika….katika kudai maslahi yetu. Hili ni muhimu sana na ninaliunga mkono kwa nguvu zote, kwani kinachoendelea sasa miongoni wa wasanii na wengineo ni mparaganyiko, ambao unaacha pengo kubwa katika uwakilishi wa matatizo. Kama watu watajielimisha na kuwa pamoja, serikali italazimika tu kusikiliza na kuchukua hatua dhidi ya matatizo husika.

Lakini serikali ikiona mgawanyiko na uelewa mdogo, basi ina kuwa rahisi kwake kulifumbia macho suala fulani au kugeuza mradi wa maslahi ya wachache.

Ni ushauri wa bure tu.

Asanteni,

Rungwe Jr.


Hawa Ndio Warembo wa Redds Miss Tanzania 2013

$
0
0

Clara Bayo

WASHIRIKI wa shindano la Redd’s Miss Tanzania leo watapata fursa ya kumjua mrembo wa kwanza kuingia katika hatua ya Nusu fainali ya Shindano la Redd’s Miss Tanzania 2013 wakati mrembo mmoja kati ya wanyange hao 30 atakapotajwa mshindi wa Miss Photogenic 2013.
Shindano  hilo no moja kati ya mataji matano ambayo yanashindaniwa na warembo hao  ambapo washindi wake wanapata tiketi ya kuingia Nusufainali ya shindano hilo litakalo fanyika baadae mwezi ujao. Miongoni mwa mataji hayo ni Miss Tanzania Photogenic, Miss Tanzania Top Model, Miss Tanzania Personality, Miss Tanzania Sports Lady na Miss Tanzania Talent.
Akizungumza na Father Kidevu Blog, Mkurugenzi wa Lino International Agency, Waandaaji wa Shindano la Miss Tanzania, Hashim Lundenga ‘Uncle’ amesema jopo la majaji watatu ambao ni wapiga picha na wanahabari wazoefu wa masuala ya urembo Tanzania watakaa na kuchagua mshindi huyo kupitia picha mbalimbali za warembo hao.
Mshindi anataraji kutangazwa leo jioni katika hoteli ya Giraffe Ocean View na kujipatia tiketi hiyo. Taji la Redd’s Miss Tanania Photogenic  linashikiliwa na Mrembo Lucy Stephano aliyelitwaa mwaka 2012. Wafuatao ndio warembo watakao wania taji hilo hii leo.

 ESHYA RASHID
JANETH AWET
 HAPPINESS WATIMANYWA
CLARA BAYO
DORICE MOLLEL
 LATIFA MOHAMED
SALSHA ISDORY
 PRISCA PAUL
 LUCY TOMEKA
SEVERINA LWINGA

 SABRINA JUMA

 MIRIAM MANYANGA

LINA ALLAN

 LUCY JAMES

 

GLORY STEPHEN

 NEEMA SHAYO

 ALICE ISAACK

 SARAH PAUL

 PHILLIOS LEMI

 

NANCY MOSHI

 JACLINE LUVANDA

 DIANA LAIZER

 LUCY CHARLES

 SVETLANA NYAMEYO

 

NARIETHA BONIFACE

 MARY CHEMPONDA

 NICE JACK HERMAN

ANASTAZIA DONALD

 NEEMA MALITI

ELIZABETH PERTY

TAIFA STARS INATAFUTA NAFASI YA PILI- KIM

$
0
0

20130904-074743.jpg

Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen amesema wanaipa umuhimu mkubwa mechi ya mwisho ya mchujo ya Kombe la Dunia dhidi ya Gambia kwa lengo ni kuhakikisha wanamaliza wakiwa wa pili katika kundi hilo.

Mechi hiyo itachezwa Septemba 7 mwaka huu jijini Banjul, Gambia ambapo Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premiem Lager itaondoka kesho (Septemba 4 mwaka huu) saa 11 alfajiri kwa ndege ya Kenya Airways kupitia Dakar, Senegal.

Kim amesema wanataka kushinda ugenini, kwani licha ya kuwa wameshatolewa lakini ushindi utawaongezea pointi kwa ajili ya viwango (rankings) vya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) na pia kuepuka kuanzia ngazi ya awali ya mechi za mchujo za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) kwa fainali za 2015.

“Tunacheza mechi hii tukiwa katika mazingira magumu, kwani wengi wa wachezaji wa kikosi cha kwanza ni majeruhi. Sijawahi kukutana na hali hii tangu nilipoanza kuifundisha Taifa Stars, lakini tumejipanga kuhakikisha tunafanya vizuri,” amesema Kim.

Amesema kwa mipango ya timu yake mechi hiyo ni muhimu tofauti na wengi wanavyofikiria, na uamuzi wake wa kumwita beki Henry Joseph amezingatia mambo mengi ya kiufundi ikiwemo nafasi anayocheza na uzoefu wa mchezaji aliyekuwa akicheza nchini Norway katika klabu ya Kongsvinger IL.

Wachezaji majeruhi katika kikosi hicho ni Shomari Kapombe, Kelvin Yondani, Aggrey Morris, Salum Abubakar, Athuman Idd na John Bocco.

Vilevile wachezaji Mbwana Samata na Thomas Ulimwengu hawatakuwemo kwenye safari baada ya klabu yao ya TP Mazembe kutuma taarifa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) leo mchana ikidai ni wagonjwa.
Wachezaji wanaoondoka kwenda Banjul ni Juma Kaseja, Mwadini Ali, Ali Mustafa, Amri Kiemba, David Luhende, David Mwantika, Erasto Nyoni, Frank Domayo, Haruni Chanongo, Henry Joseph, Jonas Mkude, Juma Liuzio, Khamis Mcha, Mrisho Ngasa, Nadir Haroub, Said Dilunga, Simon Msuva na Vincent Barnabas.

40 WAPITISHWA KUGOMBEA TFF, BODI YA LIGI
Kamati ya Uchaguzi imepitisha majina ya waombaji 40 kati ya 58 kwa ajili ya uchaguzi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na Bodi ya Ligi Tanzania (TPL Board) utakaofanyika mwezi ujao.

Waliopitishwa katika orodha hiyo ya awali kwa upande wa Bodi ya Ligi ni Hamad Yahya Juma (Mwenyekiti) na Said Muhammad Said Abeid (Makamu Mwenyekiti).

Kwa upande wa Kamati ya Uendeshaji (Management Committee) ni Kazimoto Miraji Muzo na Omar Khatib Mwindadi. Walioondolewa kwa vile si wenyeviti wa klabu za daraja la kwanza kama kanuni zinavyotaka ni Michael Njuweni Kaijage, Salum Seif Rupia na Silas Masui Magunguma.

Kanda namba moja (Kagera na Geita) aliyepitishwa kuwania nafasi ya ujumbe Kamati ya Utendaji ya TFF ni Kaliro Samson wakati Abdallah Hussein Musa ameondolewa kwa kutojaza fomu ya uchaguzi kwa mujibu wa Kanuni za Uchaguzi.

Jumbe Oddessa Magati, Mugisha Galibona na Vedastus Lufano wamepitishwa kuwania ujumbe kupitia Kanda namba mbili (Mara na Mwanza). Samwel Nyalla ameondolewa kwa kutojaza kikamilifu fomu namba 1 ya maombi ya kugombea uongozi wa TFF kwa kutoonesha malengo yake.

Waliopitishwa katika Kanda namba tatu (Shinyanga na Simiyu) ni Epaphra Swain a Mbasha Matutu wakati Stanslaus Nyongo ameondolewa kwa kukosa sifa ya uongozi wa angalau uzoefu wa miaka mitano kwa mujibu wa Kanuni za Uchaguzi na Katiba ya TFF.

Kanda namba nne (Arusha na Manyara) wamepitishwa wote watatu; ambao ni Ali Mtumwa, Elley Simon Mbise na Omar Walii Ali. Kanda namba tano (Tabora na Kigoma) nao wamepitishwa wote; Ahmed Idd Mgoyi na Yusuf Hamis Kitumbo.

Blassy Kiondo amepitishwa peke yake kuwania ujumbe Kanda namba sita (Katavi na Rukwa) huku Ayoub Nyaulingo aliondolewa kwa kutokuwa na uzoefu uliothibitika wa miaka mitano katika uongozi wa mpira wa miguu.

Naye Nazarius Kilungeja, Kamati ilikataa maombi yake ya kugombea ujumbe kutokana na vitendo vyake visivyo vya kimichezo ambavyo kwa kiasi kikubwa vilisababisha migogoro kwenye Mkoa wa Rukwa, hivyo suala lake litawasilishwa kwa Kamati ya Maadili kwa ajili ya hatua zaidi.

Kanda namba saba (Iringa na Mbeya) waliopitishwa ni David Samson Lugenge, John Exavery Kiteve na Lusekelo Elias Mwanjala. Cyprian Kuyava hakupitishwa kwa vile hana uzoefu wa uongozi kwa mujibu wa Katiba ya TFF huku Ayoub Shaib Nyenzi akiondolewa kwa kushindwa kuthibitisha uraia wake.

Elliud Peter Mvella ameondolewa kwa kushindwa kuheshimu Kanuni za Uwajibikaji wa Pamoja (collective responsibility) baada ya kushiriki kufanya uamuzi ndani ya Kamati ya Utendaji ya TFF bila ya kutaka msimamo wake wa kupinga uwekwe kwenye muhtasari na baadaye kuupinga uamuzi huo akiwa kwenye uongozi wa mkoa. Suala lake limewasilishwa katika Kamati ya Maadili kwa ajili ya hatua zaidi.

Waliopitishwa kuwania ujumbe kupitia Kanda namba nane (Njombe na Ruvuma) ni James Patrick Mhagama na Stanley William Lugenge wakati Kamanga Tambwe ameondolewa kwa vile alipatikana na hatia ya kushiriki kwenye tuhumu za rushwa kwa waamuzi na kufungiwa na TFF.

Kanda namba tisa (Lindi na Mtwara) waombaji wote watatu wameptishwa. Waombaji hao ni Athuman Kingome Kambi, Francis Kumba Ndulane na Zafarani Mzee Damoder. Pia waombaji wote wa Kanda namba kumi (Dodoma na Singida), Hussein Zuberi Mwamba, Stewart Ernest Masima na Charles Komba wamepitishwa.

Waombaji wanne kati ya watano wamepitishwa kwa Kanda namba 11 (Morogoro na Pwani). Waliopitishwa ni Farid Mbarak, Geofrey Nyange, Juma Abbas Pinto na Twahil Twaha Njoki.

Riziki Juma Majala ameondolewa kwa vile akiwa mtendaji mkuu wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Pwani (COREFA) alishindwa kusimamia Kanuni za Ligi kwa kuruhusu timu ambayo si mwanachama wa wanachama wa COREFA kucheza ligi, hivyo kusababisha mgogoro mkubwa kiasi cha mwananchi mmoja kufungua kesi ya kusimamisha Ligi ya Mabingwa wa Mikoa (RCL). Suala lake litawasilishwa Kamati ya Maadili kwa ajili ya hatua zaidi.

Kanda namba 12 (Kilimanjaro na Tanga) wamepitishwa waombaji wote wawili. Waombaji hao ni Davis Elisa Mosha na Khalid Abdallah Mohamed. Waombaji wawili kati ya watano wamepitishwa kuwania ujumbe kupitia Kanda namba 13 (Dar es Salaam).

Wagombea wawili kati ya watano wamepitishwa kuwania ujumbe kupitia Kanda namba 13 (Dar es Salaam). Wagombea hao ni Alex Crispine Kamuzelya na Muhsin Said Balhabou.

Walioondolewa ni Omar Isaack Abdulkadir kutokana na vitendo vyake vya kutoheshimu na kutotekeleza maagizo ya TFF kwa mujibu wa Kanuni za Uchaguzi na Katiba ya TFF. Atapelekwa katika Kamati ya Maadili kwa hatua zaidi.

Shaffii Kajuna Dauda ameondolewa kwa kutumia nyaraka ya mawasiliano baina ya FIFA na Rais wa TFF bila idhini na kuiweka hadharani kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii, hivyo kukiuka maadili kwa kumiliki nyaraka ambazo hazikuwa kwenye mamlaka yake. Suala lake linapelekwa katika Kamati ya Maadili.

Naye Wilfred Kidao ameondolewa kwa kutumia nyaraka za Kamati ya Utendaji ya TFF bila ridhaa ya kamati, hivyo kukosa uadilifu. Suala lake linawasilishwa kwenye Kamati ya Maadili kwa hatua zaidi.

Kwa upande wa nafasi ya Makamu wa Rais, waombaji wote watatu wamepitishwa. Waombaji hao ni Imani Omari Madega, Ramadhan Omari Nassib na Wallace John Karia.

Athuman Jumanne Nyamlani na Jamal Emil Malinzi wamepitishwa kuwania nafasi ya Rais. Omari Mussa Nkwaruro ameondolewa kwa kuwasilisha cheti chenye utata, hivyo kukiuka utashi wa Ibara ya 27(7) ya Katiba ya TFF. Pia aliwasilisha taarifa za uongo kuhusu uzoefu na kukiuka Kanuni za Maadili, hivyo suala lake linapelekwa Kamati ya Maadili.

Naye Richard Julius Rukambula ameondolewa kwa hakukidhi matakwa ya kugombea uongozi kwa mujibu wa Ibara ya 12(2)(e) ya Katiba ya TFF inayokataza masuala ya mpira wa miguu kupelekwa katika mahakama za kawaida. Hivyo naye anapelekwa katika Kamati ya Maadili kwa hatua stahiki.

IRINGA YAINYANYASA RUVUMA COPA COCA-COLA
Iringa imeanza kwa kishindo michuano ya Copa Coca-Cola kwa watoto wenye umri chini ya miaka 15 baada ya leo (Septemba 3 mwaka huu) kuitandika Ruvuma mabao 4-0.

Hadi mapumziko katika mechi hiyo iliyochezwa Uwanja wa Shule ya Sekondari Iyunga jijini Mbeya, washindi walikuwa mbele kwa mabao 2-0 yaliyofungwa dakika ya 14 na Justin Luvanda huku Alphonce Kalinga akifunga la pili dakika ya 43.

Mabao mengine yalifungwa na Juma Rogani katika dakika ya 49 na Luvanda akafumania tena nyavu dakika ya 59.

Hiyo ni mechi ya pili mfululizo kwa Ruvuma kupoteza ambapo ya kwanza ililala mbele ya wenyeji Mbeya kwa mabao 3-0.

Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF

Mashindano ya Golf ya Kombe la Waitara 2013

$
0
0
Steve Gannon akimkabidhi kombe  mshindi wa kwanza wa Div B Shabani Kibuna kutoka Club ya Lugalo

Steve Gannon akimkabidhi kombe mshindi wa kwanza wa Div B Shabani Kibuna kutoka Club ya Lugalo

Rais wa awamu ya pili Mh. Ali  Hasan Mwinyi akipiga mpira  kuashiria kufunga mashindano ya golf ya Waitara  Trophy 2013 mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam

Rais wa awamu ya pili Mh. Ali Hasan Mwinyi akipiga mpira kuashiria kufunga mashindano ya golf ya Waitara Trophy 2013 mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.

Mh. Al Hajji Ali Hassan Mwinyi  akimkabidhi zawadi na kikombe cha ushindi mshindi wa jumla wa mashindano ya  golf ya Waitara Trophy Nevile Cory kutoka Afrika Kusini nwishoni mwa wiki  jijini Dar es Salaam
Mh. Al Hajji Ali Hassan Mwinyi akimkabidhi zawadi na kikombe cha ushindi mshindi wa jumla wa mashindano ya golf ya Waitara Trophy Nevile Cory kutoka Afrika Kusini nwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.

Muasisi wa mashindano ya Waitara   Cup akimkabidhi zawadi Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia ya Serengeti  Steve Gannon ambao ni wadhamini wakuu wa mashindano hayo kupitia kinywaji  chake cha Johnie Walker
Muasisi wa mashindano ya Waitara Cup akimkabidhi zawadi Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia ya Serengeti Steve Gannon ambao ni wadhamini wakuu wa mashindano hayo kupitia kinywaji chake cha Johnie Walker”.

Steve Gannon

 

Steve Gannon

Bodi ya Ligi Yaanza Kutoa Makali, Yavifungia Viwanja Saba, Wachezaji Wafungiwa…!

$
0
0
Bodi ya Ligi Yaanza Kutoa Makali, Yavifungia Viwanja Saba, Wachezaji Wafungiwa...!

Bodi ya Ligi Yaanza Kutoa Makali, Yavifungia Viwanja Saba, Wachezaji Wafungiwa…!

BODI ya Ligi Kuu Tanzania (TPL Board) imefungia viwanja saba vilivyokuwa vikitumiwa na timu za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) na Ligi Daraja la Kwanza (FDL) hadi vitakapofanyiwa marekebisho ili kukidhi mahitaji ya mechi za mpira wa miguu.

Uamuzi huo umefikiwa na TPL Board katika kikao chake cha kwanza kilichofanyika juzi (Novemba 10 mwaka huu) jijini Dar es Salaam ambapo pamoja na mambo mengine kilipitia ripoti za mechi za VPL na FDL katika mzunguko wa kwanza.

Viwanja vilivyofungiwa na marekebisho yanayotakiwa kufanyika kwanza ili viruhusiwe kutumika tena ni Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba (majukwaa yake yamechakaa, hivyo kuhatarisha usalama wa watazamaji), na Uwanja wa CCM Mkwakwani jijini Tanga (vyumba vya wachezaji kubadilishia nguo (dressing rooms) havina hadhi).

Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya (sehemu ya kuchezea- pitch ni mbovu), Uwanja wa Kumbukumbu ya Sheikh Kaluta Amri Abeid jijini Arusha (pitch ni mbovu), Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi (vyumba vya kubadilishia kutumika kwa ajili ya shule ya awali), Uwanja wa Majimaji mjini Songea (pitch ni mbovu) na Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro (pitch ni mbovu).

Klabu ambazo timu zake zinatumia viwanja hivyo zimeshaarifiwa rasmi juu ya uamuzi huo ambapo ama vinatakiwa kuwasiliana na wamiliki wa viwanja hivyo ili wafanye marekebisho au kutafuta viwanja vingine vya kuchezea mechi zao.

Kwa upande wa ripoti za mechi za VPL; Mbeya City imepigwa faini ya sh. 500,000 na kupewa onyo kali kwa timu yake ya U20 kutocheza mechi ya utangulizi walipocheza na Yanga. Pia wanatakiwa kulipa gharama za uharibifu baada ya washabiki wao kuvunja kioo cha basi la Yanga baada ya gharama hizo kuthibitishwa na Bodi ya Ligi.

Pia Mbeya City imepigwa faini ya sh. 500,000 kwa washabiki wake kushambulia basi la wachezaji wa Tanzania Prisons baada ya mechi dhidi yao, na kulipa gharama za uharibifu baada ya kuthibitisha na Bodi ya Ligi.

Coastal Union imepigwa faini ya sh. 500,000 kutokana na vurugu za washabiki wake ilipocheza na Azam kwenye Uwanja wa Mkwakwani ambapo mwamuzi msaidizi Hassan Zani alishambuliwa kwa mawe na kujeruhiwa mkononi na kichwa, tukio lililosababisha mchezo kusimama kwa dakika tatu.

Beki wa Coastal Union, Hamad Khamis wa Coastal Union amepigwa faini ya sh. 500,000 kwa kumpiga kichwa kwa makusudi Kipre Tchetche wa Azam. Kitendo hicho kilisababisha refa amtoe nje kwa kadi nyekundu, hivyo atakosa mechi tatu zinazofuata za timu yake.

Mchezaji Cosmas Lewis wa Ruvu Shooting alifanya kitendo cha utovu wa nidhamu kwa kupiga kelele wakati mgeni rasmi akisalimia timu na kukataa kupeana mkono na kamishna kwenye mechi dhidi ya Rhino Rangers, hivyo amefungiwa mechi tatu na kupigwa faini ya sh. 500,000.

Mtunza vifaa (Kit Man) wa JKT Ruvu, Selemani Oga aliondolewa kwenye benchi la ufundi wakati wa mechi yao dhidi ya Mbeya City kwa kosa la kutoa lugha chafu kwa refa, hivyo suala lake litapelekwa katika Kamati ya Maadili.

Kocha Msaidizi wa Oljoro JKT, Fikiri Elias amepigwa faini ya sh. 500,000 na kufungiwa mechi tatu kwa kumshambulia kwa matusi refa wakati wa mechi yao dhidi ya Ashanti United. Naye mtunza vifaa wa timu hiyo Elas Justin amepelekwa Kamati ya Maadili kwa kumshambulia refa kwa matusi ya nguoni.

Simba wamepigwa faini ya sh. 500,000 kutokana na vurugu za washabiki wake wakati wa mechi dhidi ya Kagera Sugar.

Katika FDL, mchezaji Ally Mtoni wa Villa Squad amepigwa faini y ash. 200,000 na kufungiwa mechi tano. Kosa lake ni kujisaidia haja ndogo golini wakti wa mechi dhidi ya Ndanda FC iliyochezwa mjini Mtwara.

Kamishna Paul Opiyo wa mechi ya FDL kati ya Villa Squad na Transit Camp kwa kutokuwa makini. Katika ripoti yake ameeleza kuwa Transit Camp ilichelewa kufika uwanjani, lakini hakusema ilichelewa kwa muda gani.

Kocha wa Polisi Dar es Salaam, Ngelo Nyanjabha na Meneja wa timu hiyo Mrimi Masi wamepigwa faini ya sh. 200,000 na kufungiwa mechi tatu kila mmoja kwa kuongoza kundi la washabiki kumvamia refa wa mechi yao dhidi ya Villa Squad iliyochezwa Dar es Salaam.

Pia Bodi ya Ligi imeagiza Polisi waandikiwe barua ya onyo kwa vile wakati waamuzi wanapigwa walikuwepo lakini hawakutoa msaada kwa wakati.

Kocha wa Friends Rangers, Kheri Mzozo amepigwa faini ya sh. 200,000 na kufungiwa mechi sita kwa kosa la kumtukana refa na kutishia kuhamamisha washabiki waingie uwanjani kufanya fujo kwenye mechi dhidi ya Villa Squad.

Naye Kocha msaidizi wa timu ya Transit Camp, Haji Amiri amepigwa faini ya sh. 200,000 na kufungiwa mechi sita kwa kutoa lugha ya matusi kwa mwamuzi wa akida wakati wa mechi dhidi ya Friends Rangers.

Adhabu zote zimetolewa kwa mujibu wa kanuni. Pia Bodi ya Ligi imeahirisha kufanya uamuzi wa mechi kati ya Stand United na Kanembwa JKT iliyochezwa Uwanja wa Kambarage ili kukusanya taarifa zaidi. Mechi hiyo haikumalizika. Bodi ya Ligi itakutana tena Jumapili (Novemba 17 mwaka huu).

FUTURE TAIFA STARS vs TAIFA STARS UWANJANI KARUME
Timu za Taifa za Future Taifa Stars na Taifa Stars zinacheza kesho (Novemba 13 mwaka huu). Mechi hiyo ya kirafiki itafanyika Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume jijini Dar es Salaam kuanzia saa 10 kamili jioni.

Mechi hiyo ni maalumu kwa Benchi la Ufundi la Taifa Stars linaloongozwa na Kim Poulsen kuangalia wachezaji kumi kutoka Future Taifa Stars watakaoongezwa katika Taifa Stars tayari kwa mechi ya kirafiki ya kimataifa itakayochezwa Novemba 19 mwaka huu jijini Arusha.

Watazamaji 300 tu wataruhusiwa kushuhudia mechi hiyo kwa kiingilio cha sh. 5,000.
Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager imeingia kambini leo (Novemba 12 mwaka huu). Miongoni mwa wachezaji wanaotarajia kuripoti ni kipa Ivo Mapunda wa Gor Mahia.
Imeandaliwa na Boniface Wambura Mgoyo, Kaimu Katibu Mkuu
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania

Banana Zorro Excelled in the Swahili Form of R&B…!

$
0
0

Banana Zorro

Banana Zorro


Banana zoro and the B-Band

THE
son of Tanzanian legendary Dance singer Zahir Ali Zorro, Banana Zorro has excelled in the Swahili form of R&B that takes much attention on Spanish flamenco and African Zouk.

It all started when his father had a listen to a freestyle tape whereby one of the tracks caught his ear and asked his son who sung the track and he replied “Masiga and I”. He then asked them to do a recording session in his studio that produced two tracks namely ‘Anakudanganya’ and ‘Big Boss’ and with that gave birth to the group loveM meaning ‘Banana loves Masiga’.

After the massive popularity of ‘Anakudanganya’ and recording a few tracks under BloveM, he decided to do a solo project working with producers and fellow artists to record his own tracks like ‘Nimekuchagua Wewe’, ‘Mama Yangu’ featuring D-Knob, and ‘Hao hao’ featuring Mwanafalsafa produced by Mentor of the UK collective 2Point9. In 2002, he released his first album titled ‘Banana’ consisting of 13 tracks followed by ‘Subra’ in 2006.

Born Zahir Ally Zorro, Banana has won several prizes in music competitions such as the ‘Tanzania Pop Idol’ in 2003, ‘Best Male Artist’ in the 2004 Kilimanjaro Music Awards and his songs have been nominated in several music awards. Also he has been performing live with the Inafrika Band and hooked up with fellow R&B artists Bushoke and Soul n Faith duo to form their unit called “Sayari” [meaning ‘Planet’ in Swahili].
He opened the 2006 Kilimanjaro Music Awards Launch Party alongside the Jamaican group T.O.K. in Dar-es-salaam, made a mini-tour in the UK and recently dropped a track entitled ‘Mama Kumbena’. He formed his own band known as the B- BAND and he is the lead vocalist.

The band has gone ahead and recorded classical music such as NZELA , SUBIRA , BADO KIDOGO all in Swahili language. In the year 2010 during the Tanzanian Musical awards he was nominated and won the award of the best male singer.
www.bongo-kwanza.com

‘Ukiwataka FFU Lazima Uweke Ulinzi Mkali…’

$
0
0

FFU Band

PROMOTA wa muziki jijini Koloni Bw. Peter Betram (Mjerumani), amejikuta akiwekewa
masharti magumu katika juhudi zake za kutaka kuandaa onesho kubwa la muziki
katikati ya Jiji la Koloni, nchini Ujerumani. Kwa muda wa miaka miwili sasa poromota huyo amekuwa akiilalamikia Halmashauri ya Jiji la Koloni kwa kumwekea ngumu katika kuandaa onesho la muziki kwa visingizio anuai.

Kuanzia mwaka 2012 aliambiwa apeleke orodha ya bendi anazohitaji kuzipandisha jukwaani, baada ya kuonekana jina la Bendi ya Ngoma Africa katika orodha hiyo, Serikali ya jiji hilo ilimwagiza mtayarishaji wa onyesho hilo akubali kuingia gharama za ziada kwa ajili ya kuweka ulinzi kutoka na msongamano wa washabiki.

Hata hivyo alipewa sharti lingine kuwa onesho hilo liwe nje ya Mji na sio kitovuni mwa jiji, kutokana na kuepuka msongamano wa washabiki wa Ngoma Africa band aka FFU ughaibuni yenye uwezo wa kuvuta mashabiki wake. Poromota amejikuta akivimba macho na kutojua nini cha kufanya.

Wadaku walipomtafuta kiongozi wa Ngoma Africa band kamanda Ras Makunja kutaka kupata mtazamo wake, alijibu kuwa kikosi chake kipo tayari na wakati wowote ule watakapoitwa na poromota huyo, Ras akunja watafanya kazi. Pamoja na hayo alikiri kuwa muda wa miaka miwili Poromota amekuwa akiwapigia simu, na bendi ipo tayari kama matayarisho yatakamilika alisema Kamanda Ras Makunja.

Mdodosa habari alipo hoji suala la kulikoni kamanda kumiliki bundi katika himaya ya “Anunnaki Empire” Kamanda Ras Makunja alikata simu..!!! sijui kama aliishiwa chaji au aliondoka ki – FFU kwa mwendo wa kasi!? Any way tuwatafute kambini kwao  www.ngoma-africa.com 

Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mke wake Mama Salma Kikwete wakilakiwa kwa ngoma za kitamaduni mara baada ya kuwasili jijini Colombo, Sri Lanka, leo Novemba 14, 2013 tayari kwa mkutano wa wakuu wa nchi za jumuiya ya madola (CHOGM)
 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mke wake Mama Salma Kikwete wakiongea na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Defue mara baada ya kuwasili jijini Colombo, Sri Lanka, leo Novemba 14, 2013 tayari kwa mkutano wa wakuu wa nchi za jumuiya ya madola (CHOGM 
 

Kocha Mkuu Taifa Stars Awaita 32 Kupambana na Harambee Stars

$
0
0
Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen

Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen

KOCHA Mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen ameunda kikosi cha wachezaji 32 kwa ajili ya mechi ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya Kenya (Harambee Stars) itakayochezwa Jumanne, Novemba 19 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
 
Kikosi hicho kinajumuisha wachezaji 16 walioitwa Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager, na wengine 16 kutoka Future Taifa Stars. Awali kambi ya Future Taifa Stars iliyoanza Novemba 9 mwaka huu na kuvunjwa leo asubuhi ilikuwa na wachezaji 30.
 
Wachezaji walioitwa ni makipa wanne; Aishi Manula (Azam), Ally Mustafa (Yanga), Deogratias Munishi (Yanga) na Ivo Mapunda (Gor Mahia, Kenya). Mabeki ni Aggrey Morris (Azam), Ismail Gambo (Azam), Kelvin Yondani (Yanga), Michael Pius (Ruvu Shooting), Nadir Haroub (Yanga) na Said Moradi (Azam).
 
Viungo wakabaji ni Erasto Nyoni (Azam), Himid Mao (Azam), Shomari Kapombe (AC Cannes, Ufaransa) na Vincent Barnabas anayechezea Mtibwa Sugar ya Morogoro.
 
Viungo ni Amri Kiemba (Simba), Athuman Idd (Yanga), Frank Domayo (Yanga), Haruna Chanongo, Hassan Dilunga (Ruvu Shooting), Jonas Mkude (Simba), Ramadhan Singano (Simba), Salum Abubakar (Azam) na William Lucian (Simba).
 
Viungo washambuliaji ni Faridi Musa (Azam), Joseph Kimwaga (Azam), Mrisho Ngasa (Yanga), Mwingi Kazimoto (Markhiya, Qatar) na Simon Msuva (Yanga).
 
Washambuliaji ni Elias Maguli (Ruvu Shooting), Juma Liuzio (Mtibwa SugarMbwana Samata (TP Mazembe, DRC) na Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, DRC).
Imeandaliwa na Boniface Wambura Mgoyo, Kaimu Katibu Mkuu
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)


Ngoma Africa Band Kutumbuiza Mjini Bremen, Ujerumani

$
0
0
Ngoma Africa band aka FFU or Anunnaki Aliens

Ngoma Africa band aka FFU or Anunnaki Aliens

BENDI maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya “Ngoma Africa band” a.k.a FFU watarajiwa kutumbuiza usiku wa jumamosi 23.November 2013 katika ukumbi wa Übersee-Museum mjini Bremen, mchini Ujerumani.

Wakazi wa jiji la Bremen na miji ya jirani watapata burani ya kung’oa na sululu kutoka kwa mzimu wa muziki Ngoma Africa band ambayo maarufu sana kwa kuwatia kiwewe washabiki wake kila wapandapo jukwaani. Onyesho hilo limeandaliwa na makumbusho ya Oversee Museum ya jiji la Bremen kwa kushirikiana na Pan African Organization.

Ngoma Africa band wataanza kutumbuiza majira ya saa. 4.00 usiku na kabla ya hapo kutakuwa na maonyesho mbali mbali ya bidhaa za kiafrika,pamoja na vyakula. Bendi ya “Ngoma Africa” ambayo inadumu kwa muda wa miaka 20 imetajwa kuwa ndio bendi ya mwanzo ya kiafrika kufanikiwa kudumu katika medani ya muziki na kujizolea mamilioni ya washabiki katika kila kona duniani.

Watafiti wa mambo ya muziki wameitaja bendi hiyo kuwa inatumia kila nafasi waliyo nayo kuwanasa washabiki wake, na imetajwa mara nyingi kuwa ni bendi bora na kuchukuwa TUZO za kimataifa, ni bendi ambayo imepachikwa majina mengi mengi ya utani na kiusanii kama a.k.a “FFU Ughaibuni”, aka “Watoto wa mbwa” chini ya uongozi wake Kamanda Ras Makunja wa FFF, Mtawala wa
himaya ya ”Anunnaki Empire”

Usikose kuwasikiliza at www.ngoma-africa.com au http://www.ngoma-africa.com

Malinzi Kuzinduwa Michuano ya Uhai 2013

$
0
0
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi

RAIS wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi atafungua rasmi michuano ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 20 (U20) kwa klabu za Ligi Kuu ya Vodacom mwaka huu.
 
Uzinduzi wa mashindano hayo utafanyika kesho (Novemba 17 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Dar es Salaam saa 2 kamili asubuhi. Mechi ya ufunguzi itakuwa ya kundi A kati ya Azam na Coastal Union.
 
Mechi nyingine za kesho ni kundi; Yanga na Mbeya City (saa 8 mchana- Uwanja wa Karume), kundi B ni Ruvu Shooting na Ashanti United (saa 4 asubuhi- Uwanja wa Karume), Oljoro JKT na Simba (saa 10 jioni – Uwanja wa Karume).
 
Kundi C kutakuwa na mechi kati ya Kagera Sugar na Mtibwa Sugar itakayochezwa saa 2 kamili asubuhi kwenye Uwanja wa Azam Complex, na kwenye uwanja huo huo saa 10 jioni ni Rhino Rangers dhidi ya Tanzania Prisons.

RAMBIRAMBI MSIBA WA NYOTA COPA COCA-COLA

SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea kwa masikitiko kifo cha mchezaji wa Sayari, Fatuma Bahau ‘Crouch’ kilichotokea jana (Novemba 15 mwaka huu) kwenye Hospitali ya Temeke, Dar es Salaam.
 
Msiba huo ni mkubwa katika mpira wa miguu kwani Fatuma ndiyo kwanza alikuwa anachipukia katika mpira wa miguu wa wanawake ambapo alikuwa mfungaji bora wa michuano ya U15 Copa Coca-Cola ya mwaka huu akichezea timu ya Ilala, hivyo mchango wake katika mchezo huu tutaukumbuka daima.
 
Kwa mujibu wa mlezi wa mchezaji huyo, Stephania Kabumba, marehemu anasafirishwa kesho kwenda kwao Mwanza kwa ajili ya maziko ambapo kifo chake kimesababishwa na ugonjwa wa malaria.
 
TFF tunatoa pole kwa familia ya marehemu Bahau, klabu ya Sayari, Chama cha Mpira wa Miguu Wilaya ya Kinondoni (KIFA) na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) na kuwataka kuwa na subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha msiba huo mzito. Mungu aiweke roho ya marehemu Fatuma mahali pema peponi. Amina
 
*Imeandaliwa na Boniface Wambura Mgoyo, Kaimu Katibu Mkuu
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

Taifa Stars Sasa Kukipiga na Zimbabwe, Kiingilio Shs 5,000

$
0
0
Bendera ya Zimbabwe

Bendera ya Zimbabwe

TAIFA Stars sasa inacheza na Zimbabwe mechi ya Kalenda ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA)- FIFA Date itakayofanyika keshokutwa Jumanne (Novemba 19 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
 
Awali Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager ilikuwa icheze na Kenya (Harambee Stars), lakini Shirikisho la Mpira wa Miguu Kenya (FKF) lilituma taarifa jana jioni (Novemba 16 mwaka huu) likieleza kuwa timu yake haitacheza tena mechi hiyo.
 
Kikosi cha Zimbabwe chenye msafara wa watu 30 kinatarajia kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) kesho (saa 3 asubuhi) tayari kwa mechi hiyo itakayochezwa kuanzia saa 11 kamili jioni.
 
Waamuzi wa mechi hiyo wanatoka Uganda wakati Kamishna atakuwa Leslie Liunda wa Dar es Salaam. Mwamuzi wa mezani ni Oden Mbaga pia wa Dar es Salaam.
 
Stars chini ya Kocha Kim Poulsen ipo kambini tangu Novemba 12 mwaka huu kujiwinda kwa mechi hiyo. Kim amejumuisha kwenye kikosi chake wachezaji watano wanaocheza mpira wa miguu nje ya Tanzania.
 
…5,000/- NDIYO KIINGILIO CHA KUISHANGILIA STARS
Kiingilio katika mechi ya kirafiki ya kimataifa kati ya wenyeji Tanzania (Taifa Stars) na Zimbabwe ni sh. 5,000 wakati tiketi zitaanza kuuzwa Jumatatu (Novemba 18 mwaka huu) kwenye vituo mbalimbali jijini Dar es Salaam.
 
Mbali ya kiingilio hicho cha sh. 5,000 ambacho ni kwa viti vya bluu na kijani, viingilio vingine ni sh. 30,000 kwa VIP A, sh. 20,000 kwa VIP B, sh. 15,000 kwa VIP C wakati viti vya rangi ya chungwa ni sh. 10,000.
 
Tiketi zitauzwa katika magari maalumu katika vituo vya; Shule ya Sekondari Benjamin Mkapa, mgahawa wa Steers uliopo Mtaa wa Ohio na Samora, Sokoni Kariakoo, Dar Live Mbagala, OilCom Ubungo, BMM Salon iliyopo Sinza Madukani, Uwanja wa Uhuru, mgahawa wa Brake Point uliopo Kijitonyama, na kituo cha mafuta Buguruni.
*Imeandaliwa na Boniface Wambura Mgoyo, Kaimu Katibu Mkuu
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

Sensei Rumadha Fundi Azidi Kuwaimarisha Wapiga Karate Marekani

$
0
0

Sensei Rumadha Fundi Azidi Kuwaimarisha Wapiga Karate Marekani

Sensei Rumadha Fundi Azidi Kuwaimarisha Wapiga Karate Marekani


Sensei Rumadha Fundi Azidi Kuwaimarisha Wapiga Karate Marekani

Sensei Rumadha Fundi Azidi Kuwaimarisha Wapiga Karate Marekani

MTAALAMU wa michezo ya Karate na Yoga Mtanzania Sensei Rumadha Fundi siku ya jumamosi  November 16, 2013. Alitoa semina maalum ya mafunzo kuimarisha viungo kutumia vifaa asilia toka Okinawa ”Chishi na jar” kuimarisha miguu vidole na misuri yamapaja na miguu.

Mafunzo haya yana lengo la kuimarisha nguvu za mateke na utumiaji wa ngumi na kujenga msingi wa ”Kata” bora. Okinawa Goju Ryu Karate- Do ”Special training for weight and conditioning” Sugarland, Texas, USA.

Sensei Rumadha Fundi (Black belt, 3dan) ni mtaalamu wa mda mrefu katika michezo ya Karate ambaye alipata mafunzo ya mwanzo katika Dojo la Zanaki, jijini Dar- es- Salaam nchini ya mwalimu wake Marehem Sensei Nantambu Kamara Bomani.

Baadaye mafunzo ya Yoga nchini, Mafunzo ya juu na falsafa ya Goju Ryu kule Okinawa, Japan na kutunikiwa dan tatu. Sensei Rumadha Fundi ni mmoja wa wataalamu wa kiafrika wachache wanaokubalika kimataifa katika fani hii Karate. Pia ameweza kuendesha mafunzo na semina katika nchi mbali mbali duniani. SENSEI RUMADHA FUNDI KUTOKA USWAHILI NI MTALAAMU WA KUJIVUNIA KWA WATANZANIA

Kikosi cha Zimbabwe Kutua Mchana Dar Kuikabili Taifa Stars

$
0
0
Mechi ya Kalenda ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA)- FIFA Date

Mechi ya Kalenda ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA)- FIFA Date

KIKOSI cha Zimbabwe kinawasili leo mchana (Novemba 18 mwaka huu) kuikabili Taifa Stars katika mechi ya Kalenda ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA)- FIFA Date itakayofanyika kesho (Novemba 19 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
 
Msafara wa timu hiyo ukiwa na watu 30 utatua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) saa 8 kamili mchana kwa ndege ya Kenya Airways yenye mruko namba KQ 484 kupitia Nairobi.
 
Kocha wa timu hiyo Ian Gorowa atazungumza na waandishi wa habari mara baada ya timu hiyo kutua JNIA. Kiongozi wa msafara wa timu ya Zimbabwe ni John Phiri.
 
Wachezaji wanaounda kikosi hicho ni makipa; Frankson Busire, Maxwell Nyamupangedengu na Tapiwa Kapini. Mabeki ni Carrington Nyadombo, Felix Chindungwe, Innocent Mapuranga, Nkosana Siwela, Ocean Mushure na Patson Jaure.
 
Viungo ni Isaac Masami, Kundakwashe Mahachi, Milton Neube, Misheck Mburayi, Obey Mwenehari na Silas Dylan Songani. Washambuliaji ni Gerald Ndlovu, Lot Chiungwa, Nqobizitha Masuku, Simba Sithole na Themba Ndlovu.
 
Waamuzi wa mechi hiyo wanatoka Uganda wakati Kamishna atakuwa Leslie Liunda wa Dar es Salaam. Mwamuzi wa mezani ni Oden Mbaga pia wa Dar es Salaam.
 
Viingilio ni sh. 5,000 kwa viti vya rangi ya bluu na kijani, sh. 30,000 kwa VIP A, sh. 20,000 kwa VIP B, sh. 15,000 kwa VIP C wakati viti vya rangi ya chungwa ni sh. 10,000.
 
Tiketi zinauzwa kwenye magari maalumu katika vituo vya; Shule ya Sekondari Benjamin Mkapa, mgahawa wa Steers uliopo Mtaa wa Ohio na Samora, Dar Live Mbagala, OilCom Ubungo, Uwanja wa Uhuru, na kituo cha mafuta Buguruni.

*Imeandaliwa na Boniface Wambura Mgoyo, Kaimu Katibu Mkuu
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

Viewing all 521 articles
Browse latest View live