Quantcast
Channel: Michezo na Burudani – Tanzania Habari | Jamii | Michezo | Mahusiano | Kazi | Thehabari.com
Viewing all 521 articles
Browse latest View live

Jamal Malinzi Atangaza Kamati Ndogondogo za TFF

$
0
0
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi

RAIS wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi ametangaza wajumbe wa kamati ndogongo (standing committees) wakati zile za haki (judicial organs) na uchaguzi zitaundwa baadaye.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kikao cha Kamati ya Utendaji kilichofanyika leo (Novemba 23 mwaka huu) jijini Dar es Salaam, Rais Malinzi alisema kamati hizo zimeundwa kwa mujibu wa katiba ili kuisaidia Kamati ya Utendaji.

Pia ametangaza wajumbe wanne wa Kamati ya Utendaji aliowateua. Wajumbe hao ni Richard Sinamtwa na Ramadhan Nassib, wakati wengine wanaoingia moja kwa moja kwenye Kamati ya Utendaji kutokana na kamati wanazoziongoza ni Dk. Paul Marealle na Saloum Umande Chama.

Kamati ya Fedha na Mipango inaongozwa na Makamu wa Rais wa TFF, Wallace Karia wakati wajumbe ni Francis Ndulane (Makamu Mwenyekiti), Omari Walii, Eliud Mvella, Said Muhammed, Geofrey Nyange, Kidao Wilfred, Ayoub Nyenzi, Lina Kessy na Cyprian Kuhyava.

Geofrey Nyange anaongoza Kamati ya Mashindano wakati wajumbe ni Clement Sanga (Makamu Mwenyekiti), Msafiri Mgoyi, James Mhagama, Mohamed Nassoro, Moses Katabaro, Seif Ahmed, Gerald ambi, Davis Mosha, Said George na Nassoro Idrissa.

Kinara wa Kamati ya Ufundi ni Kidao Wilfred wakati wajumbe ni Athumani Kambi (Makamu Mwenyekiti), Vedstus Lufano, Blassy Kiondo, Rahim Kangezi, Patrick Kahemele, Daud Yassin, Nicholas Mihayo na Dk. Cyprian Maro.

Kamati ya Mpira wa Miguu wa Vijana inaongozwa na Ayoub Nyenzi, Khalid Abdallah (Makamu Mwenyekiti), Ali Mayay, Mulamu Ng’hambi, Apollo Kayungi, Said Tully, Luteni Kanali Charles Mbuge, Lameck Nyambaya na Ibrahim Masoud.

Lina Kessy anaongoza Kamati ya Mpira wa Miguu wa Wanawake wakati wajumbe ni Shyrose Bhanji (Makamu Mwenyekiti), Zena Chande, Amima Karuma, Dk. Cecilia Makafu, Zafarani Damoder, Beatrice Mgaya, Sofia Tigalyoma, Martin Mung’ong’o na Engrid Kimaro.

Kamati ya Waamuzi inaongozwa na Saloum Umande Chama, Nassoro Said (Makamu Mwenyekiti), Charles Ndagala (Katibu), Riziki Majala, Kanali Isaro Chacha, Paschal Chiganga, Victor Mwandike, Soud Abdi na Zahra Mohamed.

Hamad Yahya Juma ambaye ni Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi anaongoza Kamati ya Habari na Masoko wakati wajumbe ni Naibu Waziri January Makamba (Makamu Mwenyekiti), Tido Mhando, Yusuf Manji, Yusuf Bakhresa, Samwel Nyalla, Jack Gotham, Fredrick Mwakalebela na Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA).

Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji inaongozwa na Richard Sinaitwa, Moses Karuwa (Makamu Mwenyekiti), Zacharia Hanspoppe, Hussein Mwamba, Philemon Ntahilaja, Abdul Sauko na Imani Madega.

Kiongozi wa Kamati ya Ukaguzi wa Fedha ni Ramadhan Nassib wakati wajumbe ni Zitto Kabwe (Makamu Mwenyekiti), Nicholas Magarinza, Jackson Songora, Epaphra Swai, Kalilo Samson, Goodluck Moshi, Golden Sanga na Elias Mwanjala.

Dk. Paul Marealle anaongoza Kamati ya Tiba wakati wajumbe ni Dk. Fred Limbanga (Makamu Mwenyekiti), Dk. Mwanandi Mwankemwa, Dk. Nassoro Matuzya, Dk. Eliezer Ndelema na Asha Sadick.


TFF Yaingilia Simba, Yamtaka Rage Aitishe Mkutano

$
0
0
MWENYEKITI wa Simba, Ismail Aden Rage

MWENYEKITI wa Simba, Ismail Aden Rage

MWENYEKITI wa Simba, Ismail Aden Rage ameagizwa kuitisha Mkutano Mkuu wa Dharura wa klabu ndani ya siku 14 kuanzia sasa.

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetoa agizo hilo baada ya kubaini kuwa mgogoro katika klabu baada ya kupokea barua mbili; moja kutoka Kamati ya Utendaji ikielezea kumsimamisha uongozi Rage, na nyingine kutoka kwa Mwenyekiti huyo ikielezea kutotambua kusimamishwa huko.

Uamuzi wa TFF umefanywa kwa kuzingatia Ibara ya 1(6) ya Katiba ya Simba inayosema: “Simba Sports Club ni mwanachama wa TFF, itaheshimu Katiba, kanuni, maagizo na uamuzi wa TFF na FIFA, na kuhakikisha kuwa zinaheshimiwa na wanachama wake.”

TFF itatuma wawakilishi wake katika mkutano huo, na kumuagiza Mwenyekiti wa Simba kuhakikisha wanachama wote wenye hoja wanapata fursa ya kusikilizwa.

*Boniface Wambura Mgoyo, Kaimu Katibu Mkuu
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

Rage Aigomea TFF, Akifananisha Kikao Kilichomsimamisha na cha Harusi

$
0
0
Mwenyekiti wa klabu ya soka ya Simba, Ismail Aden

Mwenyekiti wa klabu ya soka ya Simba, Ismail Aden

Na Mwandishi Wetu,

MWENYEKITI wa klabu ya soka ya Simba, Ismail Aden Rage ameligomea Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kuitisha Mkutano Mkuu wa Dharura ndani ya siku 14. Rage ametoa kauli hiyo leo jijini Dar es Salaam alipokutana na waandishi wa Habari kuzungumzia agizo hilo la TFF pamoja na lile la Kamati ya Utendaji ya Simba iliyomsimamisha uenyekiti siku chache zilizopita.

“Kikao cha Kamati ya Utendaji kilichokaa na kuamua kunisimamisha ni batili kwa kuwa aliyeitisha mkutano huo hana mamlaka ya kufanya hivyo kwa Katiba ya Simba, hivyo ni sawa na kikao cha harusi,” alisema.

Alisema anaishangaa TFF kumpa siku 14 aitishe mkutano wa dharura wakati taasisi hiyo ilipaswa kupinga kitendo cha yeye kusimamishwa nafasi yake ya uenyekiti maamuzi yaliyofanyika kinyume na taratibu za michezo yaani kufanya mapinduzi.

Alisema kutokana na kukiukwa kwa Katiba ya TFF na klabu ya Simba, hatoitisha mkutano wowote kama alivyotakiwa ili naye asivunje Katiba na kama atalazimishwa kufanya hivyo yuko tayari kujiuzuru nafasi yake kuliko kusimamia kuvunja katiba.

Rage alitolea mfano wa msuguano uliotokea katika kipindi cha uchaguzi wa TFF ulioifanya Serikali kuingilia kati sanjari na Shirikisho la Mpira wa Miguu la Kimataifa (Fifa), alisema baada adha hiyo kutokea Fifa iliamuru TFF iitishe uchaguzi na kuwapangia tarehe na agenda.

Aliongeza kuwa kutokana na TFF kumuagiza kuitisha mkutano ndani ya Siku 14 pamoja na kumchagulia agenda ni kinyume cha Katiba ya TFF, hivyo hatoitisha mkutano kama alivyotakiwa na shirikisho hilo.

Hata hivyo Kaimu Katibu Mkuu wa TFF, Boniface Wambura alipotakiwa kufafanua ni hatua gani zitachukuliwa ikiwa Rage atagoma kuitisha Mkutano Mkuu wa Dharura kama alivyoagizwa, alisema wao bado wanasubiri siku 14 zikamilike ili kuchukua hatua nyingine za kuchukua endapo Rage hatotekeleza maagizo yao.

“Tunashukuru kuwa amekiri kupokea barua yetu, hivyo tunasubiri hadi siku 14 ziishe ndio itajulikana TFF nini itafanya dhidi yake, tusubiri muda uishe na leo ni siku ya pili,” alisema Wambura.

TFF juzi ilitoa agizo la kumtataka Rage aitishe Mkutano Mkuu wa dharura kwa kutumia Ibara 1(6) ya Katiba ya Simba inayosema, “Simba Sports Klub ni mwanachama wa TFF, itaheshimu Katiba, kanuni, maagizo na uamuzi wa TFF na Fifa na kuhakikisha kuwa zinaheshimiwa na wanachama wake.”

Rage katika mkutano huo, alimtangaza pia Richard Wambura kuwa ni mmoja wa wajumbe wa Kamati ya Utendaji wa klabu ya Simba. Akizungumzia suala la kusaini Mkataba na Azam TV alisema suala hilo halihitaji shule kwa kuwa mhusika Mkuu ni TFF, hivyo iwe isiwe ni lazima klabu isaini na ndio sababu alifanya hivyo miezi minne iliyopita na klabu kupewa mil 100.

Kilimanjaro Stars Kuagwa Kesho

$
0
0
Kaimu Katibu Mkuu Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Boniface Wambura Mgoyo

Kaimu Katibu Mkuu
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Boniface Wambura Mgoyo

KIKOSI cha Kilimanjaro Stars kinaagwa kesho (Novemba 25 mwaka huu) tayari kwa safari ya Nairobi, Kenya kushiriki michuano ya Kombe la Chalenji inayoanza kutimua vumbi Novemba 27 mwaka huu.

Hafla ya kuiaga timu hiyo itafanyika saa 5 asubuhi kambini kwao katika hoteli ya Accomondia jijini Dar es Salaam. Msafara wa Kilimanjaro Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager utaongozwa na Ahmed Idd Mgoyi. Timu itaondoka saa 10 alasiri kwa ndege ya RwandAir.

Wachezaji waliomo katika msafara huo ni makipa Deogratius Munishi (Yanga), Ivo Mapunda (Gor Mahia, Kenya) na Aishi Manula (Azam). Mabeki ni Erasto Nyoni (Azam), Himid Mao (Azam), Ismail Gambo (Azam), Kelvin Yondani (Yanga), Michael Pius (Ruvu Shooting) na Said Moradi (Azam).

Viungo ni Amri Kiemba (Simba), Athuman Idd (Yanga), Frank Domayo (Yanga), Haruna Chanongo (Simba), Hassan Dilunga (Ruvu Shooting), Ramadhan Singano (Simba) na Salum Abubakar (Azam).

Safu ya ushambuliaji inaundwa na Elias Maguli (Ruvu Shooting), Faridi Musa (Azam), Joseph Kimwaga (Azam), Juma Liuzio (Mtibwa Sugar), Mbwana Samata (TP Mazembe, DRC), Mrisho Ngasa (Yanga) na Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, DRC).

Hata hivyo, washambuliaji Samata na Ulimwengu watajiunga na timu hiyo jijini Nairobi, Desemba Mosi mwaka huu wakitokea Lubumbashi ambapo Novemba 30 mwaka huu TP Mazembe itacheza fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Benchi la Ufundi la timu hiyo linawajumuisha Kim Poulsen (Kocha Mkuu), Sylvester Marsh (Kocha Msaidizi), Juma Pondamali (Kocha wa Makipa), Leopold Tasso (Meneja wa Timu), Dk Mwanandi Mwankemwa (Daktari wa Timu), Frank Mhonda (mtaalamu wa tibamaungo) na Alfred Chimela (Mtunza Vifaa).

Kilimanjaro Stars ambayo ipo kundi B katika michuano hiyo itacheza mechi yake ya kwanza Novemba 28 mwaka dhidi ya Zambia kwenye Uwanja wa Machakos.

*Boniface Wambura Mgoyo, Kaimu Katibu Mkuu
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

FFU wa Ngoma Africa Band Waliteka Jiji la Bremen!

$
0
0
Wapenzi na washabiki wa ngoma Africa band ndani ya Ubersee museum Bremen

Wapenzi na washabiki wa ngoma Africa band ndani ya Ubersee museum Bremen

Bremen, Ujerumani

BENDI maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya Ngoma Africa band aka FFU ughaibuni, usiku tarehe 23 Novemba 2013 walifanikiwa kwa mara nyingine tena kuliteka jiji la Bremen, kule ujerumani. Kiongozi wa bendi hiyo kamanda Ras Makunja wa FFU alikiongoza jukwaani kikosi kazi chake katika jumba la Übersee-Museum akiwa na matumaini kuwa wanaenda kumbuiza washabiki high class wenye adhi ya kibwanyenye lakini mziki ulipoanza mdundo uliwachanganya washabiki na kuwadatisha akili! Kila mmoja alijimwaga uwanjani!

Ngoma Africa Band walijikuta wapo katika kibarua kama kawaida yao cha kushambulia kwa virungu vya muziki na kufanikiwa kuutapanua uwigo wake kwa kuwanasa washabiki wengi wa kimataifa. Bendi hiyo maarufu iliyojiimarisha na kujenga himaya ya kimataifa kwa kutumia muziki wake.

Imeshatajwa mara nyingi kuwa bendi bora ya kiafrika barani ulaya, bendi ya Ngoma Africa inafanananishwa sawa na kikosi maalumu cha kuzuwia ghasia FFU, pia ina majina mengi ya utani na kiusanii kama vile viumbe wa ajabu “Anunnaki Elien” n.k ambayo imepewa na washabiki au wapenzi wake, kiongozi wake pia ana majina kama vile kamanda Ras Makunja wa FFU, mtawala wa Anunnaki Empire. Ngoma Africa band wanasikika at www.ngoma-africa.com

Taarifa Anuai Kutoka TFF Novemba 26, 2013

$
0
0
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania

Pambano la Tanzanite Sasa Kufanyika Dar

MECHI ya kwanza ya raundi ya michuano ya Kombe la Dunia, Kanda ya Afrika kwa wanawake chini ya miaka 20 kati ya Tanzania (Tanzanite) na Afrika Kusini iliyokuwa ichezwe Mwanza sasa itafanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
 
Baada ya ukaguzi uliofanywa na maofisa wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), imebainika uwanja huo unatakiwa ufanyiwe marekebisho ambayo hayawezi kuwahi Desemba 7 mwaka huu, siku ambayo ndiyo mechi hiyo inatakiwa kuchezwa.
 
Vyumba vya wachezaji vya uwanja huo ndilo eneo ambalo linatakiwa  kufanyiwa marekebisho makubwa.
 
KILIMANJARO STARS YATUA SALAMA NAIROBI
Timu ya Tanzania Bara (Kilimanjaro Stars) imewasili salama Nairobi, Kenya tayari kwa mashindano ya Kombe la Chalenji yanayoanza kesho (Novemba 27 mwaka huu) katika Uwanja wa Nyayo.
 
Kilimanjaro Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager iliwasili saa 3 usiku kwa ndege ya RwandAir, na imefikia katika hoteli ya Sandton iliyoko katikati ya Jiji la Nairobi.
 
Kwa mujibu wa programu ya Kocha Mkuu Kim Poulsen, Kilimanjaro Stars leo (Novemba 26 mwaka huu) ni mapumziko ambapo kesho itafanya mazoezi kujiandaa kwa mechi yake ya kwanza dhidi ya Zambia itakayochezwa Novemba 28 mwaka huu Uwanja wa Machakos.
 
WANNE WASHINDA UCHAGUZI CECAFA
Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) limepata wajumbe wapya wa wanne wa Kamati ya Utendaji katika uchaguzi uliofanya leo (Novemba 26 mwaka huu) hoteli ya Hillpark jijini Nairobi.
Uchaguzi huo ulifuatiwa na Mkutano Mkuu wa CECAFA ulioongozwa na Mwenyekiti wake Leodegar Tenga na kuhudhuriwa na mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), Kalusha Bwalya na ofisa wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA), Emmanuel Maradas.
 
Rais wa zamani wa Shirikisho la Vyama vya Mpira wa Miguu Uganda (FUFA), Lawrence Mulindwa ndiye aliyeongoza katika uchaguzi huo ambapo wasimamizi walikuwa Bwalya na Maradas.
 
Mulindwa alipata kura zote 12 na kufuatiwa na Tariq Atta wa Sudan (10), Abdigaani Saeb Arab wa Somalia (9) na Raoul Gisanura wa Rwanda (8). Atta, Arab na Gisanura walikuwa wakitetea nafasi zao.
 
Walioshindwa ni Rais wa Chama cha Mpira wa Miguu Sudan Kusini (SSFA), Alei Chabor aliyepata kura tano na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu la Kenya (FKF), Sam Nyamweya aliyepata kura nne.
 
MICHUANO YA UHAI YAHAMIA CHAMAZI
Michuano ya Kombe la Uhai imeingia hatua ya robo fainali ambapo sasa mechi zinachezwa kwenye Uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
 
Uamuzi wa kuhamisha mechi hizo kutoka viwanja vya Karume na DUCE ni kuziwezesha zote kuoneshwa moja kwa moja (live) na Azam Tv.
 
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) tunaomba radhi kwa washabiki ambao watakuwa wameathirika kutokana na uamuzi huo.
 
USAJILI DIRISHA DOGO KUFUNGWA DESEMBA 15
Wakati dirisha dogo la usajili linafungwa Desemba 15 mwaka huu, Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) tunazikumbusha klabu zote kuheshimu kanuni na kuzingatia muda uliowekwa.
 
Pia tunakumbusha kuwa kupeleka mchezaji kwa mkopo katika klabu nyingine hakutoi nafasi ya kusajili mchezaji mpya. Kama klabu ilisaji wachezaji 30 maana yake ni kuwa haina nafasi ya kuongeza wachezaji.
 
Kwa upande wa wachezaji wa kigeni (foreign players), tunakumbusha kuwa kuanzia msimu ujao 2014/2015 watakuwa watatu tu badala ya watano wa sasa.
 
Kuhusu usajili wa wachezaji kutoka nje mpaka sasa hakuna hata klabu moja imeshaingia kwenye TMS kuomba uhamisho. Itakapofika Desemba 15, system ya TMS itafunga.
 
RAMBIRAMBI MSIMBA WA ANDREW KILOYI
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea kwa masikitiko taarifa za kifo cha mwamuzi wa zamani wa FIFA, Andrew Kiloyi kilichotokea mjini Iringa.
 
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Chama cha Waamuzi wa Mpira wa Miguu Mkoa wa Iringa, Ramadhan Mahano, Kiloyi alifariki dunia juzi (Novemba 24 mwaka huu) kutoka na ugonjwa wa fangasi ya ubongo, na marehemu amesafirishwa kwenda kwao Kigoma ambapo atazikwa.
 
Kiloyi alizaliwa Mei 5, 1968. Alijiunga na uamuzi wa mpira wa miguu mwaka 1988 ambapo alipata beji ya FIFA mwaka 2001 akiwa mwamuzi msaidizi. Alistaafu uamuzi mwaka 2009, na hadi anafariki akiwa mjumbe wa Kamati ya Waamuzi ya Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Iringa (IREFA).
 
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linatoa pole kwa familia ya marehemu, IREFA, ndugu, jamaa na marafiki kutokana na msiba huo na kuwataka kuwa na moyo wa subira na uvumilivu katika kipindi hicho cha majonzi. Mungu aiweka mahali pema roho ya marehemu Kiloyi.  
 
*Zimeandaliwa na Boniface Wambura Mgoyo, Kaimu Katibu Mkuu
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

Kikosi cha Afrika Kusini Kutua Dar Kuivaa Tanzanite

$
0
0
Kaimu Katibu Mkuu TFF, Boniface Wambura Mgoyo

Kaimu Katibu Mkuu TFF, Boniface Wambura Mgoyo

KIKOSI cha Afrika Kusini kwa ajili ya mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia kwa wasichana wenye umri chini ya miaka 20 dhidi ya Tanzania (Tanzanite) kinatua nchini Desemba 5 mwaka huu. Afrika Kusini ambayo itafikia hoteli ya Sapphire itatua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) itatua saa 8 kamili mchana kwa ndege ya South Africa Airways.
 
Mechi hiyo itachezeshwa na refa Nabikko Ssemambo kutoka Uganda wakati mwamuzi msaidizi namba moja ni Gebreyohanis Trhas kutoka Ethiopia. Waamuzi wengine ambao pia wanatoka Uganda ni Nakitto Nkumbi na Irene Namubiru.
 
Kamishna wa mechi hiyo ni John Muinjo kutoka Namibia. Muinjo pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Namibia (NFA) na mjumbe wa Kamati ya Mpira wa Miguu wa Wanawake ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF).
 
Viingilio katika mechi hiyo itakayochezwa Jumamosi (Desemba 7 mwaka huu) kuanzia saa 10 kamili jioni Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ni sh. 1,000 kwa viti vya rangi ya kijani, bluu na orange, sh. 2,000 kwa VIP C, sh. 5,000 kwa VIP B wakati VIP A watalipa sh. 10,000.
 
Tanzanite chini ya Kocha Rogasian Kaijage inaendelea na mazoezi kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume na ule wa Taifa kujiandaa kwa mechi hiyo. Kambi ya Tanzanite hivi sasa imehamia Msimbazi Hotel kutoka Ruvu mkoani Pwani.
 
*Imeandaliwa na Boniface Wambura Mgoyo, Kaimu Katibu Mkuu
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

FIFA Yaipa TFF Tiketi 260 za Kombe la Duniam, AFCON Kupangwa..!

$
0
0
FIFA Yaipa TFF Tiketi 260 za Kombe la Dunia

FIFA Yaipa TFF Tiketi 260 za Kombe la Dunia

SHIRIKISHO la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) limeipa Tanzania mgawo wa tiketi 260 za Fainali za Kombe la Dunia nchini Brazil. Watanzania wanaohitaji tiketi hizo wanatakiwa kutuma maombi TFF kwa maandishi wakielezea aina ya tiketi na mechi wanazotaka kushuhudia. Hakuna tiketi zitakazoombwa FIFA bila kuwepo maombi kwa maandishi.
 
Tiketi zilizopo kwa Tanzania ni ifuatavyo; kwa hatua ya makundi (ukiondoa mechi ya ufunguzi), raundi ya 16 bora, robo fainali na mechi ya kutafuta mshindi wa tatu ni 250.
 
Kwa mechi ya ufunguzi, nusu fainali mbili na fainali (mechi namba 1, 61, 52 na 64) ni tiketi kumi tu ndizo zitakazopatikana. Bei za tiketi ziko katika viwango vitatu tofauti.
 
Mechi ya ufunguzi tiketi zake ni dola za Marekani 495, 330 na 220. Hatua ya makundi (mechi namba 2-48) ni dola 175, 135 na 90. Hatua ya 16 bora (mechi namba 49-56) ni dola 220, 165 na 110.
 
Robo fainali (mechi namba 57-60) ni dola 330, 220 na 165 wakati nusu fainali (mechi namba 61 na 62) ni dola 660, 440 na 275. Mechi ya mshindi wa tatu ni dola 330, 220 na 165. Kiingilio kwa fainali kitakuwa dola 990, 660 na 440.
 
TFF itawasilisha maombi ya tiketi hizo FIFA kuanzia Desemba 8 mwaka huu  hadi Februari 7 mwakani. Idadi ambayo itaombwa FIFA itatokana na Watanzania waliowasilisha maombi TFF kwa vile zinaweza zisipatikane tiketi zote hizo zilitengwa kwa Tanzania. Hivyo tunasisitiza maombi ya tiketi yatakayofanyiwa kazi ni yale ambayo yamewasilishwa TFF kwa maandishi tu.
 
JOPO LA WATAALAMU KUPANGA MKAKATI WA AFCON 2015
Jopo la wataalamu 20 walioteuliwa na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi linakutana kupanga mkakati wa kuonesha jinsi Tanzania inavyoweza kushiriki Fainali za Afrika (AFCON) zitakazofanyika mwaka 2015 nchini Morocco.
 
Kikao hicho maalumu (retreat) kitafanyika mjini Zanzibar kuanzia Desemba 6-8 mwaka huu. Jopo hilo litaongozwa na Mwenyekiti wa zamani wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Kanali mstaafu Idd Omari Kipingu.
 
Wengine wanaounda jopo hilo linalohusisha pia makocha ni Dk. Mshindo Msolla, Peter Mhina, Ayoub Nyenzi, Abdallah Kibaden, Pelegrinius Rutahyuga, Kidao Wilfred, Salum Madadi, Juma Mwambusi, Ken Mwaisabula, Boniface Mkwasa, Fred Minziro, Meja Abdul Mingange, Ally Mayay, Boniface Mkwasa na Dan Korosso. Wajumbe wengine wa jopo hilo wanatoka Chama cha Mpira wa Miguu Zanzibar (ZFA).
 
*Imeandaliwa na Boniface Wambura Mgoyo, Kaimu Katibu Mkuu
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)


Malinzi Aunda Kamati Kutathmin Muundo wa Ligi

$
0
0
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi

Na Mwandishi Wetu

RAIS wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi ameunda kamati mbili maalumu (ad hoc) kwa ajili ya kutathmini muundo wa ligi na kupendekeza namna ya kuuboresha, na kutahmini muundo wa Bodi ya Ligi na kupendekeza namna ya kuuboresha ikiwemo kuunda kampuni.
 
Kamati ya Kutathmini Muundo wa Ligi inaongozwa na Kocha wa zamani wa Taifa Stars, Dk. Mshindo Msolla wakati Katibu ni Ofisa Mashindano wa TFF, Idd Mshangama. Wajumbe ni Rahim Kangezi, Amri Said, Sunday Manara, Salim Bawazir na Lucas Kisasa.
 
David Nchimbi kutoka Delloitte ndiye anayeongoza Kamati ya Muundo wa Bodi ya Ligi wakati wajumbe ni Edwin Kidifu (Mwanasheria wa SUMATRA), Jones Paul (Mkurugenzi wa Sunderland/Symbion Academy), Evans Aveva, John Jambele, Masoud Sanani na Pelegrinius Rutahyuga.
 
Wakati huo huo, Rais Malinzi amemteua Pelegrinius Rutahyuga kuwa Mshauri wa Rais (Ufundi). Mshauri wa Rais (Utawala) atateuliwa baadaye.

AFRIKA KUSINI KUTUA KWA SOUTH AFRICA AIRWAYS

Wakati huo huo; Kikosi cha Afrika Kusini (Basetsana) kwa ajili ya mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia kwa wasichana wenye umri chini ya miaka 20 dhidi ya Tanzania (Tanzanite) kinatua nchini kesho (Desemba 5 mwaka huu).
 
Afrika Kusini itatua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) itatua saa 8 kamili mchana kwa ndege ya South Africa Airways.
 
Wanaounda Basetsana ni makipa Kaylin Swart, Regirl Ngobeni na Juliet Sethole. Mabeki ni Abongile Dlani, Caryn van Reyneveld, Chamelle Wiltshire, Meagan Newman, Nomonde Nomthseke, Tiisetso Makhubela na Vuyo Mkhabela.
 
Viungo wapo Amanda November, Amogelang Motau, Gabriella Salgado, Koketso Mamabolo, Nomvula Kgoale na Thembi Kgatlane. Washambuliaji ni Mosili Makhoali, obyn Moodaly, Sduduzo Dlamini na Shiwe Nogwanya.
 
Viingilio katika mechi hiyo itakayochezwa Jumamosi (Desemba 7 mwaka huu) ni sh. 1,000 kwa viti vya rangi ya kijani, bluu na orange, sh. 2,000 kwa VIP C, sh. 5,000 kwa VIP B wakati VIP A watalipa sh. 10,000.

U.S. Draws Into ‘Group of Death’ for 2014 World Cup

$
0
0
U.S. Draws Into 'Group of Death' for 2014 World Cup

U.S. Draws Into ‘Group of Death’ for 2014 World Cup

U.S. Draws Into 'Group of Death' for 2014 World Cup.1

U.S. Draws Into ‘Group of Death’ for 2014 World Cup.1

U.S. Draws Into 'Group of Death' for 2014 World Cup.

U.S. Draws Into ‘Group of Death’ for 2014 World Cup.

UNITED States head coach Jurgen Klinsmann described his team’s World Cup draw as “the worst of the worst” after it was pooled with Germany, Portugal and Ghana in one of two “Groups of Death.”

Klinsmann could scarcely believe his ill fortune after the draw was made in Bahia, Brazil, with the Americans lumped into Group G and a situation that immediately installed them as long shots to reach the last 16. To add to his discomfort, Klinsmann’s side also will have to battle a grueling travel schedule, including a visit to the Amazonian jungle city of Manaus with its extreme humidity and hostile weather environment.

“It is one of the most difficult groups of the whole draw,” Klinsmann said. “It couldn’t get any more difficult or any bigger but that is what the World Cup is all about.

“We are looking forward to the challenge and we don’t see ourselves as any kind of outsiders. If you want to get into the top 10 or 12 teams in the world you have to beat these guys.

“We discussed before the draw that there could be some difficult schedules and we hit the worst of the worst. Every coach said, ‘Anything but Manaus’ and we got Manaus.”

Germany is one of the strongest teams in the tournament and reached the semifinal in 2010, while Portugal will be led by Cristiano Ronaldo, currently the world’s best and most dominant player. Supposedly the weakest opponent, Ghana, eliminated the U.S. at the round of 16 stage four years ago. The Ghanaians also ended the Americans’ 2006 World Cup with a victory in the teams’ final group game.

“After two losses, it’s about time to beat them, I guess,” Klinsmann said.

The Ghana matchup will be the first for the U.S. and is scheduled for Natal on June 16. Portugal follows in Manaus six days later before group action ends against Germany in Recife on June 26.

“I kind of had a feeling in my stomach that we were going to get Germany,” said Klinsmann, who starred for the West Germany national team as it won the 1990 World Cup and later led the German side to the 2006 semifinals on home soil.

The “other” Group of Death is Group B where 2010 finalists Spain and the Netherlands square off in the opening match. Host nation Brazil kicks off the tournament against Croatia in Sao Paulo on June 12.

Group A:
Brazil – Host nation is a clear favorite to win it all and was the seed no one wanted to meet.
Croatia – Shaky in qualifying and winless in World Cups since 1998; Luka Modric is a shining light.
Mexico – Fortunate to qualify after desperate CONCACAF form pushed it to the brink of elimination.
Cameroon – Lowest-ranked of the African nations after patchy form over the past year.

Group B:
Spain – Defending champion started slowly in 2010, losing to Switzerland in first game.
Netherlands – 2010 runner-up was somehow unseeded and a team nobody wanted to face.
Chile – Struggled early in qualifying but was near perfect late on and will be a real threat.
Australia – Fired coach Holger Osieck after heavy friendly defeats and comes in with little momentum.

Group C:
Colombia – Radamel Falcao heads a deep squad keen to shine after missing last three tournaments.
Greece – Not much fun to watch; defensively excellent but short on attacking firepower.
Ivory Coast – Eliminated in the Group of Death last time, Didier Drogba’s back for one last shot.
Japan – Greatly improved team more than capable of creating some shocks against bigger opponents.

Group D:
Uruguay – Reached the semis four years ago but survived a qualifying scare this time around.
Costa Rica – Qualifying success was built upon outstanding home form, struggles on the road.
England – Lacking in confidence and inspiration and comes in with its lowest expectations in decades.
Italy – Champions in 2006, awful in 2010, full of talent and believes it can go all the way.

Group E:
Switzerland – Considered the weakest seeded team but a skillful unit capable of going deep.
Ecuador – Clinched a World Cup spot for only the third time and has never gone past the last 16.
France – Scraped through with a playoff comeback, hopes to atone for humiliating 2010 campaign.
Honduras – Has reached two previous World Cups but has yet to record its first victory.

Group F:
Argentina – Lionel Messi heads a confident team looking to secure first title since 1986.
Bosnia-Herzegovina – The only newcomer in the 32-strong field, highly talented but unpredictable.
Iran – Managed just one point from three games in 2006 and failed to qualify in 2010.
Nigeria – One of the youngest squads in the tournament that should not be underestimated.

Group G:
Germany – Third in 2010 and aims to build on positive vibe created by its dominant club teams.
Ghana – Knocked out the U.S. in 2010 before being heartbreakingly denied a semifinal spot.
United States – Regarded as the strongest team in its pot after topping CONCACAF group.
Portugal – Cristiano Ronaldo single-handedly won a tense playoff but has yet to shine at World Cup.

Group H:
Belgium – Reached first World Cup since 2002 after huge improvement and a superb qualifying campaign.
Russia – Finished first in a tough qualifying group that also featured Portugal and Sweden.
Algeria – Bottom of the U.S. group in 2010 and one of the weakest teams, at least on paper.
South Korea – An easy campaign became nail-biting late on; finally booked place on goal differential.

TFF Yamlilia Nelson Mandela, Tanzanite Fiti Kuikabili Basetsana

$
0
0
TFF Yamlilia Nelson Mandela, Tanzanite Fiti Kuikabili Basetsana

TFF Yamlilia Nelson Mandela, Tanzanite Fiti Kuikabili Basetsana

SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea kwa masikitiko kifo cha Rais wa zamani wa Afrika Kusini, Nelson Mandela kilichotokea Desemba 5 mwaka huu nchini humo. Msiba huo ni mkubwa katika familia ya mpira wa miguu kwa Afrika Kusini, Afrika na Dunia kwa ujumla kutokana na mchango mkubwa wa Mzee Mandela katika mchezo huo.
 
Mzee Mandela anakumbukwa kwa mchango wake katika Fainali za Afrika (AFCON) zilizofanyika mwaka 1996 nchini Afrika Kusini na hata zile za Kombe la Dunia zilizofanyika nchini humo mwaka 2010.
 
TFF tunatoa pole kwa Rais wa Chama cha Mpira wa Miguu Afrika Kusini (SAFA), Danny Jordan, na wananchi wa Afrika Kusini na kuwataka kuwa na subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha msiba huo mzito. Mungu aiweke roho ya marehemu Mandela mahali pema peponi. Amina.

TUMEJIANDAA VIZURI KWA MECHI- TANZANITE
TANZANITE imesema iko vizuri kwa ajili ya mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia kwa wasichana wenye umri chini ya miaka 20 dhidi ya Afrika Kusini (Basetsana) inayochezwa Jumamosi ya Desemba 7 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
 
Kocha Mkuu wa Tanzanite, Rogasian Kaijage amesema wamejiandaa vizuri kwa mechi hiyo ya kwanza ya raundi ya pili itakayochezwa kuanzia saa 10 kamili jioni.
 
“Tumejiandaa, vijana wako vizuri wanasubiri saa ya mechi tu. Licha ya kwamba Afrika Kusini wako mbele kwenye mpira wa miguu wa wanawake si sababu ya matokeo,” amesema Kaijage.
 
Amesema anaamini vijana wake watafanya vizuri, na kuwataka Watanzania wajitokeze kwa wingi kuwashangilia ili waweze kupata matokeo mazuri kwenye mechi hiyo inayotarajiwa kuwa na msisimko mkubwa.
 
Naye nahodha wa Tanzanite, Fatuma Issa amewataka Watanzania kuwaamini kwani wamejipanga kwa ajili ya pambano hilo, hivyo wawe nyuma yao katika kuwaongezea ari ili waweze kufanya vizuri.
 
Viingilio katika mechi hiyo ni sh. 1,000 kwa viti vya rangi ya kijani, bluu na orange, sh. 2,000 kwa VIP C, sh. 5,000 kwa VIP B wakati VIP A watalipa sh. 10,000. Tiketi zitauzwa uwanjani katika magari maalumu. Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara.

Fransic Miyeyusho Kuzichapa na Mkenya Dec 31

$
0
0
Fransic Miyeyusho

Fransic Miyeyusho

BONDIA Fransic Miyeyusho wa Tanzania amewataka Watanzania kujitokeza kwa wingi katika mchezo wake na David Chalanga kutoka Kenya utakaofanyika Desemba 31 katika ukumbi wa Msasani Klabu. Mchezo huo wa kufunga na kuukaribisha mwaka utakuwa wa raundi nane.

Akizungumzia mpambano huo bondia Miyeyusho alisema yupo fiti wakati wowote kupambana na mpinzani wake hata kama ingeamuliwa pambano hilo lifanyike leo. “Mimi nipo tayari muda wote kupambana…,” alisema Miyeyusho.

Pamoja na hayo mchezo huo ni chachu kwa mabondia wote wawili ambao wanatamba Afrika Mashariki kwa kushindsnis mikanda mikubwa ya ubingwa na kujijengea rekodi ya ushindi.

Hata hivyo kabla ya mpambano huo mkubwa kutakuwa na mapambano ya utangulizi, ambapo bondia Iddy Mnyeke ataoneshana ubabe na Cosmasi Cheka, Antony Mathias akizipiga na Fadhili Majiha, huku Ibrahimu Class ‘King Class Mawe’ akizichapa na Mohamed Kashinde.

Rais Kikwete Atoa Changamoto Uongozi Mpya TFF

$
0
0
Rais wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete

Rais wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete ametoa changamoto kwa uongozi mpya wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kusukuma mbele zaidi gurudumu la maendeleo ya mchezo huo nchini.
 
Ametoa changamoto hiyo katika barua yake kwa Rais mstaafu wa TFF, Leodegar Tenga na kumtaka asichoke kutoa ushauri na uzoefu wake kila utakapohitajika katika shughuli mbalimbali zinazohusu maendeleo ya mpira wa miguu Tanzania. Rais Kikwete ametoa changamoto hiyo wakati akijibu barua ya Tenga iliyokuwa ikimuarifu kuhusu kumaliza kipindi chao cha uongozi, na kumshukuru yeye binafsi (Rais Kikwete) na Serikali anayoiongoza kwa mchango waliotoa katika kuendeleza mpira wa miguu nchini.
 
“Pongezi zako zimetupa moyo na ari ya kuongeza maradufu juhudi zetu za kuboresha kiwango cha ubora wa mchezo wa mpira wa miguu nchini. Kwa niaba ya Serikali napenda kuchukua nafasi hii kutoa pongezi za dhati kwako wewe na uongozi wote uliopita wa TFF kwa mchango wenu muhimu mlioutoa wa kuendeleza mpira wa miguu nchini.
 
“Mafanikio ya kutia moyo yamepatikana chini ya uongozi wako,” amesema Rais Kikwete katika barua yake hiyo na kumtakia kila la heri Tenga katika shughuli zake.
 
Hata hivyo, ameongeza kuwa Tanzania bado haijafika pale ambapo inapataka, lakini dalili njema zimeanza kuonekana, hivyo kinachotakiwa sasa ni uongozi mpya kusukuma mbele zaidi gurudumu la kuendeleza mpira wa miguu nchini.
 
Tenga ambaye hivi sasa ni mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) na Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) aliiongoza TFF kwa vipindi viwili kuanzia Desemba 2004 hadi Oktoba 2013.
 
PAMBANO LA TANZANITE LAINGIZA MIL 5/-
Pambano kati ya timu ya Taifa ya wanawake kwa vijana wenye umri chini ya miaka 20 ya Tanzania (The Tanzanite) dhidi ya Afrika Kusini (Basetsana) lililochezwa jana (Desemba 7 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam limeingiza sh. 5,353,000.
 
Washabiki waliohudhuria mechi hiyo ya kwanza ya raundi ya pili ya Kombe la Dunia, Kanda ya Afrika iliyomalizika kwa The Tanzanite kulala mabao 4-1 walikuwa 4,282. Viingilio vilikuwa sh. 1,000, sh. 2,000, sh. 5,000 na sh. 10,000.
 
Mgawo wa mapato hayo ulikuwa kama ifuatavyo; Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) sh. 816,559.32, gharama za kuchapa tiketi sh. 1,649,754, asilimia 20 ya gharama za mchezo sh. 577,573) wakati wamiliki wa uwanja walipata sh. 433,003. Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) lilipata sh. 144,334.33 huku Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) likipata sh. 1,732,012.01.
 
Mechi iliyopita ya Tanzanite dhidi ya Msumbiji iliyochezwa Oktoba 26 mwaka huu Uwanja wa Taifa, na timu hiyo kushinda mabao 10-0 ilishuhudiwa na watazamaji 5,003 na kuingiza sh. 6,190,000. Tanzanite na Basetsana zitarudiana kati ya Desemba 20 na 22 mwaka huu jijini Johannesburg, Afrika Kusini.

Kilimanjaro, Harambee Stars Kukipiga Machakos

$
0
0
Baadhi ya wachezaji wa Kilimanjaro Stars

Baadhi ya wachezaji wa Kilimanjaro Stars

MECHI ya kwanza ya nusu fainali ya michuano ya mwaka huu ya Kombe la Chalenji kati ya Tanzania Bara (Kilimanjaro Stars) na wenyeji Kenya (Harambee Stars) itapigwa Uwanja wa Machakos.
 
Kwa mujibu wa ofisa wa CECAFA, Amir Hassan mechi hiyo itachezwa Uwanja wa Machakos ulioko takribani kilometa 64 kutoka jijini Nairobi. Mechi hiyo itachezwa Jumanne (Desemba 10 mwaka huu) kuanzia saa 10 kamili jioni na itaoneshwa moja kwa moja  na kituo cha televisheni cha SuperSport kupitia chaneli ya SS9.
 
Kilimanjaro Stars imetinga hatua hiyo baada ya kuivua ubingwa Uganda (The Cranes) kwa mikwaju 3-2 ya penalti katika mechi ya robo fainali ya michuano hiyo iliyochezwa jana Uwanja wa Aga Khan katika Jiji la Mombasa.
 
Hadi dakika 90 za kawaida zinamalizika timu hizo zilikuwa zimefungana mabao 2-2. Mabao ya Kilimanjaro Stars yalifungwa na Mrisho Ngasa wakati katika mikwaju ya penalti walofumania nyavu ni Amri Kiemba, Athuman Idd na nahodha Kelvin Yondani.
 

Kongamano la Wanawake Viongozi wa Michezo Afrika Kufanyika Dar

$
0
0
Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Vijana wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni, na Michezo Bwana Leornad Thadeo akizungumza na Wanahabari (Hawapo Pichani) kuhusu Kongamano la Wanawake Viongozi wa Michezo wa Afrika litakalofanyika 16-17/2013 jijini Dar es Salaam wa kwanza kulia ni Meneja wa kinywaji cha Grand Malt Bi Consolata Adam. Picha na Benjamin Sawe wa WHVUM

Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Vijana wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni, na Michezo Bwana Leornad Thadeo akizungumza na Wanahabari (Hawapo Pichani) kuhusu Kongamano la Wanawake Viongozi wa Michezo wa Afrika litakalofanyika 16-17/2013 jijini Dar es Salaam wa kwanza kulia ni Meneja wa kinywaji cha Grand Malt Bi Consolata Adam. Picha na Benjamin Sawe wa WHVUM


Wasanii Chipukizi Watakao Tumbuiza Tamasha la UCA Tanzania Wakutana

$
0
0

Tamasha la UCA Tanzania

IMG_3488

IMG_3466

IMG_3479

IMG_3376

Pichani juu ni baadhi ya wasanii chipukizi watakaopewa nafasi ya kuonesha vipaji vyao Jumamosi hii katika tamasha la kukuza vipaji vya sanaa na muziki litakalofanyika viwanja vya Biafra Kinondoni jijini Dar es Salaam Dec 14. Wasanii hawa wataungana na wasanii wengine vijana walionza kufanikiwa katika tasnia akiwemo msanii Ally Nipishe na kuonesha vipaji vyao kwa vijana wenzao.

IMG_3587

Baadhi ya wasanii chipukizi watakaoonesha vipaji vyao wakiwa na msaanii anayeanza kufanya vizuri katika tasnia ya muziki wa kizazi kipya Ally Nipishe (watatu kutoka kulia waliosimama) wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufanya mazoezi na kubadilishana uzoefu.

IMG_3483

Msanii Ally Nipishe (aliyevaa kofia) akitoa ushauri kwa baadhi ya vijana waliopewa nafasi kutumbuiza katika tamasha la vipaji vya Sanaa na Muziki kwa vijana lililoandaliwa na UCA-Tz kwa kushirikiana na kampuni za Zantel, Coca Cola- Tanzania, Maezeki, LBGY Media na mtandao wa Thehabari.com.

IMG_3412

Mmoja wa wasanii chipukizi (wa kwanza kulia) akipokea mrejesho baada ya kuimba wimbo wake toka kwa wadau vijana wa UCA Tz leo. Wa kwanza kushoto ni MC wa zoezi la kuwatambua chipukizi waliopata nafasi ya kutumbuiza kwenye tamasha hilo.

IMG_3402

 Baadhi ya vijana wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikiendelea kutoka kwa vijana waandaaji wa UCA-Tz leo.

IMG_3485

Mwanadada mwakilishi wa Vijana kutoka UCA-Uganda aliyewasili Tanzania kushiriki tamasha hilo akitoa mchango wake kwa wasanii vijana walioshiriki kwenye zoezi hilo.

IMG_3603

Baadhi ya vijana waandaaji wa Tamasha la Vipaji kwa Sanaa na Muziki kwa Vijana UCA TZ wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumaliza kikao cha majadiliano namna ya kufanikisha tamasha hilo litakalozinduliwa na Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo.

 

Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Kuzinduwa Tamasha la Vipaji

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa asasi ya ukuzaji vipaji vya sanaa na muziki (Unscripted Concert for Africa-Tanzania, UCA-Tz), Emmanuel Mushy (katikati) akizungumza na waandishi wa habari juu ya tamasha la UCA-Tz litakalofanyika kesho jijini Dar es Salaam. Wa kwanza kutoka kushoto ni Mwakilishi kutoka kampuni ya Zantel, Divine Mosi na Fadhil Nandonde kutoka UCA-Tz, kulia ni mwakilishi wa vijana kutoka nchini Uganda, Ms. Faridah Nalunkuma.

Mkurugenzi Mtendaji wa asasi ya ukuzaji vipaji vya sanaa na muziki (Unscripted Concert for Africa-Tanzania, UCA-Tz), Emmanuel Mushy (katikati) akizungumza na waandishi wa habari juu ya tamasha la UCA-Tz litakalofanyika kesho jijini Dar es Salaam. Wa kwanza kutoka kushoto ni Mwakilishi kutoka kampuni ya Zantel, Divine Mosi na Fadhil Nandonde kutoka UCA-Tz, kulia ni mwakilishi wa vijana kutoka nchini Uganda, Ms. Faridah Nalunkuma.

Mkurugenzi Mtendaji wa asasi ya ukuzaji vipaji vya sanaa na muziki (Unscripted Concert for Africa-Tanzania, UCA-Tz), Emmanuel Mushy (katikati) akizungumza na waandishi wa habari juu ya tamasha la UCA-Tz litakalofanyika kesho jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mtendaji wa asasi ya ukuzaji vipaji vya sanaa na muziki (Unscripted Concert for Africa-Tanzania, UCA-Tz), Emmanuel Mushy (katikati) akizungumza na waandishi wa habari juu ya tamasha la UCA-Tz litakalofanyika kesho jijini Dar es Salaam.

Mwakilishi wa vijana kutoka nchini Uganda, Ms. Faridah Nalunkuma akizungumza na waandishi wa habari juu ya uwakilishi wake wa UCA, na kuzungumzia tamasha kwa ujumla.

Mwakilishi wa vijana kutoka nchini Uganda, Ms. Faridah Nalunkuma akizungumza na waandishi wa habari juu ya uwakilishi wake wa UCA, na kuzungumzia tamasha kwa ujumla.

Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa asasi ya ukuzaji vipaji vya sanaa na muziki (Unscripted Concert for Africa-Tanzania, UCA-Tz), Emmanuel Mushy alipozungumza nao juu ya tamasha la UCA-Tz litakalofanyika kesho jijini Dar es Salaam. PICHA ZOTE NA THEHABARI.COM

Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa asasi ya ukuzaji vipaji vya sanaa na muziki (Unscripted Concert for Africa-Tanzania, UCA-Tz), Emmanuel Mushy alipozungumza nao juu ya tamasha la UCA-Tz litakalofanyika kesho jijini Dar es Salaam. PICHA ZOTE NA THEHABARI.COM

Na Mwandishi Wetu

KATIBU Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kesho anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa tamasha la vipaji vya sanaa na muziki lililoandaliwa na asasi ya ukuzaji vipaji (Unscripted Concert for Africa-Tanzania, UCA-Tz).
Akizungumza na vyombo vya habari leo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa asasi hiyo, Emmanuel Mushy alisema tamasha hilo la pekee litakalofanyika Uwanja vya Biafra jijini Dar es Salaam linatarajia kushirikisha vijana zaidi ya 500 kutoka maeneo anuai ya jiji.

Akifafanua zaidi juu ya tamasha hilo, Mushy alisema UCA-Tz ni program yenye dhumuni la kutoa nafasi kwa vijana wenye vipaji vya muziki na sanaa ili vijana hao waweze kukua katika vipaji vyao.

“…Neno ‘unscripted’ linamaanisha kitu ambacho kipo lakini hakijaandikwa, yaani kwa maana nyingine ni kitu kilichopo nyuma ya pazia. UCA-Tz baada ya utafiti imebaini kuwa kuna vijana wengi ambao wanajihusisha na muziki pamoja na sanaa lakini hawapati ile nafasi (platform) ya kuendeleza vipaji vyao, hivyo ni kama vijana hawa wapo nyuma ya pazia,” alisema Mushy.

Aliongeza kuwa UCA Tz kwa kutambua umuhimu wa vipaji vya vijana vinavyopotea imeona umuhimu wa kutengeneza njia kwa vipaji hivyo ili vitoke nyuma ya pazia kukua na hatimaye kujionesha kwa jamii. Aidha alisema moja ya njia ambazo UCA-Tz inazifanya ni kuandaa matamasha ya vipaji kwa kila mwaka kuwashirikisha vijana na kwa mara ya kwanza inazindua Tamasha la vipaji nchini Tanzania, ambalo litashirikiza vijana zaidi 500 kutoka maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam.

“…Tamasha hili la vipaji linatarajia kufanyika kesho, Jumamosi ya tarehe 14th December pale Uwanja wa Kinondoni Biafra, kuanzia saa 7 mchana hadi saa 12 za jioni. Katika tamasha hilo vijana wenye vipaji vya kuimba, ku-rap, kucheza, kuchora na ubunifu (ku-design) watawasilisha kazi zao kwa umati utakao jitokeza na vijana wenzao,” alisema Mushy.

Alisema ili kuleta radha na hamasa zaidi asasi hiyo imealika wawakilishi vijana kutoka nchi mbalimbali za Africa kama Kenya, Uganda na Ghana ambao nao watashiriki. “…Kutakua na outside performances kutoka kwa wasanii mbalimbali ambao wameshapiga hatua kwenye tasnia za muziki na sanaa nao watashiriki kwa pamoja.

Naye Mwakilishi kutoka kampuni ya Zantel, Divine Mosi ambao ni moja wa makampuni yaliofanikisha tamasha hilo, akizungumza alisema kampuni yao itaendelea kuunga mkono shughuli anuai za kuwawezesha vijana ikiwa ni sehemu ya kurudisha mchango wa wateja wao wanaotumia mtandao wao.

Kampuni nyingine zilizounga mkono kiushirikiano (supporters/sponsers) kufanikisha tamasha hilo ni pamoja na kampuni ya Coca Cola, Maezeki, Arise Media, LGBY Media na mtandao wa kijamii wa habari-Thehabari.com (www.thehabari.com) na mitandao mingine ya kijamii nchini.

Ile Siku ya Tamasha la Vipaji kwa Vijana ni Leo…! Karibu Biafra Kinondoni Ujionee Kiingilio ni Bureeeee..!

$
0
0
Ile Siku ya Tamasha la Vipaji kwa Vijana ni Leo...! Karibu Biafra Kinondoni Ujionee Kiingilio ni Bureeeee..! Pichani ni mwakilishi wa vijana kutoka nchini Uganda, Ms. Faridah Nalunkuma (kulia) akizungumzia tamasha hilo kwa waandishi wa habari. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa asasi ya ukuzaji vipaji vya sanaa na muziki (Unscripted Concert for Africa-Tanzania, UCA-Tz), Emmanuel Mushy.

Ile Siku ya Tamasha la Vipaji kwa Vijana ni Leo…! Karibu Biafra Kinondoni Ujionee Kiingilio ni Bureeeee..!
Pichani ni mwakilishi wa vijana kutoka nchini Uganda, Ms. Faridah Nalunkuma (kulia) akizungumzia tamasha hilo kwa waandishi wa habari. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa asasi ya ukuzaji vipaji vya sanaa na muziki (Unscripted Concert for Africa-Tanzania, UCA-Tz), Emmanuel Mushy.

Ile Siku ya Tamasha la Vipaji kwa Vijana ni Leo...! Karibu Biafra Kinondoni Ujionee Kiingilio ni Bureeeee..!

Ile Siku ya Tamasha la Vipaji kwa Vijana ni Leo…! Karibu Biafra Kinondoni Ujionee Kiingilio ni Bureeeee..!KARIBU SANA UJIONEE VIPAJI ANUAI TOKA KWA VIJANA.

TFF Yagawa Mipira 10 Kila Mkoa Tanzania, Waamuzi Kutainiwa…!

$
0
0
Kaimu Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Boniface Wambura Mgoyo

Kaimu Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Boniface Wambura Mgoyo

SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetoa mipira kumi kwa kila chama cha mpira wa miguu cha mkoa ili isaidie kuendesha ligi za mikoa husika. Mipira hiyo 250 yenye thamani ya sh. 16,250,000 tayari imeanza kutumwa kwa makatibu wa vyama vya mikoa husika. Mpira mmoja una thamani y ash. 65,000.
 
Ni maratajio ya TFF kuwa mipira hiyo itakuwa chachu kwa vyama vya mikoa katika uendeshaji wa ligi hizo.
 
MITIHANI YA WAAMUZI KUFANYIKA JUMAPILI
Robo ya mwisho ya mitihani ya waamuzi (Cooper Test) na utimamu wa mwili (physical fitness test) kwa mwaka 2013 kwa waamuzi inafanyika Jumapili (Desemba 15 mwaka huu).
 
Mitihani hiyo inayofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam inashirikisha waamuzi wenye beji za Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (TFF) na wale wa kundi la waamuzi (elite) ambao wanaweza kupendekezwa kupewa beji za FIFA.
 
Wakufunzi wa mitihani hiyo ya waamuzi ni Leslie Liunda, Soud Abdi na Riziki Majala.
 
Waamuzi wa FIFA watakaofanya mitihani hiyo ni Ferdinand Chacha, Hamis Chang’walu, Israel Mujuni, Jesse Erasmus, John Kanyenye, Josephat Bulali, Mgaza Kinduli, Oden Mbaga, Ramadhan Ibada, Samwel Mpenzu na Waziri Sheha.
 
Washiriki kutoka kundi la elite ni Charles Simon, Dalali Jaffari, Hellen Mduma, Issa Bulali, Issa Vuai, Janeth Balama, Jonesia Rukyaa, Judith Gamba, Lulu Mushi, Martin Saanya, Mfaume Nassoro na Mohamed Mkono.
 
KILIMANJARO STARS YAREJEA DAR
Timu ya Tanzania Bara (Kilimanjaro Stars) iliyoshiriki michuano ya Kombe la Chalenji iliyomalizika jana jijini Nairobi, Kenya inarejea jijini Dar es Salaam leo.
 
Kilimanjaro Stars iliyomaliza michuano hiyo katika nafasi ya nne inatua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) saa 12 kamili jilioni kwa ndege ya RwandAir.
 
Wenyeji Kenya (Harambee Stars) ndiyo walioibuka mabingwa wa michuano hiyo baada ya kuifunga Sudan mabao 2-0 katika mechi ya fainali iliyochezwa jana Uwanja wa Nyayo.
 
Boniface Wambura Mgoyo, Kaimu Katibu Mkuu
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

Serikali ‘Yaifagilia UCA-Tanzania’ Kuwanyanyua Vijana

$
0
0
Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Utamaduni Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Bi. Leah Kihimbi kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara hiyo.

Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Utamaduni Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Bi. Leah Kihimbi kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara hiyo.

Mkurugenzi Mtendaji wa UCA-Tz, Emmanuel Mushy akizungumza na vijana kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kufanya uzinduzi.

Mkurugenzi Mtendaji wa UCA-Tz, Emmanuel Mushy akizungumza na vijana kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kufanya uzinduzi.

Baadhi ya wasanii chipukizi wa muziki na sanaa wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi pamoja na baadhi ya viongozi wa UCA-Tanzania.

Baadhi ya wasanii chipukizi wa muziki na sanaa wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi pamoja na baadhi ya viongozi wa UCA-Tanzania.

Mmoja wa wasanii wa kuchora akionesha kipaji chake cha kuchora michoro anuai kwa jamii kwenye tamasha hilo

Mmoja wa wasanii wa kuchora akionesha kipaji chake cha kuchora michoro anuai kwa jamii kwenye tamasha hilo

IMG_3968

IMG_4010

IMG_3950

IMG_3948

IMG_3913

IMG_3910

IMG_3868

 

Picha mbalimbali juu ni baadhi ya wasanii chipukizi wakionesha vipaji vyao kwenye tamasha hilo.

Baadhi ya wasanii chipukizi wakimsikiliza mgeni rasmi kabla ya kuonesha vipaji vyao.

Baadhi ya wasanii chipukizi wakimsikiliza mgeni rasmi kabla ya kuonesha vipaji vyao.

Baadhi ya wasanii chipukizi wakimsikiliza mgeni rasmi kabla ya kuonesha vipaji vyao.

 

Baadhi ya Wasanii chipukizi mbalimbali waliopata nafasi ya kuonesha vipaji vyao kwenye tamasha hilo.

IMG_4052

 Msanii anaoanza kufanya vizuri kwenye tasnia ya muziki wa kizazi kipya Ally Nipishe akiwaunga mkono wasanii chipukizi katika tamasha hilo.

IMG_4040

 Msanii anaoanza kufanya vizuri kwenye tasnia ya muziki wa kizazi kipya Ally Nipishe (kushoto) akiwaunga mkono wasanii chipukizi katika tamasha hilo pamoja na msanii kutoka nyumba ya vipaji THT.

IMG_4017

 

Mmoja wa wasanii chipukizi akifanya vitu vyake jukwaani.

Na Mwandishi Wetu

KATIBU Mkuu, Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo ameipongeza Asasi ya Ukuzaji Vipaji vya Sanaa na Muziki nchini (UCA-Tanzania) kwa wasanii chipukizi. Pongezi hizo zimetolewa jana jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Utamaduni Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Bi. Leah Kihimbi kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara hiyo.

Bi. Kihimbi alisema hayo alipokuwa akizinduwa tamasha la ukuzaji Vipaji vya Sanaa na Muziki kwa vijana lililoandaliwa na asasi ya UCA-Tz kwa lengo la kutoa nafasi kwa vijana wenye vipaji kuonesha vipaji vyao kwa jamii kila mwaka.

“…Nimeambiwa kuwa asasi hii imesajiliwa kwa lengo la kuwashirikisha na kuwaunganisha vijana wenye vipaji vya sanaa na muziki pamoja na waliokwishafanikiwa katika kuwezesha kukuza vipaji walivyonavyo,” alisema Bi. Kihimbi akimuwakilisha Katibu Mkuu.

“Kimsingi hili ni jambo jema la kusaidiana na serikali katika kukuza vipaji na kuongeza viwango vya sanaa, ili kuwawezesha wasanii wetu kukabiliana kikamilifu katika ushindani wa soko la kimataifa,” alisema.

“…Nawashauri vijana watumie fursa kama hii kila kila zinapopatikana katika kufanikisha malengo yao kupitia fani za sanaa. Kama sote tunavyofahamu kuwa sanaa ni ajira na inanafasi kubwa ya kubadili maisha ya watu na nchi kiuchumi na kifikra ni vema watu wakaondokana na dhana potofu kuwa sanaa si kazi ya maana na ni kwa wasiohitaji kujifunza,” alisisitiza.

Aidha alitoa changamoto kwa badhi ya watu kuacha fikra finyu za kuichukulia sanaa kama si kazi kama ilivyo kazi nyingine, kwani mawazo hayo hayaitendei haki pamoja na kuzingatia umuhimi wa sanaa kwa jamii. “…Ninapata furaha kubwa kusikia kuwa tamasha hili litakuwa likifanyika kila mwaka. Ninakupongezeni sana kwa kubeba sura ya uzalendo unaolenga kuikuza, kuiendeleza na kuipa hadhi fani ya sanaa na muziki,” aliongeza.

“…Ninatambua kuwa kazi hii kubwa na nzuri mnayoifanya ni utakelezaji wa sera ya utamaduni inayosisitiza na kusimamia maadili ya Mtanzania pamoja na kuzingatia mafunzo na elimu katika fani zetu. Tunafahamu kuwa utamaduni ni mali ya jamii, hivyo ni jukumu la wananchi wenyewe kuupenda, kuuthamini na kuuendeleza utamaduni wetu kwa kutumia kazi za sanaa.”

Awali akizungumza kabla ya uzinduzi wa tamasha hilo, Mkurugenzi Mtendaji wa UCA-Tz, Emmanuel Mushy aliishukuru Serikali kwa ushirikiano iliouonesha kufanikisha tamasha hilo na kutoa shukrani kwa makampuni ya Zantel, Coca Cola- Tanzania, Maezeki, LBGY Media na mtandao wa Thehabari.com kushiriki kuwasaidia vijana wasiosikika kusikika.

Zaidi ya wasanii 25 chipukizi walipata nafasi kwenye tamasha hilo ya kuonesha uwezo wao kwa jamii wakiwemo baadhi ya wasanii chipukizi wanaoanza kunufaika na kazi zao kama Menina, M Rap na Ally Nipishe.

Viewing all 521 articles
Browse latest View live