Quantcast
Channel: Michezo na Burudani – Tanzania Habari | Jamii | Michezo | Mahusiano | Kazi | Thehabari.com
Viewing all 521 articles
Browse latest View live

Bondia Fadhili Majia Ashinda Kombe la Masumbwi Kimataifa Indonesia

$
0
0

Bondia Fadhili Majia akiwa na kombe la ubingwa wa ngumi kimaifa alilolinyakua nchini Indonesia wiki iliyopita alipo mpiga bondia, Heri Amol akilakiwa baada ya kurudi Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni Kocha wa masumbwi nchini Super D wengine ni mabondia Japhet Kaseba, Kanda Kabongo na Pendo Njau. (Picha na Super ‘D’ blog )


Ngoma Africa Band Watuma Rambirambi Msiba wa Bi. Kidude, Wasitisha Shughuli za Muziki Siku 10..!

$
0
0

Marehemu Bi. Kidude akiimba enzi za uhai wake

BENDI maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya “Ngoma Africa Band” imepokea kwa hudhuni na majonzi makubwa taarifa ya kifo cha mwanamuziki mkongwe barani Afrika hayati Bibi Fatuma binti Baraka (Bi.KIDUDE) na kutaka mwenyezi Mungu amrehemu.

Ngoma Africa band inatoa mkono wa pole na rambirambi kwa familia ya marehemu Bi.Kidude, pia kwa Watanzania wote walioguswa na msiba huo, hasa wanamuziki kwa kuondokewa na mkongwe wetu Bi. Fatuma Binti Baraka (Bi.Kidude),ambaye alikuwa ni balozi na hadhina ya utamaduni wa muziki wa mwambao na waswahili, kitaifa na kimataifa.
Marehem Bi. Kidude hakuwa msanii au mwanamuziki tu bali alikuwa mpiganaji jemedari aliyeupigania na kuulinda utamaduni wa jadi ya Kiswahili na muziki wa mwambao.

Bendi ya Ngoma Africa inaungana na watanzania wote wa ndani na nje ya nchi katika kuomboleza msiba huu wa mkongwe wa sanaa barani barani Afrika hayati Bibi. Fatuma Binti Baraka (Bi. Kidude), Ngoma Africa band itasimamisha shuguli za kutumbuiza kwa muda wa siku 10 kuanzia sasa kwa ajili ya maombolezo ya msiba wa marehemu Bi. Kidude.

Mwenyezi mungu amlaze mahala pema peponi Bibi.Fatima binti Baraka (Bi.Kidude)
Amin.

Tanzania Watolewa Mashindano ya Guinness Football Challenge

$
0
0

Washindi wa kipindi cha tano cha Guinness Football Challenge Ken Muturi (kushuto) na Chis Mwamgi(kulia) wakishangilia ushindi walioupata huku wakiwa wamebeba pesa taslimu walizojishindia katika shindano hilo jana usiku na pembeni ni mmoja wa watangazaji wa kipindi hicho Lary Asengo (anayepiga makofi kulia).

Washindi wa kipindi cha Tano cha Guinness Football Challenge, Chris Mwamgi(kushoto)  na Ken Muturi(kulia) katika picha ya pamoja na watangazaji wa kipindi hicho Larry Asego and    Flavia Tumsiime jana baada ya ushindi.

*Washindwa Kufanya Vizuri Kipindi cha Tano cha Guinness Football Challenge

JANA usiku (17 Aprili 2013) kupitia Televisheni za ITV na Clouds TV timu ya Tanzania ilishindwa kutumia nafasi ya kipindi cha mwisho cha mashindano ya “Guinness Football Challenge” katika hatua ya Afrika Mashariki baada ya kutolewa na timu kutoka Kenya.

Rangi nyekundu imeonekana kuwa ni rangi ya bahati kwa timu za Kenya kwani hii ni timu ya nne kutoka Kenya kufanikiwa kufuzu kuingia hatua ya Pan-African GUINNESS® FOOTBALL CHALLENGETM. Kenneth Mukuri na Chris Mwamgi ndio walioibuka washindi jana usiku kwani walifanikiwa kufika katika hatua ya mwisho ya kulenga ukuta wa pesa wa Guinness ambapo walijishindia dola za kimarekani 1,500.

Ni vipi Kenneth na Chris wataweza kumudu hatua ya Pan – African? Sasa wana nafasi ya kuiwakilisha nchi yao katika mashindano ya Pan-African ambapo watakutana na wawakilishi pekee kutoka Tanzania, Daniel Msekwa na Mwalimu, washiriki kutoka Uganda Alex Muyobo na Ibrahim Kawoova pamoja na wenzao kutoka Kenya, Francis Ngigi na Kepha Kimani(washindi wa kipindi cha 2), Kenneth Kamau na Wills Ogutu(washindi kipindi cha 3) na Ephantus Nyambura na Samuel Papa (washindi kipindi cha 4).

Timu hizi tano zitakua uwanjani kutimiza malengo yao, ambapo watakutana uso kwa uso na washiriki kutoka Ghana na Cameroun kuonesha ni nani ana maarifa zaidi na ujuzi wa kusakata kabumbu, hata kuvishwa ubingwa wa Pan-African na kuondoka na dola za kimarekani 250,000. Usikose kuangalia mashindano haya kupitia televisheni za ITV na Clouds TV huku ukiburudika na kinywaji cha GUINNESS.

Tafadhali kunywa kistaarabu – Hairuhusiwi kwa wenye umri chini ya miaka 18.

Mabondia Juma, Kibuga na Kaoneka Kuhamasisha Ngumi Chalinze

$
0
0

MABONDIA Mwaite Juma, Cosmas Kibuga na Shabani Kaoneka ni baadhi ya mabondia wa Dar es Salaam watakaokwenda Chalinze kuhamasisha ngumi za kulipwa wilayani humo kwa kuzipiga na mabondia wakali wa Chalinze.

Kampuni inayoandaa mapambano kwa ajili ya kunyanyua vipaji vya mabondia machipukizi ya Bigright Promotion, imaeandaa pambano hilo ili kutanua wigo wa michezo nchini kwa kuanzia kutembelea wilaya zinazohamasika kimchezo ikiwemo chalinze.

Tumeamua kufanya chalinze kwa sababu tunataka chalinze iwe ndio mfano kwa kuandaa pambano hili ambalo litawakutanisha chipukizi wakali wa dar na wakali wa chalinze, pia kutakuwepo na mapambano mengine yenye ushindani wa hali ya juu na vituko kama vile la Pius puto atakaezipiga na iddi mkatatiketi – hawa ni mbabe wa sokoni na mbabe wa stendi watazipiga kumaliza ubishi wao uliotanda kwa muda mrefu.

Ukiondoa pambano hilo Minyusi abdala atazipiga na shaban kaoneka, Baraka nuhu”chalinze hamjambo” atazipiga na goodluck suleiman, alex kdo atazipiga na herman shekivuli, iddi mwera atazipiga na ramadhan misugwa na mapambano mengineyo mengi likiwemo la ustadh mwenye msimamo mkali ustadh Kurasheni aliyeahidi kuchinja kama anachinja kondoo ulingoni atakaezipiga na makali wa bodaboda mzee kachacha.

Mgeni rasmi wa pambano hilo atakuwa ni diwani wa Chalinze bwilingu bw naser Karama ambaye muda wote amekuwa mstari wa mbele kuhamasisha vijana kushiriki michezo na ametoa basi kubwa kwa ajili ya mashabikitoka daresslaam kwenda kushangilia na kurudi. Wakati huohuo diwani Karama anategemea kujenga ukumbi mkubwa wangumi hapo chalinze, hivyo ngumi zote za kimataifa zitakuwa zikipigwa hapo.

IBF Wateuwa Majaji na Mwamuzi wa Mpambano wa Cheka na Mashali

$
0
0

Francis Cheka

SHIRIKISHO la Ngumi la Kimataifa (IBF) limeteua refarii na majaji wa pambano la kutetea ubingwa wa Afrika kati ya anayeushikilia ubingwa huo Francis Cheka wa Tanzania na mpinzani wake Thomas Mashali ambaye ni bingwa wa uzito wa Middle ukanda wa Afrika ya Mashariki na Kati (ECAPBA).

Refarii wa mpambano huo wa kukata na shoka atakuwa ni John Shipanuka kutoka nchini Zambia mbaye alilisimamia pambano kati ya Francis Chaka na Mada Maugo mwaka jana kwa ustadi mkubwa. Shipanuka ni Afisa Ugavi katika jeshi la Jamhuri ya Watu wa Zambia na ana ujuzi mkubwa wa kusimamia mapambano ya ngumi ya kimataifa.
 
Aidha, majaji wa mpambano huo ni Daudi Chikwanje kutoka Malawi ambaye ndiye Katibu Mkuu wa Chama Cha Ngumi Cha Malawi na ambaye anakuwa jaji namba moja. Steve Okumu wa Kenya ambaye anakuwa jaji namba mbili na Ismail Sekisambu wa Uganda ambaye anakuwa jaji namba tatu. Msimamizi mkuu wa mpambano huo ni Rais wa IBF katika bara la Afrika, Ghuba ya Uajemi na Mashariki ya Kati Mtanzania Onesmo Ngowi.
 
Hata hivyo Ngowi amemwagiza Mwenyekiti wa Kamati ya Viwango na Ushindi wa Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Nchini (TPBC) Boniface Wambura amshikie nafasi hiyo ili Ngowi apate nafasi nzuri ya kusimamia mapambano matatu (moja la ubingwa wa dunia kwa vijana,, lingine la ubingwa wa mabara kwa wanawake na lingine ubingwa wa Afrika) yatakayofanyika nchini Ghana tarehe 3 mwezi Mei.
 
Nayo Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa nchini TPBC imeshateua maofisa watakaosimamia mapambano ya awali pamoja na kutoa kibali kwa kampuni ya Mumask Investment and Gebby ili iendeshe mpambano huo!
 
Hii ni mara ya pili kwa bondia Francis Cheka kutetea ubingwa wake tangu amsambaratishe kwa TKO bondia machachari Mada Maugo katika mpambano uliofanyika mwaka jana mwezi wa Aprili katika ukumbi wa PTA jijini Dar Es Salaam.

Imetolewa na: SHIRIKISHO LA NGUMI LA KIMATAIFA AFRICA (IBF/AFRICA), DAR ES SALAAM, TANZANIA

Wasanii Chipukizi 300 Kushiriki Maonesho ya Kukuza Vipaji

$
0
0

Ofisa Habari wa SHIWATA, Peter Mwenda

WASANII chipukizi 300 kutoka vikundi 15 jijini Dar es Salaam wamejitokeza kushiriki maonesho ya kukuza vipaji yaliyoandaliwa na Mtandao wa Wasanii Tanzania (SHIWATA) Jumamosi ya Aprili 27 katika ukumbi wa hoteli ya StarLight, Mnazi Mmoja Dar es Salaam.
Vikundi ambavyo vimethibitisha kushiriki pamoja na Kaole Sanaa Group, Splendid, Uyoga Boga na vingine katika fani ya Bongo Flava, Taarab, Maigizo, Ngoma, Mazingaombwe, Sanaa za Ufundi, Kung Fu, Sarakasi, Kusheki, Kwaya, na Ngonjera.
Maonesho kama haya yatafanyika kila mwezi na kiingilio ni bure na vikundi vingine ni Super Shine Morden Taarab, Zijiu, Edeneza Brass Band, Asili Africa, Mege Arts, Kintu, Army Kwanza, Wachapakazi, Tanhope, Tanz Arts, Mshikamano, Big House, Lutenga Boys, Kilimasta, Manuary.
Madhumuni makubwa ya tamasha hilo ni kuibua vipaji vya wasanii chipukizi ili kazi zao ziweze kupata soko hivyo mapromota, Majd, Maproduza wa filamu wasikoke kufika katika maonesho hayo ili kuona mastaa chipukizi ambao ambavyo vipaji vyao bado havijaonekana.

Vijana wa sanaa mbalimbali wanatakiwa kufika katika ofisi za SHIWATA zilizopo Bungoni Ilala ili kujisajili kwa ajili ya maonesho mengine yanayofuata.
Tanzania kuna wasanii wengi wenye vipaji lakini kazi zao hazisikiki wala kuonekana kwenye vyombo vya habari hivyo hiyo ni fursa kutumia maonesho hayo kama soko la kazi zao katika jiji la Dar es Salaam.

Wasanii mbalimbali ambao vipaji vyao vitakubalika sokoni watanufaika kupata ajira ya kuuza kazi zao pamoja na kushiriki katika matamasha mbalimbali ndani na nje ya nchi.

Imeandaliwa na Peter Mwenda, Ofisa Habari wa SHIWATA
0715/0752 222677

Kutoka Uswahilini Hadi Ughaibuni!

$
0
0

Sensei Rumadha

Sensei Rumadha Fundi (Romi) mtaalam wa ngazi za juu wa karate na Yoga

TUNAPOZUNGUMZIA Watanzania waliozaliwa na vipaji na kufanikiwa kuvipigania na kuviendeleza hadi kufikia kiwango cha kimataifa jina la Sensei Rumadha Fundi a.k.a Romi huwezi kulikwepa. Huyu ni Mtanzania mwenye makazi yake nchini Marekani, kabla ya kujikita nchini Marekani alikuwa mmoja wa wanafunzi wa karate pale Zanakaki, jijini Dar es Salaam chini ya mwalimu wake.

Sensei Natambo Guru Kamara Bomani (RIP), baada ya hapo akaenda kwa mafunzo zaidi nchini Japan, Sweden na Denmark, akachaguliwa kwenda nchini India kwa mafunzo ya kuwa mtaalamu wa Yoga, Vipaji hivi vya Karate na Yoga, Sensei Rumadha Fundi anaiwakilisha Tanzania kuwa nchi ya wenye vipaji.

Sensei Rumadha Fundi ni mwalimu wa karate na yoga mwenye utalaamu na upeo wa hali ya juu sana, tena mwenye nidhamu. Sensei Rumadha Fundi (Romi)(3rd Dan black belt), akiwajibika katika semina ya karate Dojo ya Sugarland, Texas USA katika seminar ya walimu wa karate (ma-sensei) wiki iliyopita chini ya uongozi wake Sensei Ramon Veras (7th Dan), wa Traditional Okinawan Goju Ryu Karate-Do.

Sensei Rumadha ni mmoja wa walimu wa Kitanzania wa karate ambao wanafanya vizuri katika fani hii ughaibuni, ni matumaini yetu wahusika katika sekta ya michezo hasa upande wa mapambano kama ngumi, kick boxing, judo nk wataangalia uwezekano wa kupata mchango wao ambao unaweza kusaidia katika kuboresha wanamichezo wetu kufikia kiwango cha kimataifa na kuliletea sifa taifa letu.

Nani Kuwa Bingwa wa Pan – African Guinnes Football Challenge?

$
0
0

Guinnes Football Challenge

MASHINDANO makubwa na mazuri ya GUINNESS® FOOTBALL™ CHALLENGE yamekuwa yakiwasisimua na kuwafurahisha watazamaji wake kwa wiki tano zilizopita.Sasa mashindano ya Pan-African yataanza kuoneshwa katika televisheni za ITV na Clouds TV kuanzia kesho tarehe 24 April, 2013 saa 3:15 ITV na 2:15 Clouds TV.

Sasa timu kutoka Cameroon, Ghana, Uganda, Kenya na Tanzania zitakutana uso kwa uso kushindana ili kujua ni nani ana maarifa zaidi na ujuzi wa kusakata kabumbu, hata kuvishwa ubingwa wa Pan-African.

Washiriki kutoka Afrika yote waliowashinda wapinzani zao ili kuwakilisha nchi zao sasa watakutana na timu bora za Pan-African ambazo zina maarifa na ujuzi zaidi. Katika hatua hii ya robo fainali washiriki wanawania kushinda hadi dola za Kimarekeni 250,000.

Kila timu sasa itacheza kuwakilisha nchi yake na kuonesha uwezo wao katika kusakata kabumbu. Washiriki watahitaji kucheza vizuri kwa kiwango cha juu katika mchezo ili kujipa nafasi ya kushinda mashindano haya na kufanya nchi zao kujivunia. Timu nne zitakazo shiriki katika robo fainali ya kipindi cha kwanza ni:

• Gregory Doamekpor na Kyei Edmond Nana, wenye umri wa miaka 21 kutoka Accra,Ghana. Hawa walikuwa washindi katika sehemu ya kwanza ya GUINNESS FOOTBALL CHALLENGE Ghana. Gregory ni mwanafunzi wa Saikolojia na ndiye kichwa cha timu wakati Kyei ni mwanafunzi wa Mahusiano ya jamii, atakuwa anachezea mpira.
• Timu kutoka Uganda itakuwepo pia, Ibra Kawooya(30) na Alex Muyobo(31),wote mashabiki wa Man.United, Ibra atakuwa kichwa cha timu wakati Alex atacheza uwanjani.
• Kutoka Cameroon watakuwa Emerand Tchouta(24) na Abdul Salam(25). Emerand atakuwa kichwa cha timu na Abdul ataonesha uwezo wa kusakata kabumbu. Japo walifanikiwa kuondoka na dola 1,500 tu lakini walionesha kiwango kizuri hivyo wana nafasi kubwa ya kushinda.
• Timu nyingine kutoka Kenya Francis Ngigi(23) kutoka Nairobi na Kepha Kimani(25) kutoka Thika. Timu hii ilishinda dola 3,000 katika mashindano ya GUINNESS FOOTBALL CHALLENGE. Francis atakuwa kichwa cha timu wakati Kepha ataonesha kipaji chake cha kucheza soka.

Meneja wa kinywaji cha Guinness, Davis Kambi alisema: “Tumeona timu mbalimbali kutoka mataifa mbalimbali zilishindana kufikia hatua ya robo fainali ya Pan-African- GUINNESS FOOTBALL CHALLENGE na sasa tunafurahia kuona timu zetu bora katika hatua za mwisho.

Kila timu imeiwakilisha vizuri nchi yake na wamefanya vizuri katika mashindano haya kwa kujiamini. Sasa timu zote zina nafasi ya kuthibitisha uwezo wao wa kucheza na si kuangalia tu pale watakapo shindana ili kufikia nusu fainali.Tunasubiri kwa hamu na kuzitakia timu zote kila la heri!”

Robo fainali ya kwanza ya Pan-African itaoneshwa katika televisheni za ITV na Clouds TV kwa hiyo hakikisha unaangalia na kuishangilia timu ya taifa lako.
Wapenzi wa kipindi hiki cha Guiness football challenge barani Afrika wanakumbushwa kwamba nao wanaweza kushiriki kwa kufuatilia kwa karibu. Wanaweza kufanya hivyo kwa kujisajili bure kabisa katika tovuti ya m.guinnessvip.com kwa kupitia simu ya mkononi.

Hakikisha kuufwatilia ukurasa wa facebook wa GUINNESS FOOTBALL CHALLENGE kwa habari mbalimbali.
-www.facebook.com/guinnesstanzania

GUINNESS FOOTBALL CHALLENGE, ni kipindi cha mchezo wa soka kinachotayarishwa na kampuni ya kimataifa ya Endemol. Usikose kuangalia na kufuatialia kipindi hiki katika runinga yako kupitia televisheni za ITV na Clouds TV kila siku ya Jumatano usiku. Usisahau kuwa na chupa ya bia uipendayo ya Guiness wakati unaangalia kipindi hiki. Tafadhali kunywa kistaarabu- Hairuhusiwi kuuzwa kwa wale wenye umri chini ya miaka 18.


Bondia ‘Star Boy’ Ajifua Kumkabili Jibaba

$
0
0

Kocha wa mchezo wa masumbwi nchini Habibu Kinyogoli kushoto akimwelekeza jinsi ya kutupa makonde bondia Shabani Mhamila ‘Star Boy’ katika kambi ya Ilala iliyopo Amana CCM jana Sta Boy anajiandaa na mpambano wake na Yusuph Jibaba utakaofanyika siku ya mei mosi katika ukumbi wa PTA Sabasaba Dar es salaam. (Picha na Super d blog)

Na Mwandishi Wetu

BONDIA Shabani Mhamila ‘Star Boy’ anaendelea kujifua kwa ajili ya kumkabili Yusuf Jibaba katika pambano la utangulizi wakati wa mchezo wa kati ya Francis Cheka na Thomas Mashali. Pambono la raundi nne linatarajiwa kufanyika katika Ukumbi wa PTA Sabasaba, Dar es Salaam Mei Mosi mwaka huu, linatarajiwa kuwa la vuta nikuvute kutokana na kila mmoja kujigamba kujiandaa vema.

Kocha wa Star Boy, Habibu Kinyogoli ‘Masta’ akisaidiwa na Rajabu Mhamila ‘Super D’ wamesema kuwa bondia wao anaendelea vizuri na mazoezi kwa ajili ya  kujiandaa kumchakaza Jibaba ili kuendelea kujiwekea sifa nzuri.

“Bondia wangu yuko katika maandalizi ya kutosha kuhakikisha anafanya vizuri katika pambano hilo la utangulizi kati ya Cheka na Mashali” alisema Super D na kuongeza Star Boy alishawai kuwa bingwa wa masumbwi mwaka 1998 ambapo alisimama kwa kipindi kidogo kutokana na maisha ya nchini lakini kwa sasa ameamua kurudi katika ulingo wa masumbwi ili aweze kutoa changamoto za mchezo huo kutokana na mabondia wengi kutokujua sheria na kanunu za mchezo huo.

Star Boy mwenye rekodi ya; won 14 (KO 5) + lost 7 (KO 4) + drawn 2 = 23 ambaye mkanda wa kwanza wa taifa alichukua kwa kumtwanga Theodor Luanda Frebruary 2,1996 na kutetea vema 10 Februari 1997 kwa kumtwanga bondia Chaurembo Palasa wa Super D.

Kocha huyo wa kimataifa wa mchezo wa ngumi nchini, alisema kuwa katika mchezo huo kutakuwa na DVD za mafunzo ya mchezo huo zenye mapambano makubwa ya mabondia wa ndani na nje ya nchi.

Timu Kutoka Afrika Mashariki Yaingia Nusu Fainali Guiness Football Challenge

$
0
0

Watangazaji wa kipindia cha Guiness Football Challenge wakiwa na baadhi ya washiriki

*Washiriki bora kutoka Afrika kuingia robo fainali ya pili kuwania kufuzu nusu fainali

ROBO fainali ya kwanza ya Pan-African GUINNESS® FOOTBALL CHALLENGE™ ilifanyika jana usiku ambapo mashabiki wa Afrika masharik i walikuwa wakishangilia timu za nchi zao. Washiriki mahiri kutoka Cameroon, Ghana, Kenya, Uganda na Tanzania walikutana uso kwa uso ili kushindania dola za kimarekani 250,000 na kutwaa ubigwa wa Pan-African.

Timu ya Afrika mashariki iliyoweza kufuzu kuingia nusu fainali kutoka kipindi cha kwanza ni Francis Ngigi na Kepha Kimani kutoka Kenya. Japokuwa hawakufanikiwa kufikia hatua ya mwisho ya ukuta wa pesa wa GUINNESS lakini walifanikiwa kuingia nusu fainali.

Emerand Tchouta (24) na Abdul Salam (25) kutoka Cameroon walionesha kuwa wao ni wachezaji wazuri ambapo walifanikiwa kufikia hatua ya mwisho ya ukuta wa pesa. Katika hatua ya mwisho, ambapo walifanikiwa kujipatia dola za kimarekani 5,000 kuongezea walizokuwa nazo waliposhinda mwanzoni dola 1,500.

Timu zitahitaji kuwa na umoja na kujiamini ili kuweza kujiandaa kwa hatua zinazofuata. Timu moja kutoka Dar es Salaam Tanzania wataingia uwanjani wiki ijayo itakua na Daniel Msekwa(21) na Mwalimu Akida Hamad(26).

Meneja wa kinywaji cha Guinness, Davis Kambi alisema, “Robo fainali ya GUINNESS FOOTBALL CHALLENGE ilisisimua katika runinga ambapo Francis na Kepha walifanikiwa kuiwakilisha Afrika mashariki katika nusu fainali. Timu kutoka Kenya na Cameroon zimefuzu kuingia nusu fainali, wiki ijayo washiriki wengine watakutana ili kujua ni nani atashinda na kufuzu hatua ya nusu fainali. Nawatakia wote kila la heri”.

Timu nne zitakazo shiriki wiki ijayo kutafuta nafasi ya kuingia nafasi ya nusu fainali ni:

• Watakao kuwa na jezi za bluu ni Daniel Msekwa (21) ambaye ni kichwa cha timu, na mwenzie Mwalimu Akida Hamad (26). Walifanikiwa kujishindia dola za kimarekani 5,500 katika mashindano ya Afrika Mashariki hivyo wana nafasi kubwa ya kufuzu nusu fainali.
• Wenye jezi nyekundu watakuwa wakenya, kocha wa vijana Kenneth Kamau(23) na dereva Wills Ogutu (30) wote kutoka Nairobi. Ingawawa hawakufanya vizuri sana katika sehemu zilizopita lakini wanaweza kufanya vizuri wiki ijayo wakijipanga vizuri.
• Archille Stephanie na Martial Toubou kutoka Douala Cameroon watavaa jezi za kijani. Archille atajibu maswali wakati Martial ataonesha uwezo wake wa kucheza soka. Walifanikiwa kujishindaia dola 4,000 katika sehemu zilizopita.
• Jezi nyeusi watakuwa ni Dennis Nyaku(25) na Francis Nyarko(27) wote kutoka Ho Ghana ambapo walifanikiwa kujishindia dola 1,500 katika mashindano ya kitaifa. Dennis atakuwa kichwa wakati Francis atakuwa akionesha uwezo wake wa kusakata kabumbu na kuweka chini vifaa vya uchoraji.

Wapenzi wa kipindi hiki cha Guiness football challenge barani Afrika wanakumbushwa kwamba nao wanaweza kushiriki kwa kufuatilia kwa karibu. Wanaweza kufanya hivyo kwa kujisajili bure kabisa katika tovuti ya m.guinnessvip.com kwa kupitia simu yako ya mkononi.

Robo fainali ya pili ya Pan-African itaoneshwa katika televisheni za ITV na Clouds TV kila jumatano saa 3:15 ITV na Clouds TV saa 2:15 usiku.

Hakikisha kuufwatilia ukurasa wa facebook wa GUINNESS FOOTBALL CHALLENGE kwa habari mbalimbali-www.facebook.com/guinnesstanzania

GUINNESS FOOTBALL CHALLENGE, ni kipindi cha mchezo wa soka kinachotayarishwa na kampuni ya kimataifa ya Endemol. Usikose kuangalia na kufuatialia kipindi hiki katika runinga yako kupitia televisheni za ITV na Clouds TV kila siku ya Jumatano usiku.

Usisahau kuwa na chupa ya bia uipendayo ya Guiness wakati unaangalia kipindi hiki.

Tafadhali kunywa kistaarabu- Hairuhusiwi kuuzwa kwa wale wenye umri chini ya miaka 18.

Msanii ‘FFU’ Aibiwa Bundi Wake Nyumbani

$
0
0

Mmoja wa bundi kutoka Latin Amerika aliyeibiwa kwa Ras Makunja

Na Mpekuzi wa Habari Ughaibuni

WATU wasio julikana wamefanikiwa kuiba ndege wawili aina ya bundi wanaofugwa nyumbani kwa Kamanda Ras Makunja ambaye ni kuingozi Mkuu wa Ngoma Africa Band. Hata hivyo taarifa zinasema moja ya ndege wake walioibiwa wamepatiaka katika kituo cha hifadhi ya wanyama.
Kamanda Ras Makunja anamlaumu jirani yake kuwa ndiye aliyechonga dili ya kuchukuliwa kwa ndege wake.

Habari za uhakika zimevuja kuwa mkuu wa bendi hisiyo kaukiwa na virungu “Ngoma Africa band” aka FFU kule Ujerumani, kamanda wao Ras Makunja amejikuta akishika kichwa baada ya watu wasio julikana kuingia katika imaya yake kuvunja moja ya matundu yaliokua na ndege aina bundi jirani ya nyumba na kutoweka nao! Inasemekana kamanda na familia yake walikua hawapo nyumbani, na wajanja awakatumia nafasi hiyo.

Kamanda Ras Makunja alishikwa na butwaa baada ya kugundua kuwa kwenye chumba kilichokua na ndege aina bundi mlango uko wazi na ndani hakuna ndege! Baada ya kuenda kurepoti Polisi ikagundulika kuwa bundi hao wawili walichukuliwa na idara ya kuifadhi wanya ya Ujerumani, kwa madai kuwa ndege hao walikua wakubwa mno na chumba chao futi 12X12 hakitoshi.

Kwa kupitia wakili wake mkuu wa kikosi kazi kamanda Ras Makunja ameambiwa bora awaruhusu ndege hao warudishe katika nchi za joto walikotoka. Bundi hao walikua katika imaya ya mwanamuziki huyo kama ndege wa kufuga nyumbani, ambao alipewa na moja wa marafiki zake miaka ya nyuma.

Moja wa majirani wa kamanda Ras makunja ndiye anayetupiwa lawama na kamanda huyo kuwa awapendi ndege hao aina ya bundi, na jirani naye anarudisha lawama kwa kudai labda baadhi ya wanafamilia ya kamamnda ndio waliotengeneza fitina ya kuondolewa kwa bundi hao, kwani walikuwa wanatisha.

Mwanamuziki Makunja anamsaka mbaya wake aliyesabisha kuchukuliwa kwa bundi wake ambao ana kibali cha kuwamiliki katika imaya yake ya Anunnaki Empire. Tunampa pole Kamanda Ras Makunja kwa yaliyomkuta.

IBF/Africa Super Middleweight on the Line as Mashali Attempts to Grab the Crown

$
0
0

Francis Cheka (right) and Uensal Arik (left)


REELING from the recent defeat in the hands of the German strongman Uensal Arik, TEAM Francis Cheka is back on the drawing board as it attempts to defuse negative impact of the loss in their forthcoming rumble against the man of the people and dreadlock Thomas Mashali. The duo is competing for the “IBF Continental Africa Super Middleweight Title” as optional defense for Cheka.

The tournament slated for 1st May, 2013 (May Day) has elicited a lot of excitements from thousands of boxing stakeholders in Tanzania and the whole of East African region. Thomas Mashali is the East & Central African Middleweight Champion and the biggest crowd puller in the region todate.
 
Cheka’s recent defeat was kind of embarrassment as he took the fight as a warm up but alas, things turned bitter as the Germany strongman Uensal Arik sent him reeling to the floor before Thomas Mtua threw out the towel as SOS for the Tanzanian slugger! It was a defeat from “Manna”as this kind of taught Cheka a lesson or two about taking boxing serious as there is nothing as a small fight in boxing.
 
Adam Tanaka of Mumask Investment and Gebby Presure LTD, the man of the hour promoting this fight has been working over drive to have all the details finalized. Of the top priority is the arrival of the ring officials (all coming outside Tanzania) who have been summoned to preside over the rumble. This is so because Adam want to avoid complaints from either boxer should the decision goes against their expectations.
  
The man who has been charged with the responsibility to stand in as “the third man in the ring” is no other than the Zambian Army Officer, John Shipanuka who himself looks like a heavyweight boxer in refereeing uniform. Shipanuka’s body language and impatiality with boxers in the ring has illuminated his CV and make him one of the most sort-out ring officials in Sub Sahara Africa.
 
To assist him would be two Sedentary Generals of; Uganda Professional Boxing Commission (UPBC), master Simon Katogole and Daudi Chikwanje of Malawi Boxing Association (MBA). These two gentlemen would be in the company of one of the most experienced judges in East Africa Alhaj Ismail Sekisambu also from Uganda.

So, “the chickens have finally come home to roost” as any of the two has to face the consequences of his mistakes in the ring on that particular day.
 
So, as the clock ticks to the morning hours of May Day 2013, Dar Es Salaam landscape may turn into a “quicksand” for the two gladiators as fans from all walks of life jams the PTS Social Hall to witness yet another rumble of the year!
 
 Nothing has been left to chances as the World’s premier professional boxing “top dog” the IBF has already given its blessing by sanctioning for the title!
 
 
ISSUED BY, INTERNATIONAL BOXING FEDERATION AFRICA (IBF/AFRICA0
DAR ES SALAAM, TANZANIA

Lady Jay Dee Kuzindua ‘Album’ ya Sita, Atimiza Miaka 13 ya Muziki

$
0
0

Msanii Lady Jay Dee


MSANII maarufu nchini Tanzania, Lady Jay Dee anatarajia kuzinduzi wa album yakie ya sita inayokwenda kwa jina la NOTHING BUT THE TRUTH ambayo ina jumla ya nyimbo 10.
Katika taarifa aliyoitoa kwa vyombo vya habari msaanii huyo mwenye mafanikio lukuki amesema uzinduzi wa album hiyo utakwenda sambamba na sherehe za yeye kutimiza miaka 13 katika tasnia ya muziki.
“…Mwaka huu (2013), natimia miaka 13 tangu nianze kazi ya muziki. Namshukuru Mungu tuko pamoja na pia, nashukuru umma wa Tanzania kwa kuendelea kuni- support (unga mkono) muziki wa Tanzania na kunipa nguvu mimi kama msanii,” alisema Lady JayDee.
“Nashukuru vyombo vyote vya habari vinavyoshiriki kikamilifu kukuza na kulinda sanaa ya Tanzania bila kujali maslahi binafsi. Tumeandaa sherehe kubwa na nzuri ya miaka 13 ya LADY JAYDEE, katika muziki.”
Sherehe ya miaka 13 ya Lady JayDee katika muziki itashirikisha show ya nyimbo zote bora za JayDee kwa kuwashirikisha pia baadhi ya wasanii wa nchini. Sherehe hizo zitafanyika Ijumaa tarehe 31 May 2013.
Nawakaribisha wote tufurahi pamoja, na Mungu awabariki

Bondia Fransis Cheka Amtwanga Thomas Mshali Mei Mosi

$
0
0

Bondia Fransic Cheka Kushoto akimshambulia makonde ya nguvu Thomas Mshali wakati wa mpambano wao uliofanyika katika Sikukuu ya Mei Mosi katika Ukumbi wa PTA Sabasaba Dar es Salaam, Cheka alishinda kwa knockout raundi ya 10.

Bondia Fransic Cheka kushoto akipambani na Thomas Mshali wakati wa mpambano wao uliofanyika katika sikukuu ya Mei Mosi katika ukumbi wa PTA Sabasaba Dar es Salaam.

Shomari Kimbau akiwa na Cheka baada ya kumvisha ubingwa wa IBF Africa aliokuwa akiutetea

Timu za Tanzania na Kenya Zaingia Nusu Fainali Guiness Challenge cup

$
0
0

baadhi ya washiriki katika shindano la Guinness Challenge Cup

Timu kutoka Tanzania na Kenya ziliwakilisha vizuri Afrika mashariki katika sehemu ya saba ya GUINNESS® FOOTBALL CHALLENGE™. Timu ya Kenya ilifanikiwa kuzishinda timu nyingine na kufikia hatua ya mwisho ya ukuta wa pesa wa Guinness. Kenneth kamau na Wills Ogutu wote kutoka Nairobi wamefuzu nusu fainali pamoja na watanzania Daniel Msekwa na Mwalimu Akida Hamad ambao walipata nafasi ya pili jana usiku.

Timu hizi mbili kutoka Kenya na Tanzania sasa zina nafasi ya kuwakilisha Afrika mashariki na kushinda hadi dola za kimarekani 250,000 pamoja na kuvikwa taji la ushindi wa Pan-African, watakapoendelea hatua z juu zaidi. Timu hizi zitahitaji kujiandaa vizuri zaidi na kujiamini ili kufanya vizuri katika hatua ya nusu fainali.

Timu zingine nne zitakutana katika robo fainali ijayo ili kuwania nafasi ya kuingia nusu fainali ya mashindano ya GUINNESS FOOTBALL CHALLENGE.

Usikose kuangalia robo fainali za Pan-African kupitia televisheni za ITV na Clouds TV ambapo timu za Africa Mashariki zinapokutana na timu na timu zingine kutoka Afrika Magharibi huku ukiburudika na kinywaji cha GUINNESS.

Hakikisha kuufwatilia ukurasa wa facebook wa GUINNESS FOOTBALL CHALLENGE kwa habari mbalimbali.
-www.facebook.com/guinnesstanzania

GUINNESS FOOTBALL CHALLENGE, ni kipindi cha mchezo wa soka kinachotayarishwa na kampuni ya kimataifa ya Endemol. Usikose kuangalia na kufuatialia kipindi hiki katika runinga yako kupitia televisheni za ITV na Clouds TV kila siku ya Jumatano usiku.

Tafadhali kunywa kistaarabu – Hairuhusiwi kwa wenye umri chini ya miaka 18


Mazoezi Kumsaka Malkia wa Tanga Yaanza

$
0
0

Mkurugezi wa Kampuni ya DATK Intertaimeint, Asha Kigundula

Na Mwandishi Wetu

MAZOEZI kwa ajili ya kujiandaa na shindano la kumsaka malkia wa Mkoa wa Tanga mwaka huu
“Redd’s Miss Tanga 2013″ yanatarajia kuanza Jumatano Mei 8 kwenye Ukumbi wa Lavida uliopo jijini Tanga.

Akizungumza na mtandao huu Mkurugezi wa Kampuni ya DATK Intertaimeint, Asha Kigundula
Mratibu wa shindano hilo, alisema kuwa maandalizi ya shindano hilo yanaendelea vizuri.

Kigundula alisema kuwa walimu watakaosimamia warembo hao ni Miis Tanga 2012 Teresia Kimolo na Miss Tanga 2011 Zubeda Seif. Alisema kuwa maandalizi yanaendelea vizuri, ambapo
warembo wameanza kuitikia wito wa kushirikishi shindano hilo.

Kigundula alisema kuwa mpaka sasa jumla ya warembo 8 wamejitokeza kushiriki shindano hilo
ambapo nafasi bado iko wazi kwa wasichana wote wenye sifa za kushiriki.

“Kila kitu kinaendelea vizuri, ikiwa na warembo kuendelea kujiandikisha kushiriki shindano la mwaka huu, ambalo nina hakika litakuwa la aina yake,” alisema Kigundula

Alisema kwamba shindano la mwaka huu litaandika historia mpya ya urembo mkoani humo kwa kuwa Kampuni DATK imejipanga, hivyo mashabiki wa mashindano ya urembo wa jijini hapo kwa ujumla wakae mkao wa kupata raha.

Pia alisema fomu zinapatika katika ofisi ya Mwananchi iliyopo Bandari Tanga ghorofa ya Nne, Five Brathers kwa Nassa Makau iliyopo jijini humo, kwa Dar es Salaam zinapatikana katika ofisi za Jambo Leo zilizopo Jengo la Hifadhi Hause Posta.

Warembo wa Redd’s Miss Kibaha Waanza Kujifua

$
0
0

Warembo watakao wania taji la Redd’s Miss Kibaha wakiwa katika pozi wakati wa mazoezi yao yanayoendelea katika ukumbi wa vijana Kinondoni Dar es Salaam.

Mkufunzi wa warembo wa Redd’s Miss Kibaha, Rehema Uzuwiya akizungumza na warembo hao wakati wa mazoezi yao katika ukumbi wa Vijana Kinondoni. (Picha na burudan blog)

Big Day For IBF, Ghana, Nigeria and Africa

$
0
0

Albert Mensah

GHANAIAN fighting machine and BEIJING 2008 Olympiad, Issa Samir becomes the first ever Ghanaian “IBF Youth Champion of the World” after stopping the Georgian handsomely true man Robison Omsarashvili 1 minute 29 seconds in round 3 at the Accra National Sports Stadium last night.

Cheered on by thousands of Ghanaians who thronged the stadium from all walks of life, Samir lured the handsomely Georgian to his much anticipated “killer punches”. He peppered him with his telling jabs while dancing like a butter fly (Muhammad Ali’s style) as thousands of Ghanaians in attendance including several ministers and Nigerian Ambassador to Ghana cheered him throughout the rumble.

Every punch that BEIJING 2008 Olympiad Samir threw was calculated to do damage to the handsomely Georgian and it became obvious that his team had the perfect game plan.  Charming the Georgian with his telling jabs so as to lure him to his WEB, Samir’s fighting speed and power was awesome in that Robison could hardly see his punches coming.

As the Ghanaians kept counting when he was administering his lethal punches tearing the handsomely Georgian, Samir’s huge right drove straight to Robison’s jaw and sent him crashing on the canvas with the sound of the falling tree! It was all over even before referee May Mensah Akakpo of Ghana started counting!

In another epic rumble of the evening, Princess Helen Joseph of Nigeria became the Champion of the “IBF Intercontinental Featherweight Female Title” after humiliating the beautiful Mariana Gulyas from Hungary in the shortest fight in history. As thousands of boxing fans (many from Nigerian community in Ghana and other who arrived by hired busses from Nigeria, including their Ambassadot to Ghana) cheered her, Helen’s brinkmanship of the game proved her rightful Princess role on the mantles of the IBF Intercontinental Featherweight division after stopping te beautful Hungarian 23 seconds in round one.          

AND! The man who is touted as the next Sugar Ray Leonard in the making Albert Mensah proved his prowess in boxing as a professional sport after beating his “arch-rival” and boatful Ben Odamettey. It was really drama as groups from each camp danced and beating their drums as the bout progressed on.

Mensah’s articulated style and strength became obvious as the rumble progressed to Odamattey’s anguish as if he wanted to teach “the Bad Boy on the Block” a lesson or two! The two made the stadium live with drums and dance from their camps but as it is always said in boxing, it was Albert Mensah who had the “last laugh” after becoming the “IBF Continental Africa Jr. Welterweight” champion by TKOed Odametey in round 7. Years from now as they judge his performance, historians would begin at this stage when he assumed his mantles as the “IBF Continental Africa Jr. Welterweight” champion!

Thumb up to both GoldenMike Boxing Promotions Syndicate, Ghana and Nigeria for the excellent rumble. This put the Ghana way ahead of others in the continent as it consolidates its role as the “boxing powerhouse”.

Harrah to IBF as it continue its “top dog” position in boxing as a professional sport. Indeed, African professional boxing has “come of age”.

Linah na Barnaba ‘Kufukuzwa’ THT…!

$
0
0

Msanii Linah katika pozi

Na Andrew Chale

KUELEKEA shoo maalumu ya Miaka 13, ya mwanamuziki nguli wa bongo fleva nchini na kiongozi wa bendi yenye msisimko mkubwa ya ‘Machozi Band’, Judith Wambura ‘Lady Jay Dee’ au Jide’  huenda kwa upande wa wasanii wa Nyumba ya Vipaji ya THT, Linah Sanga na Barnaba  mwaka huu ukawa mchungu kwao kufuatia kuwepo taarifa za kutimuliwa na uongozi wa juu.

Kwa mujibu wa vyanzo kutoka kwa mtu wa karibu wa Linah kilieleza kuwa mpaka sasa msanii huyo hana raha na wala hajui ataanza vipi katika harakati zake za kimuziki hasa kufuatia hivi karibuni kukacha shoo ya nguli Lady Jay Dee kwa shinikizo kutoka kwa wakubwa zake.

Hata hivyo, Linah inadaiwa uongozi wa juu umekaa kikao na hatua iliyofuatia kwenye kikao hicho ni kuwaondoa kabisa kwani huenda wakatia doa wasanii wenzao ndani ya kundi hilo.

“Juzi Linha,haikuwa kawaida yake maana hata alipopigiwa simu na ** kwa ajili ya hatua zingine alionekana kuw na hofu, na wala hakutaka kusikia ushahuri wangu ambao nilikuwa nikimhusia kuwa aachane na mawazo hayo kwani jambo analoliwaza huenda likaisha na hata maamuzi yatakayotoka yatakuwa ni kawaida” kilieleza chanzo kutoka kwa mtu wakaribu wa Lina, amabaye hata hivyo alisema kuwa huenda ukweli wa jambo ukawa hadharani.

Hata hivyo taarifa za ndani za uongozi wa THT zilibainisha kuwa mpango wao wa kuwashughulikia wasanii hao upo pale pale na taratibu zinafuata ilizisilete madhara kwa wasanii waliopo ndani ya THT  na watu wa karibu wanaoiunga THT.

“Wewe nani kakwambia kama tumewaadhibu Lina na Barnaba?, ndio kwanza tunakusikia wewe hizo taarifa,  sisi tunafanya mambo yetu wao waache wafanye yao tukiwa nao sie na tunaouwezo wa kuwatimua ilikulinda hadhi ya THT” Kilieleza chanzo hicho ambacho hata hivyo kutokana na usalama wa jina lake tumelihifadhi. Ambapo namba yake inaishia na**08.

Aidha, katika ‘ku-balance’ huondo kamili wa habari hizi wasanii hao wote walipotafutwa kwenye simu zao za mkononi lakini hawakuweza kuwa hewani kwa muda mrefu.. na hata alipopigiwa mtu wao huyo wa karibu naye alizima simu.

Katika kile kinachoeleza kupamba moto shoo hiyo, na kujaa kwa taarifa mbalimbali juu ya wasanii watakaopamba shoo ya miaka 13, Mei 31 ndani ya Nyumbani Lounge, Tayari tiketi zimeanza kuuzwa maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Saalam.

Shoo hiyo ya kijanja Nyumbani Lounge, patakuwa hapatoshi pale wadau wa burudani na wastaarabu wote watakapojumuika kwa pamoja ku-shoo love kwa Lady Jay Dee  na Machozi Band, huku listi ya mastaa mbalimbali wanatarajia kuudhuria sambamba na ‘surprise’ kutoka kwa mastaa hao ambao kwa sasa wengi wapo kimya wakihofia kutengwa na wazee wa ‘fitina bin Logiki’.

Awali kulikuwapo na taarifa za kuwapo kwa msanii Matonya, ambaye hata hivyo mtandao wa Lady Jay Dee ulitoa hadharani kuwa mwanamuziki huyo ameshachukua ‘advance’ ya shoo hiyo na wazee wa ‘kuingilia logik’ wameshamtisha Matonya ili ajitoe, lakini akiwa ameshatafuna pesa ya watu.

Mtandao huo wa kijamii  blog, ilinukuu kila kitu juu ya Makubaliano baina ya Capt.Gadna G Habashi na Matonya ambapo pia unaweza kuyasoma kupitia (www.ladyjaydee.blogspot.com)

Pia ulitoa kwa mara ya kwanza picha,maelezo muhimu na video ya wanamuziki hao wawili Linah na Barnaba wakiingia mkataba wa shoo hiyo na pia kuhamasisha watu kufika Mei 13..

Rumadha: Kutoka Uswahilini Hadi Ughaibuni

$
0
0

Sensei Rumadha na mkewe Anita pamoja na mdogo wake Rumadha, Kibwana Fundi katika shangwe

Sensei Rumadha Fundi (mstari wa nyuma) akiwa na wataalamu wenzie wa mapafu

SENSEI Rumadha Fundi amefanikiwa kujiongezea taaluma kutoka Usensei wa Karate na Mwalimu wa Yoda na sasa kufikia kuwa mtaalamu wa tiba za binadamu upande wa mapafu! Huyu si mwingine bali ni Mtanzania mtaalamu wa michezo ya Karate na Yoga Sensei Rumadha Fundi (3rd Dan, Black Belt) mwenye maskani yake kule nchini 
Marekani. 

Mai 17, 2013 Sensei Rumadha Fundi akishangiliwa na kupongezwa na ndugu na marafiki waliomshuhudia akipokea shahada ya ‘Associate in Applied Science Cardiopulmonary Respiratory Care’ kutoka Collin College, McKinney, Texas, nchini USA.

Sensei Rumadha anafanikiwa kuongezea CV yake kwa kula nondo ya utaalamu wa tiba za mapafu na moyo. Sensei Rumadha sasa amekuwa mtaalam Respiratory Therapist: Mtaalam wa hewa na gasi ya kupumua, anayetibu mapafu na moyo chini ya maelekezo ya mganga wa mapafu ‘pulmonalogist’. Pia, Respiratory therapist anamajukumu mengi kama kuwatibu wagonjwa wa pumu, COPD, Ephysema, Asthma, TB na majonjwa yote yanayohusu mapafu na moyo.
 
Pia, anauwezo wa kutafsiri damu baada ya kupima hali yamgonjwa kama ana oxygen ya gas inahitaji tiba yeyote. Kwa mengi zaidi  kuhusiana na utaalam wa Respiratory Therapist fuata Link ile ipo mwisho wa “Who is Respiratory Therapist? http://en.wikipedia.org/wiki/Respiratory_therapy

Kumjua zaidi Sensei Rumadha Fundi bofya http://dartalk.com/2013/04/22/sensei-rumadha-fundi-romi-mtaalam-wa-ngazi-za-juu-wa-karate-na-yoga%E2%80%A6/

Viewing all 521 articles
Browse latest View live