Quantcast
Channel: Michezo na Burudani – Tanzania Habari | Jamii | Michezo | Mahusiano | Kazi | Thehabari.com
Viewing all 521 articles
Browse latest View live

Redd’s Miss Tanga, Kupatikana Juni 22

$
0
0

Mkurugezi wa Kampuni ya DATK Intertaimeint, Asha Kigundula

Na Mwandishi Wetu

SHINDANO la kumtafuta malkia wa Mkoa wa Tanga mwaka huu “Redd’s Miss Tanga 2013″ linatarajiwa kufanyika Juni 22 kwenye Uwanja wa Mkwakwani, mkoani humo.

Akizungumza na mtandao huu jana Mkurugezi wa Kampuni ya DATK Intertaimeint, ambao ni waandaaji wa shindano hilo, Asha Kigundula, alisema kuwa warembo wote wanaoshiriki kinyang’anyiro hicho tayari wameanza mazoezi yanayofanyika kwenye Ukumbi wa Lavida uliopo jijini Tanga.

Kigundula alisema shindano hilo litaanza saa 2, usiku likienda sambamba na burudani mbalimbali kutoka kwa moja ya bendi maarufu hapa nchini pamoja na wasanii wanaotamba katika muziki wa kizazi kipya.

Alisema maandalizi ya shindano hilo yanaendelea vizuri na jumla ya warembo 14 watashindania taji hilo. Kigundula aliongeza kuwa mpaka juzi warembo 10 walikuwa wamejitokeza na kuanza mazoezi yanayosimamiwa na Miss Tanga 2012, Teresia Kimolo na Mwanaid Omar.

Aliwataja miongoni mwa warembo watakao chuana kuwa ni pamoja na Hawa Ramadhan (18), Hazina Mbaga (19), Like Abdulraman (19), Jack Emannuel (18),Waida Mmbwambo(20), Tatu Hussein(19), Mwanahamis Mashaka(20), Neema Abdallah (18), Winfrida Gutram (21)Lulu Mbonea (19) na Aisha Rashid (21).
“Kila kitu kinaendelea vizuri, ikiwa na warembo kuendelea kujiandikisha kushiriki shindano la mwaka huu, ambalo nina hakika litakuwa la aina yake,” alisema Kigundula.

Alisema kwamba shindano la mwaka huu litaandika historia mpya ya urembo mkoani humo kwa kuwa Kampuni DATK imejipanga, hivyo mashabiki wa mashindano ya urembo wa jijini hapo kwa ujumla wakae mkao wa kupata raha.

Redd’s, Miss Tanga, imedhaminiwa na CXC Africa, Executive Solutions, Busta General Supply, Mkwabi Interprises, Lusindic Investment LTD, Lavida Pub, Jambo Leo, Staa Spoti, Five Brothers, Cloud’s Media Group, pamoja na Blog Michuzi Media Group, Bongostaz.com, Saluti5, Kajuna, JaneJohn, na Kidevu.


Bayern Munich Mabingwa Champions League

$
0
0

BAADA YA KUSHINDA ubingwa wa ligi ya Ujerumani, Bundesliga, kabla ya ligi hiyo kufikia mwisho na kuweka rekodi ya aina yake ya pointi, sasa Bayern Munich imetia kibindoni taji lake la tano la ubingwa wa Ulaya.

Ni Arjen Robben ndiye aliyepachika bao la ushindi katika dakika ya 89 na kuipatia Bayern Munich ushindi muhimu dhidi ya mahasimu wao Borussia Dortmund Jumamosi 25.05.2013, baada ya mchezo wa kuvutia wa fainali ya Champions League katika uwanja wa Wembley mjini London.

Wakati muda wa nyongeza ukipiga hodi, Robben alipokea pasi ya kisigino kutoka kwa Frank Ribery, akamkwepa Mats Hummels na kuuweka mpira wavuni akimwacha Roman Weidenfeller bila majibu na kuipatia Bayern Munich taji lake la tano la mabingwa wa Ulaya.

Ulikuwa muda uliokuwa unasubiriwa mno kwa Bayern na Robben baada ya kushindwa kulitwaa taji hilo katika fainali za mwaka 2010 na 2012, wakati walipobwagwa kwa mikwaju ya penalti dhidi ya Chelsea London katika uwanja wake wa nyumbani.

“Kipindi changu chote cha kucheza soka kilipita katika mawazo yangu wakati nilipopachika bao hilo. Ni hali ya kipekee kabisa unayoweza kuihisi, huwezi kuielezea,” Robben amesema.
Heynckes amwagiwa sifaKocha wa Bayern Munich, Jupp Heynckes, akifurahia ushindi.

Lakini zaidi ni kocha wa Bayern Munich, Jupp Heynckes, ambaye alimiminiwa sifa tele baada ya timu yake kunyakua taji hilo. Rais wa klabu hiyo, Uli Hoeness, alimwagia sifa Heynckes mwenye umri wa miaka 68 ambaye anaweza kushinda mataji matatu na Bayern mwishoni mwa juma lijalo iwapo timu hiyo itaishinda VFB Stuttgart katika fainali ya Kombe la Shirikisho, DFB Pokal.

“Nimefurahi kwamba klabu hii sasa iko juu kabisa katika Ulaya,” Hoeness amesema.
“Jupp amefanya kazi nzuri sana. Kuiweka timu hii na nyota wake wote katika hali sahihi na kuifanya kuendelea kufanya vizuri katika kiwango cha juu kabisa ni mkono wa Jupp Heynckes.”

Mchezaji wa kiungo wa Bayern Munich, Bastian Schweinsteiger, amesema: “Tumekuwa na msimu mzuri sana na Heynckes ana sehemu kubwa katika mafanikio hayo. Anakwenda na wakati na anaongoza akiwa mbele.”
Bastian Schweinsteiger wa Bayern Munich akishangiria ushindi na kombe mkononi.

Kocha wa Dortmund, Juergen Klopp, alimkumbatia Heynckes baada ya mchezo na alimmwagia sifa tele. “Ni mtu mzuri na muhimu,” amesema Klopp na kuongeza kwamba ulikuwa mchezo wenye mambo mengi na

“Timu zote zimeonyesha mchezo wa kiwango cha juu na kwamba zilistahili kuwapo katika fainali hii. Timu ambayo ilikuwa katika fainali tatu katika muda wa miaka minne inastahili kushinda ubingwa huu. Huenda ilikuwa kwamba ni zamu ya Bayern mwaka huu,” amesema Loew.
Wachezaji maarufu waimwagia sifa Bayern

mgumu. “Ni matokeo yanayostahili na mliona kuwa pia tulistahili kuwapo katika fainali. Tulikuwa karibu sana na kulibeba taji hili. Nimewaambia wachezaji wangu kuwa tutarejea tena, huenda sio Wembley lakini tutajaribu kurejea tena katika fainali nyingine. Hicho ndicho nilichowaeleza wachezaji.”

Naye kocha wa timu ya taifa ya Ujerumani, Joachim Loew, amesema anaipongeza Bayern kwa ushindi lakini “zaidi ya yote nampongeza Jupp Heynckes.” Loew ameuita mchezo huo kuwa fainali ya hali ya juu kabisa ambayo ilikuwa na kila kitu kinachohitajika kutoka katika soka.

“Timu zote zimeonyesha mchezo wa kiwango cha juu na kwamba zilistahili kuwapo katika fainali hii. Timu ambayo ilikuwa katika fainali tatu katika muda wa miaka minne inastahili kushinda ubingwa huu. Huenda ilikuwa kwamba ni zamu ya Bayern mwaka huu,” amesema Loew.
Wachezaji maarufu waimwagia sifa Bayern

Mchezaji wa Borussia Dortmund, Ilkay Guendogan´, akifunga bao la penalti dhidi ya Bayern Munich.
Ottmar Hitzfeld, ambaye aliwahi kushinda taji hilo akiwa na Borussia Dortmund na Bayern Munich na ambaye hivi sasa ni kocha wa timu ya taifa ya Uswisi, amesema Dortmund walionesha ujasiri wa hali ya juu kabisa.

“Wakati wote walipokuwa na uwezo na nguvu za kuwasukuma mbele walicheza mchezo safi wa kulazimisha na kutoa mbinyo, ” amesema Hotzfeld na kuongeza kuwa kila muda ulivyokwenda katika mchezo huo timu iliyokuwa ikipigiwa upatu kutoroka na taji hilo, Bayern, ilikuwa inazidi kuwa na nguvu zaidi. “Uliweza kuhisi nguvu walizokuwa nazo.”

Ushindi wa Bayern unamfanya kocha Jupp Heynckes kuwa kocha wa nne kushinda taji hilo akiwa na timu mbili tofauti, baada ya ushindi wa mwaka 1998 akiwa na Real Madrid, wakati akijitayarisha kung’atuka na kumpisha kocha wa zamani wa Barcelona, Pep Guardiola, kuchukua nafasi yake.

Iddy Kipandu Kuzichapa na Bahati Mwafyela

$
0
0

Kocha kwame mkuluma kulia akimwelekeza Bondia Iddy Kipandu ‘Iddy Bonge’ jinsi ya kutupa makonde mazito wakati wa mazoezi yaliyofanyika kigogo mburahati Dar es Salaam bonge anajitaalisha na mpambano wake na Bahati Mwafyelautakao fanyika wakati wa sikukuu ya Idi Pili (Picha na Super D Blog)

Na Mwandishi Wetu

BONDIA Iddy Kipandu ‘Iddy Bonge’ yupo kambini kwa ajili ya kupambana na bondia Bahati Mwafyela mpambano utakaofanyika siku ya Sikukuu ya Idi pili jijini Dar es Salaam kwenye Ukumbi wa Friends Corner Manzese.

Akizungumzia maandalizi ya mpambano mtayarishaji wa mpambano, Waziri Rosta amesema pambano hilo la uzito wa juu ambalo limekuwa gumzo kwa mashabiki wa mchezo yanakwenda vema. Alisema pambano hilo limekuwa gumzo kutokana na mabondia hao kuwa wakitafutana muda mrefu na sasa wanakutana kwa ajili ya kumaliza ubishi.

Mpambano huo wa raundi 8 si wakukosa kwani ndio mpambano pekee kwa mwaka huu kukutanisha uzito wa juu kwani mabondia wa uzito huu wanaotamba viwango vyao ni vidogo ukizingatia kuwa wapo wachache nchini.

Aliongeza kuwa mbali na mpambano huo kutakuwa na mapambano mengine ya mabondia chipkizi na wanaotamba hapa nchini. Kwa upande wa kocha anaemnoa bondia Iddy Kipandu ‘Iddy Bonge’ amesema kuwa bondia wake alikuwa na manyama nyama mengi lakini kwa sasa akuna kutokana na mazoezi anayompatia kwani kwa sasa dozi yake ni kutwa mara tatu na mpaka siku ya mchezo naisi mambo yatakuwa safi.

Zanzibar International Film Festival Kuanza Juni 29

$
0
0

Na Genofeva Matemu na Lorietha Laurence – MAELEZO

MAONESHO ya filamu, utamaduni, kazi za mikono na burudani yajulikanayo kama Zanzibar International Film Festival (ZIFF) yanatarajiwa kufanyika mjini Zanzibar kuanzia tarehe 29 Juni hadi tarehe 7 Julai mwaka huu.

Hayo yamesemwa leo na Mkurugenzi wa Tamasha la ZIFF Profesa Martin Mhando alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na tamasha hilo la 16 la kimataifa litakalohusisha nchi za Jahazi jijini Dar es Salaam.

 Alisema dhamira kuu ya tamasha hilo ni kuhakikisha kuwa ZIFF inaleta mabadiliko katika tasnia ya filamu hapa nchini kwani imekuwa ikitoa ajira za muda mfupi kwa washiriki wote na kuibua vipaji kwa kuzingatia kazi mbalimbali za sanaa na wasanii.

“Kupitia tamasha hili la 16 tunatarajia kutoa ajira za muda mfupi kwa washiriki wa filamu mbalimbali na kuibua vipaji kwani mara nyingi tumekuwa tukifanikisha malengo ya wasanii mbalimbali na kuwawezesha kuwa wasanii mahiri katika tasnia ya filamu,” amesema Prof. Mhando.

Naye Meneja Tamasha la ZIFF Bw. Daniel Nyalusi amesema kuwa tamasha limewahusisha watayarishaji wa filamu zaidi ya 35 mahiri kutoka nchi mbalimbali duniani ambao filamu zao zimechaguliwa kuingia ZIFF na kuwapa fursa hiyo maalumu kuongelea filamu zao na utengenezaji wa filamu kwa ujumla.

hapa nchini kuhudhuria kwa wingi na kupata nafasi ya kubadilishana mawazo na wenzao toka nchi mbalimbali ili kuweza kukuza vipaji vyao na kuweza kutoa filamu nzuri zitakazonyanyua soko la filamu hapa nyumbani.

“Miaka ya nyuma Tanzania hatukuwa na filamu nzuri katika soko la filamu hivyo kusababisha filamu za kinaijeria kuchukua nafasi kubwa na kuwafanya Watanzania wengi kufatilia filamu hizo, lakini kwa kipindi hiki filamu zetu zimekuwa zikija juu kwa kasi kubwa sana hivyo kuua soko la filamu za kinaijeria kitu ambacho ni kizuri kwa taifa letu,” amefafanua Bw. Nyalusi.

Alisema katika maandalizi ya tamasha hilo linalohusisha nchi za Jahazi ZIFF lilihusisha filamu 257 toka nchi mbalimbali ambapo filamu 80 zilifanikiwa kuchaguliwa, kuoneshwa ili kuweza kushindania tuzo za ZIFF za mwaka huu.

BFT Kufanya Uchaguzi Mkuu Julai 7

$
0
0

Mchezo wa Ngumi Tanzania

Yah: Uchaguzi wa viongozi wa Shirikisho la Ngumi Tanzania (BFT)

SHIRIKISHO la ngumi Tanzania (BFT) kwa kulingana na Katiba yake, sheria na kanuni za Baraza la Michezo la Taifa (BMT)linatarajia kufanya uchaguzi wa kuwapata viongozi wa kuongoza Shirikisho kwa kipindi cha miaka mine ijayo.

Uchaguzi huo unatarajia kufanyika tarehe 07/07/2013 jijini Mwanza, sambamba na mashindano ya majiji. Nafasi zitakazogombewa ni kama ifuatavyo:-
1. Rais.
2. Makamu wa Rais.
3. Katibu Mkuu.
4. Mweka Hazina.
5. Wajumbe tisa wa kamati ya utendaji kwa nafasi zifuatazo:-
i. Kamati ya Mipango na Fedha
ii. Kamati ya Wamuzi na Majaji
iii. Kamati ya Mashindano na Vifaa
iv. Kamati ya Walimu, Ufundi na Utafiti.
v. Kamati ya Uhusiano, Habari na Masoko
vi. Kamati ya Wanawake.
vii. Kamati ya Maendeleo ya Mikoa na Taasisi za Umma.
viii. Kamati ya Tiba.
ix. kamati za Maendeleo ya Vijana na Wachezaji.

Fomu zitaanza kutolewa kesho tarehe 04/06/2013 katika Ofisi za Baraza la Michezo la Taifa (BMT)

Usaili kwa wagombea wote utafanyika jijini Mwanza tarehe 05/07/2013

Ada ya fomu kwa wagombea zitatolewa kwa gharama zifuatavyo:-
• Kwa nafasi ya Rais ni Tsh. 150,000/=
• Kwa nafasi ya Makamo wa Rais, Katibu Mkuu na Mweka Hazina ni Tsh. 100,000/=
• Kwa nafasi za wajumbe wote tisa na Tsh. 50,000/=

Shirikisho linatoa wito kwa watanzania wenye uwezo wa kuongoza michezo kujitokeza kwa wingi kuchukua fomu za kugombea nafasi kama zilivyoelezwa hapo juu.

Taarifa hii inaletwa kwenu na

Makore Mashaga
Katibu Mkuu.

Barrick Gold Mining Watoa Milioni 10 Kudhamini Redd’s Miss Mara

$
0
0

Ofisa kutoka kitengo cha Mawasiliano na Mahusiano wa Barrick Gold Mining Fatuma Mssumi akimkabidhi Kaimu Ofisa Tawala wa Mkoa wa Mara mfano wa hundi yenye thamani ya Shilingi milioni 10, ikiwa ni sehemu ya udhamini wa kampuni hiyo kwenye mashindano la Redd’s Miss Mara yatakayofanyika leo mjini Musoma.


 

Baadhi ya washiriki wa shindano la Redd’s Miss Mara 2013 wakiwa katika picha ya pamoja jana ikiwa ni siku moja kabla ya warembo hao hawajapanda jukwaani kuwania taji hilo ambalo linashikiliwa na Miss Tanzania namba mbili 2012. Shindano hilo linataraji kufanyika leo.
 Baadhi ya washiriki wa Redd’s Miss Mara 2013 wakiwa wenye furaha.
Baadhi ya warembo wakiwa katika pozi

Baadhi ya washiriki wa shindano la Redd’s Miss Mara 2013 wakitembea kwa pamoja leo ikiwa ni siku moja kabla ya warembo hao hawajapanda jukwaani kuwania taji hilo ambalo linashikiliwa na Miss Tanzania namba mbili 2012. Shindano hilo linataraji kufanyika leo.

Mafuriko Yavamia Tamasha Ujerumani, Wasanii Waponea Chupu Chupu

$
0
0

Maji yakivamia eneo la tamasha

Mafuriko Yavamia Tamasha Ujerumani, Wasanii Waponea Chupu Chupu



JUMAMOSI
ya Juni Mosi 2013, katika viwanja vya maonesho ya Wurzburg Festival, ilikuwa ni majonzi na simanzi baada ya eneo hilo kukumbwa na mafuriko yalisababisha hasara kubwa na kuvunjwa kwa tamasha hilo lililokuwa likisherekea maadhimisho ya miaka 25.

Habari za uhakika zimevuja kuwa vikosi vya zimamoto na wanausalama viliingiwa na mashaka baada ya wasanii wa Ngoma Africa Band a.k.a FFU, kutoweka ghafla katika chumba cha kubadilishia nguo (back Stage) na kutojulikana waliko. Wasiwasi ulitanda zaidi baada ya watu kuhisi watakuwa wamezolewa na mafuriko!

Hata hivyo hofu iliondoka baada ya saa kadhaa ambapo watayarishaji waligundua kuwa mkuu wa bendi hiyo field-marshal Kamanda Ras Makunja alikiondoa kikosi chake baada ya makachero wa bendi hiyo maarufu kama “Anunnaki Empire” kumtonya boss wao kuwa eneo la festival sio salama.

Mto ulio jirani na eneo hilo ulijaa maji kablda ya kadhia hiyo, hivyo Kamanda bila kuaga alikiondoa kikosi cha FFU wa Ngoma Africa katika hali ya usiri na kuwanusuru vijana wake na kuzima simu hadi baada ya saa fulani ndipo ikawashwa na kuwajulisha waandalizi wa onesho wasiwe na shaka kamanda na kikosi cha Ngoma Africawapo salama kambini, kitendo hiko kiliwaacha midomo wazi baadhi ya wadau! Wengine kudiriki kusema kuwa ‘Simba ni Simba’.

Tamasha hilo lilianza Mai 31, 2013 kukiwa na maelfu ya watu na wasanii mbali mbali walioalikwa wakiwamo mkongwe Manu Dibando, Alfa Blondy, Salifu Keita ndio walioanza kufungua dimba, Ijumaa hiyo hali ilikuwa shwari lakini ilipofika jumamosi hali ya hewa ilianza kubadilika kwa mvua na upepo,wasinii wengine wakiwa kwenye vyumba vya kujitayarishia miongoni mwao wakiwamo “Ngoma Africa band ” a.k.a FFU Ughaibuni, baada ya hali ya hewa kuanza kubadilika kwa upepo na mvua ndio.

inasemekana kuwa Kamanda Ras Makunja na kikosi chake Ngoma Africa band, Kuondoka katika eneo la festival (eneo la hatari) lilikumbwa na maji, katika mazingira ya ajabu. Watonyaji wa habari wamedai kuwa walitoroshwa kwa magari mawili meusi aina ya van yalikuwa na madilisha ya kiza.Kamanda Ras Makunja kateleza kama nyoka na kikosi chake. Mafuliko hayo yamevamia pia baadhi ya miji nchini Ujerumani na ulaya ya mashariki ka kusababisha vifo vya watu 12.

DATK Entertainment Ltd Inawaletea Redd’s Miss Tanga 2013

$
0
0

DATK Entertainment Ltd Inawaletea Redd’s Miss Tanga-Redd’s Miss TANGA 20013


DATK Entertainment Ltd Inawaletea Redd’s Miss Tanga

Bondia Kaseba Kuzipiga Rasco Chimwanza wa Malawi

$
0
0

Japhet Kaseba akitunisha misuli mbele ya Anthony Ruta ambaye alikuwa akisimamia zoezi zima la upimaji akisaidiwa na Ibrahim Kamwe ‘bigright’

Baadhi ya mabondia wengine watakao pigana jumamosi ddc magomeni

BONDIA Japhet Kaseba leo amepima tayari kumkabili mpinzani wake Rasco Chimwanza kutoka nchi ya Malawi katika pambano la ubingwa wa kimataifa.

Zoezi zima la upimaji lilisimamiwa na Anthony Ruta, Ibrahim Kamwe, Pendo Njau na doctor John Lugambila wa muhuimbili na kueleza kuwa mabondia wote wapo katika hali nzuri ya ushindani. Kwa upande wake Jafet Kaseba amejinadi kumsambaratisha mpinzani wake katika raundi za mapema za mchezo huo.

Pia kutakuwepo na mapambano ya utangulizi kama Juma Fundi atazipiga na Hasan Kiwale (moro best), Josef Onyango toka Kenya atazipiga na Seba Temba wa Morogoro, huku Issa Omar-peche boy atakapomvaa bondia mkongwe Juma Seleman na mapambano mengineyo mengi yatapigwa katika ukumbi huo wa DDC Magomeni Kondoa.

Hata hivyo katika hali ambayo si ya kawaida kwa vyama vya ngumi hapa nchini kuwa pamoja kikazi katika mapambano wanayoyasimamia, kwa pambano la jumamosi itakuwa tofauti kwa baadhi ya maofisa wa chini wa vyama vya ngumi kusimamia mapambano kwa pamoja na kuua tofauti zao, na kujirudi kuwa wao ni wamoja katika michezo.

Wajue Washindi wa Tuzo za Muziki za Kilimanjaro

$
0
0

Matokeo ya Washindi wa Tuzo za Kilimanjaro

-Wimbo bora wa Mwaka wa Taarab: Mjini Chuo Kikuu (Khadija Kopa)

-Kikundi bora la taarab: Jahazi Modern Taarab

-Mtunzi Bora wa Mashairi ya taarab: Thabit Abdul

-Mtayarishaji bora wimbo wa taarab: Enrico

-Msanii Bora wa Kike Taarab: Isha Mashauzi

-Msanii Bora wa Kiume wa Taarab: Mzee Yusuf

-Wimbo wenye vionjo vya asili: Chochea (Mrisho Mpoto)

-Msanii Bora wa Mashairi ya Bongo Fleva: Ben Pol

-Mtayarishaji bora wa mwaka Bongo Fleva: Man Walter

-Msanii Bora wa Kiume Bongo Fleva: Diamond

-Msanii Bora wa Kike Bongo Fleva: Rachel

-Wimbo Bora Bongo Pop: Ommy Dimpoz

-Msanii Bora anayechipukia: Ally Nipishe

-Kikundi Bora cha Kizazi Kipya: Jambo Squad

-Mtayarishaji Bora Wimbo wa Chipukizi: Mene Selekta

-Wimbo Bora wa Kiswahili: Risasi Kidole (Mashujaa Band)

-Mtunzi Bora Mashairi ya Bend: Chaz Baba

-Mtayarishaji Bora wa Wimbo wa Bend: Amoroso

-Msanii Bora wa Kike wa Bend: Luiza Mbutu

-Msanii Bora wa Kiume wa Bend: Chaz Baba

-Rapa Bora wa Bend: Fagason

-Band Bora ya Mwaka: Mashujaa

-Wimbo Bora wa Zuku: Niwewe (Amin)

-Wimbo Bora wa Regge: Warriors (From East)

-Wimbo Bora wa Ragga: Prideta

-Msanii Bora wa Hip Hop: Kala Jeremiah

-Mtunzi Bora Mashairi ya Hip Hop: Kala Jeremiah

-Wimbo Bora wa Hip Hop: Ney Wamitego

-Wimbo wa Kushirikiana: Me & U (Ommy Dimpoz)

-Wimbo Bora wa Mwaka: Dear God (Kala Jeremiah)

-Video Bora ya Mwaka: Ommy Dimpoz(Baadae)

-All Fame (Kilimanjaro Band, Wana njenje)

-Individual All Fame: Salum Abdallah Yazidu

-Msanii Bora wa Kike: Lady Jay Dee (Joto Hasira)

-Msanii Bora wa Kiume wa Mwaka: Diamond (Kesho)

Bondia Japhet Kaseba Amchapa Mmalawi kwa TKO

$
0
0

Bondia Japhet Kaseba kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana masumbwi na Rasco Simwanza wa Malawi wakati wa mpambano wao wa Ubingwa wa Kimataifa wa PST mpambano uliofanyika Dar es salaam jana Kaseba alishinda kwa TKO ya raundi ya sita.

Bondia Japhet Kaseba akiwa amevishwa mkanda wake wa kimataifa wa PST

BONDIA Jafet Kaseba wa Tanzania amemshinda bondia Rasco Chimwanza wa kutoka Malawi katika pambano la ubingwa lililofanyika Ukumbi wa DDC Magomeni Kondoa, ukumbi ambao kwa sasa umesahaulika na kuwa katika hali mbaya ya kiuchakavu.

Kaseba ameshinda mpinzani wake kwa TKO katika ’round’ ya sita baada ya M-malawi Chimwanza kushindwa kuendelea kufuatia makonde mfululizo aliyotupiwa na mpinzani wake, ambaye alionekana kutokuwa na wasiwasi na kucheza chini ya kiwango kilichotarajiwa.

Kabla Jafet Kaseba hajatoana jasho na mpinzani wake kulikuwepo na mapambano zaidi ya nane ya utangulizi ambayo yalikuwa makali na kusisimua, kati ya hayo ni bondia mdogo Issa Omar alitwangana na mkongwe Juma Seleman katika pambano lililokuwa na mvuto na kuwafanya watu muda wote washindwe kukaa katika viti.

Omar alimshinda mkongwe huyo, pambano lingine Juma Fundi alimsambaratisha Moro Best kwa kichapo kikali, huku Kamanda wa Makamanda alishindwa vibaya na Ibrahim Maokola. Mgeni mwalikwa wa pambano hilo mamaa Dotnata alimvisha kaseba mkanda wa ubingwa na kuahidi kuandaa pambano la ngumi kwa siku zijazo na hasa kati ya Alphonce Mchumiatumbo na Iddi Bonge.

Washiriki Redd’s Miss Tanga Kufanya Usafi na Kutembelea Wagonjwa

$
0
0

Warembo wanaowania shindano la kumtafuta mlimbwende wa Mkoa wa Tanga ‘Redd’s Miss Tanga 2013′ wakiwa katika pozi mara baada ya kumalizika mazoezi yao kwenye ukumbi wa Lavida Loca jijini Tanga. Shindano hilo linatarajiwa kufanyika June 22 mwaka huu katika uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga.

Na Mwandishi Wetu, Tanga

WAREMBO wanaowania umalkia wa Mkoa wa Tanga “Redd’s Miss Tanga 2013” wanatarajiwa kushiriki katika shughuli za usafi wa mazingira mkoani Tanga “Kalembo Day” June 15 mwaka huu na baadae kutembelea wagonjwa katika hospitali ya Mkoa wa Tanga, Bombo kuwaona wagonjwa na kutoa zawadi anuai.

Shughuli hizo za usafi watazifanya katika maeneo mbalimbali jijini Tanga siku hiyo ambayo ni siku maalumu ya usafi katika mkoa wa Tanga wakati wakiwa wanajiandaa na shindano hilo ambalo litafanyika June 22 mwaka huu kwenye uwanja wa Mkwakwani.

Siku mbili baada ya warembo hao kumaliza zoezi hilo watakwenda kutembelea vivutio vya utalii na maeneo ya kihistoria yaliyopo mkoani hapa June 17 mwaka huu lengo likiwa ni kujifunza utalii wa ndani ili kuweza kupata fuksa nzuri ya kuweza kuutangaza kwa wageni na wenyeji.

Vivutio ambavyo warembo hao wanatarajiwa kutembelea ni Mbuga ya Wanyama ya Sadani na Mapango ya kihistoria ya Amboni yaliyopo jijini Tanga ambapo watapata fursa ya kuona na kujifunza mambo mbalimbali yanayohusu maeneo hayo.

Shindano hilo linatarajiwa kufanyika 22 kwenye Uwanja wa Mkwakwani mkoani hapa ambapo litapambwa na wasanii nguli wa muziki wa bongo fleva nchini ili kuweza kuwapa burudani wakazi wa mkoa huu ambao watajitokeza kushuhudia kinyang’anyiro hicho.

Mkurugezi wa Kampuni ya DATK Intertaimeint, Asha Kigundula, ambaye ndiye muandaaji wa shindano hilo alisema shindano hilo litakuwa la aina yake kutokana na kushirikishs warembo bomba.

Alisema kuwa warembo hao tayari wanaedelea na mazoezi kwenye Ukumbi wa Lavida uliopo jijini Tanga ambapo tayari wameshaanza kuwateka wadau wa tasnia hiyo ambao wamekuwa wakijitokeza kila siku kushuhudia mazoezi hayo.

“Ninachoweza kusema shindano la mwaka huu litakuwa la aina yake kutokana na kusheheni warembo bomba wenye mvuto na hivyo kuonyesha kutakuwa na mchuano mkali miongoni mwao,” alisema Kigundula

Shindano hilo litaanza saa 2, usiku na kueleza kuwa maandalizi ya shindano hilo yanaendelea vizuri na jumla ya warembo 12 watashindania taji hilo ambalo hivi sasa linashikiliwa na Miss Tanga 2012 Teresia Kimolo.

Warembo hao ni Hawa Ramadhan (18), Hazina Mbaga (19) Like Abdulraman (19), Jack Emmanuel (18), Wahida Hashimu (20), Tatu Athuman (19), Mwanahamis Mashaka (20), Neema Abdallah (18), Winfrida Gutram (21), Lulu Mbonea (19), Aisha Rashid (21), Azina Daniel (19), Lulu Matawalo (22), Judithi Moreli (21), na Hawa Twaybu (21).

Alisema kwamba shindano la mwaka huu litaandika historia mpya ya urembo mkoani humo kwa kuwa Kampuni DATK imejipanga vilivyo, hivyo kuwaomba mashabiki wa mashindano ya urembo wa jijini hapa kwa ujumla wakae mkao wa kupata raha.

Redd’s, Miss Tanga, imedhaminiwa na Dodoma Wine,CXC Africa, Executive Solutions, Busta General Supply, Mkwabi Interprises, Lusindic Investment LTD, Lavida Pub, Jambo Leo, Staa Spoti, Five Brothers Cloud’s Media Group, pamoja na Blog Michuzi Media Group, Bongostaz.com, Thehabari.com, Saluti5, Kajuna, Jane John, Kidevu na assengaoscar blog.

Zuku Pay Tv Yazindua Zuku Swahili Movies chanel

$
0
0


ZUKU Pay Tv imezindua Zuku Swahili Movies chaneli namba 210 ambayo ni watakua wakionesha burudani za muziki na filamu za kiswahili.

Tukio hili la kifalme lilitekwa utamaduni wa kiswahili na kuthamini historia ya filamu nchini Tanzania na kuthamini mchango wa waenzi pamoja na nyota mpya wa sekta ya filamu.
Waigizaji, wakuzaji wa filamu wa Arusha na Dar es Salaam walikaribishwa kwa kapeti nyekundu.

Akizungumza katika uzinduzi wa Zuku Kiswahili Channel, Mohammed Jenneby Mkurugenzi Mtendaji Wananchi Satellite alionyesha matumaini yake na kueleza mkakati wa biashara kwa zaidi ya wateja million mia moja katika kanda ya Afrika Mashariki. “Kiswahili ni lugha ambayo inawaunganisha wakazi wa Afrika Mashariki, Kati na Kusini. Lugha ya Kiswahili itaendeleza jukumu muhimu ya kuleta maendeleo ya kanda. Chaneli ya Zuku Swahili inasherekea maendeleo yetu na pia kukuza nje utamaduni wetu kupitia filamu duniani

Mtange wa Satelitie wa Zuku hupatikana kwa nchi 15 Afrika Mashariki na kampuni ya Wananchi inalengo la kupanua utaambazi wake kufikia nchi 40 hivi karibuni. Kampuni pia imeelezea nia yake ya kuendelea kuwekeza katika kanda ya Afrika Mashariki

Zuku Swahili Channel 210 inajivunia filamu bora, sinema na burudani ya kiswaili kutoka Tanzania na inelenga kujumuisha uzalishaji kutoka Uganda, Kenya, Rwanda na DRC katika miezi ijayo.

Zuku Kiswahili Channel 210 inaonyesha filmau, michezo ya kuigiza, majadiiano na muziki. Chaneli hii inapatikana katika vifurushi vya Zuku Poa, Zuku Classic, na Zuku Premium

Fadhili Mwasyeba, Meneja Mkuu Zuku Tanzania aliwashukuru wazalishaji na watunga filamu ambao wameshirikiana na Zuku kuzindua chaneli hii. “Kampuni inaendelea kutafuta filamu bora; nia yetu ni kununua haki za kuonyesha filamu hiii kwenye jukwaa letu la Zuku Pay TV. Tunawakaribisha watengenezaji wa filamu katika kanda ya Afrika Mashariki kutumia jukwaa letu na kufanya biashara na sisi, alisema.

“Ili kuhakikisha tunakutana na watunga filamu wote tutakuwa na msafara wa Zuku Caravan ambao utatembea kote nchini. Tunawahimiza wadau wote kukutana na kufanya biashara nasi” alisema Bw. Mwasyeba.

Ziara ya kwanza ya msafara utaanza Arusha tarehe 15 Juni Arusha na baadaye kutembelea mikoa ya Moshi, Mbeya, Iringa, Morogoro, Dodoma, Shinyanga, Bukoba na Dar es Salaam.

Wizara ya Afya Wapokea Msaada wa Magari ya Wagonjwa

$
0
0

Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dk. Donan Mmbando akiponyeza kitufe cha kingora katika moja ya magari ya wagonjwa kama ishara ya kuyapokea magari manne ya wagonjwa kutoka kwa wahisani ambao ni Plan International na Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Canada (CIDA) katika halfa iliyofanyika jana. Picha na Lorietha Laurence- Maelezo.

Redd’s Miss Kinondoni 2013 Kufanyika Golden Tulip Juni 21

$
0
0

Kila mmoja akiwa na furaha na bashasha, baada ya mkutano na waandishi wa habari warembo walipata nafasi ya kutembelea ofisi za wadhamini wao ambao ni Oriflame Natural Beauty Products zilizopo jengo la Mkapa jijini Dar es Salaam, na hapo waliweza kupata semina ya kuelezewa jinsi vipodozi vyao vinavyofanya kazi kama pichani unavyoona mwezeshaji akitoa somo kwa warembo.

Mratibu wa shindano la Redd’s Miss Kinondoni 2013, Deniss Ssebo akiongea na waandishi wa habari kuhusiana na shindano hilo, alisema kuwa mwaka huu imeleta mapinduzi Makubwa katika sekta ya Afya, Elimu pamoja na Ajira.

Ambapo mshindi wa kwanza atapata udhamini wa masomo (Scholarship) kwa muda wa mika miwili katika kuendeleza masomo yake na kama amemaliza kusoma basi atapa ajira kwenye hoteli ya kimataifa ya JB Belmonte kulingana na elimu aliyonayo. Pia atapata shopping vocha kutoka Oriflame ya tshs. 300,000 pamoja na fedha taslimu tshs. 500,000.

Mshindi wa pili;  atapata udhamini wa masomo (Scholarship) ya mwaka mmoja, fedha taslimu 300,000 na shopping vocha kutoka Oriflame ya tshs. 200,000.

Mshindi wa tatu;  atapata udhamini wa masomo (Scholarship) ya mwaka mmoja, fedha taslimu 200,000 na shopping vocha kutoka Oriflame ya tshs. 100,000.
Mshindi wa 4 na tano; watapata uthamini wa masomo ya kompyuta ya miezi sita. Mshindi wa nne atapata pia pesa taslimu laki mbili  na nusu na wa 5 laki moja na nusu.Washiriki wengine wote watapata kifuta jasho cha shilingi laki mbili kwa kila mmoja.

Mashindano ya Redd’s Miss Kinondoni 2013 yanatarajia kufanyika kwenye ukumbi wa hoteli ya Golden Tulip siku ya Ijumaa 21 June 2013. Viingilio katika onyesho hilo ni shs. 60,000 VIP, shs. 25,000 kwa tiketi za kawaida na meza ya watu ukitazama zawadi.

Mashindano ya Redd’s Miss Kinondoni yanatarajiwa kufanyika June 21, huku walowa yamedhaminiwa na Redd’s Original, Chilly Willy Energy Drink, Oriflame Natural Beauty Products, Times Fm, JB Belmonte Hotel, Michuzi Media Group, Michuzijr Blog, Mtaa Kwa Mtaa Blog, Fullshangwe Blog, Mrokim Blog, SufianMafoto Blog, Global Publisher, Mdimuz Blog, Lukaza Blog, MO Blog, DjChoka Blog na Kajunason Blog.
 Muonekano wa warembo wa Redd’s Miss Kinondoni 2013.
 Kila mmoja akiwa na furaha na bashasha.
 Baada ya mkutano na waandishi wa habari warembo walipata nafasi ya kutembelea ofisi za wadhamini wao ambao ni Oriflame Natural Beauty Products zilizopo jengo la Mkapa jijini Dar es Salaam, na hapo waliweza kupata semina ya kuelezewa jinsi vipodozi vyao vinavyofanya kazi kama pichani unavyoona mwezeshaji akitoa somo kwa warembo.
 Mmoja ya warembo wa Redd’s Miss Kinondoni 2013 akiuliza swali kwa mwezeshaji.
Kila mrembo akijaribu kuweka kumbu kumbu kwa yale waliyokuwa wakifundishwa.

Redds Miss Kinondoni 2013 Wafanya Harambee Kusaidia Hospitali Mwananyamala

$
0
0

Warembo wa Redds Miss Kinondoni 2013 wakitambulishwa kwa Naibu Mustahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni Songolo ambaye alimwakilisha mgeni rasmi meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda. Mgeni huyo pia alipata fulsa ya kuzinduliwa rasmi kambi ya Redds Miss Kinondoni 2013 iliyopo katika hoteli ya JB Belmont jijini Dar es Salaam.

Naibu Mustahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni Mheshimiwa  Songolo ambaye alimwakilisha mgeni rasmi meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda akiongoza harambee ya kuchangisha fedha kwa ajili ya kununua vitanda kwa ajili ya akina mama wanaojifungua (delivery beds) kwa hospitali za Mwananyamala pamoja na Sinza Palestina ambapo warembo hao walitembelea wodi za akina mama na kufanya usafi. Pamoja na harambee kulizinduliwa rasmi kambi ya Redds Miss Kinondoni 2013. Pembeni ni Mkuu wa Itifaki wa Mashindano ya Miss Tanzania, Albert Makoye na Mratibu wa shindano la Redd’s Miss Kinondoni Bw. Ssebo. Harambee hiyo ilifanyika ukumbi wa Ambassador uliopo hoteli ya JB Belmont jijini Dar es Salaam. 
Jumla ya vitanda 15 vyenye thamani ya shilingi milioni 52.5 zimepatikana katika harambee iliyoandaliwa na warembo wa Redds Miss Kinondoni 2013 kwa ajili ya kununua vitanda kwa ajili ya akina mama wanaojifungua (delivery beds) kwa hospitali za Mwananyamala pamoja na Sinza Palestina iliyofanyika katika ukumbi wa Ambassador uliopo hoteli ya JB Belmont jijini Dar es Salaam. 

Akizungumza mshiriki wa shindano hilo, Sarah Paul alisema kuwa wanamshukuru Mungu kwa kuweza kuwawezesha kufanya harambee hiyo ambayo ilitokana na wao baada ya kutembelea hospitali ya Mwananyamala pamoja na Sinza Palestina wakajionea uhaba wa vitanda vya akina mama wakati wa kujifungua.

“Tulisononeshwa sana na hali tuliyoikuta hospitalini hapo ambapo baada ya kuongea na mganga mkuu wa Manispaa ya Kinondoni dokta Gunini Kamba alitueleza kuwa jumla ya akina mama wapatao 50 mpaka 80 hujifungua kwa siku moja hivyo wanauhaba wa vitanda, tukaona tukae na viongozi wetu watusaidie kuandaa harambee na tunamshukuru Mungu tumefanikiwa kupata vitanda 15 japo nia yetu ilikuwa ni kupata vitanda 20,” alisema mrembo huyo.

Mashindano ya Redd’s Miss Kinondoni 2013 yanatarajia kufanyika kwenye ukumbi wa hoteli ya Golden Tulip siku ya Ijumaa 21 June 2013. Viingilio katika onyesho hilo ni shs. 60,000 VIP, shs. 25,000 kwa tiketi za kawaida na meza ya watu ukitazama zawadi.

Warembo wa Redds Miss Kinondoni 2013 walipata fulsa ya kucheza mara baada ya harambee na ufunguzi rasmi ya kambi yao. 
Furaha zilitanda.
Kila mmoja akionyesha ufundi wake.
Mashindano ya Redd’s Miss Kinondoni yamedhaminiwa na Redd’s Original, Chilly Willy Energy Drink, Oriflame Natural Beauty Products, Times Fm, JB Belmonte Hotel, Michuzi Media Group, Michuzijr Blog, Mtaa Kwa Mtaa Blog, Fullshangwe Blog, HandeniKwetu Blog, Mrokim Blog, TheHabari.com, JestinaGeorge Blog, SufianMafoto Blog, Global Publisher, Mdimuz Blog, Lukaza Blog, MO Blog na Kajunason Blog.

Happiness Watimanywa Aibuka Redds Miss Kanda ya Kati

$
0
0

Mshindi wa taji la Redds Miss Kanda ya Kati Happiness Watimanywa (Katikati) akiwa na nyuso ya furaha mara baada ya kamati ya majaji kumtangaza mshindi katika kinyang’anyiro kilichoshirikisha walimbwendwe 12 kutoka Mikoa ya Dodoma, Singida, Tabora na Kigoma Wa Kwa Kwanza kulia Ni Mshindi wa Tatu Jackline huku Mshindi wa Pili ni (wa kwanza kushoto) Sabrina Juma Kutoka mkoani Tabora


Jaji Mkuu wa Shindano ya Kumsaka Mlimbwende wa Kanda ya Kati, Hashim Lundenga akipungia mikono kwa Watanzania waliofika kushuhudia mlimbwende wa Kanda ya kati anapatikana.
Mshiriki wa kinyang’anyiro Cha Redds Miss Kanda ya Kati Hawa Nyange akijitambulisha. 
 Mmoja wa washiriki wa kinyang’anyiro Cha Kumtafuta Mlimbwende wa Kanda ya kati akijitambulisha mbele ya hadhara.
 Muda wa Kuonyesha Vipaji ukawadia.
 Mavazi ya Ubunifu.
 Walimbwende walioingia hatua ya Tano Bora.
 Wadau wa Miss Tabora wakifuatilia shindano kwa ukaribu.
Mratibu na mwandaaji wa Redds Miss Kanda ya Kati akizungumza pembeni yake ni Mgeni Rasmi (katikati), Mbunge, John Komba akiwa na baadhi ya wabunge wenzake kutoka Zanzibar.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Amin akicheza na mmoja wa mashabiki wake ambaye alikua akiigiza kama Linah jana wakati wa shindano la kumtafuta Redds Miss Kanda ya Kati.
Mmoja wa mashabiki wakimtunza Amin wakati alipokuwa akitoa burudani katika Kinyang’anyiro cha kumtafuta Mlimbwende wa Kanda ya Kati
Baadhi ya wadau waliojitokeza kwenye kushuhudia Shindano la Redds Miss Kanda ya Kati lililofanyika Usiku wa Kuamkia Leo Katika Ukumbi wa Kilimani Mkoani Dodoma. Picha zote Na Josephat Lukaza Wa Lukaza Blog.

Redd’s Miss Kinondoni Talent 2013 Kufanyika Juni 20

$
0
0

Warembo wa Redds Miss Kinondoni 2013 wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kutambulishwa mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani), kwa sasa warembo hao wameshaingia katika hoteli ya JB Belmont jijini Dar es Salaam kujinoa kwa ajili ya Redd’s Miss Kinondoni Talent 2013 zinazofanyikia ukumbi wa Shekinah Garden Mbezi Beach na Fainali zinafanyika Juni 20 ukumbi wa hoteli ya Golden Tulip.

Na Cathbert Angelo, Wa Kajunason Blog

SHINDANO la Redd’S Miss Kinondoni Talent 2013 linatarajiwa kufanyika Alhamisi ya Juni 20 katika ukumbi wa Shekinah Garden, Mbezi Beach jijini Dar es Salaam ambalo litashirikisha warembo wapatao kumi na mbili ambao watachuana kumpata mrembo mwenye kipaji.

Akizungumza Mratibu wa Shindano hilo, Dennis Ssebo alisema maandalizi ya kuelekea shindano hilo yanaendelea vizuri na kueleza mshindi atakabidhiwa zawadi zake kwenye fainali ya shindano hilo ambalo litafanyika Juni 21 mwaka huu katika uwanja wa hoteli ya Golden Tulip.

“Ninachoweza kusema shindano la mwaka huu litakuwa la aina yake kutokana na kusheheni warembo bomba wenye mvuto na hivyo kuonyesha kutakuwa na mchuano mkali miongoni mwao,” alisema Ssebo.

Warembo warembo wanaotarajiwa kumenyana ni kutoka katika vitongoji vya Sinza, Ubungo na Dar Indian Ocean ambao kwa pamoja wanaunda Redd’s Miss Kinondoni 2013.

Alisema kwamba shindano la mwaka huu litaandika historia mpya ya urembo kwa wilaya ya Kinondoni maana wamejipanga na kupata sapoti ya kutosha, hivyo mashabiki wa mashindano ya urembo wakae mkao wa kupata raha.

Mashindano ya Redd’s Miss Kinondoni yamedhaminiwa na Redd’s Original, Chilly Willy Energy Drink, Oriflame Natural Beauty Products, Times Fm, JB Belmonte Hotel, Michuzi Media Group, Michuzijr Blog, Mtaa Kwa Mtaa Blog, Fullshangwe Blog, HandeniKwetu Blog, Mrokim Blog, TheHabari.com, JestinaGeorge Blog, SufianMafoto Blog, Global Publisher, Mdimuz Blog, Lukaza Blog, MO Blog na Kajunason Blog.

Mpigie kura Amir Nando abaki ndani ya nyumba!

$
0
0

Amir anashiriki kwenye “Big Brother Africa”.

Kwa sasa hivi anahitaji msaada wetu …Amir is up for eviction this week… Naomba tumpe vote ili asitolewe. Vilevile naomba tuhamasishe ndugu, jamaa, na marafiki wa nchi mbalimbali wampe vote.
…Please vote #TeamNando…NO EVICTION TO TEAM NANDO……LET’S SUPPORT HIM PLEASE!!!.. at http://bigbrotherafrica.dstv.com/vote/

Tunamtakia ushindi!

20130619-074258.jpg

Mabondia Juma Fundi na Nasibu Ramadhani Kupambana Siku ya Iddi

$
0
0

Bondia Juma Fundi kushoto na Nasibu Ramadhani wakitambulishwa na Promota wa mpambano huo, Side Mkigoma.

Bondia Juma Fundi kushoto akitunishiana misuri na Nasibu Ramadhani wakati wa utambulisho wa mpambano wao utakaofanyika sikukuu ya Idi pili wengine kushoto ni mratibu Duni Lianjara Promota wa Mpambano huo Side Mkigoma na kocha wa Nasibu Christpher Mzazi.

Mabondia Juma Fundi na Nasibu Ramadhani wakisaini mikataba ya pambano lao. (Picha na super d blog)

Viewing all 521 articles
Browse latest View live