Quantcast
Channel: Michezo na Burudani – Tanzania Habari | Jamii | Michezo | Mahusiano | Kazi | Thehabari.com
Viewing all 521 articles
Browse latest View live

TFF Yazinduwa Mpango wa Maendeleo 2013-2016

$
0
0

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Leodger Chilla Tenga

SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limezindua rasmi Mpango wa Maendeleo wa Mpira wa Miguu (Technical Development Plan- TDP) wa 2013-2016 ambao pamoja na mambo mengine unahusisha kutazama upya mfumo wa mashindano na kuunda kanda kwa ajili ya kusimamia maendeleo.

Uzinduzi huo umefanywa leo (Aprili 4 mwaka huu) na Rais wa TFF, Leodegar Tenga katika hafla iliyofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kuhudhuriwa na washirika mbalimbali wakiwemo wachezaji, viongozi wa mpira wa miguu, Serikali, klabu na Wahariri wa Michezo.

Rais Tenga amesema mpango huo unafuatia ule wa 2004-2007, na 2008-2012 ambayo ilitengenezwa kwa msaada wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA). Mpango wa sasa umetengenezwa na TFF kwa kufuata mpango mfano (standard plan) wa FIFA.

Amesema mpango wa sasa ni wa kiufundi zaidi kwa vile umelenga kuendeleza mpira wa miguu, kwani iliyotangulia ilihusisha zaidi kutengeneza muundo wa TFF, kazi ambayo imekamilika kwani sasa shirikisho lina vyombo mbalimbali vya kusimamia mchezo huo.

“Wakati ule tulikuwa na Ligi Kuu tu, lakini tumeongeza mashindano ya aina mbalimbali kama U17, U20, Kombe la Taifa na sasa michuano ya Copa Coca-Cola itakuwa ya U15. Pia tukatengeneza Kanuni za Fedha, kilichomo katika mpango wa sasa ni kujenga mpira. Chombo (TFF) tayari kipo,” amesema.

Rais Tenga amesema TFF imefika hapa kutokana na watu kujitolea ambapo ametaka moyo huo uendelezwe, lakini akasisitiza washirika wote kuwa na mpango huo na kuusoma kwani umetokana na maoni yao ambapo kila mmoja ana kazi ya kufanya katika mpango huo.

“Naomba washirika wote wasome mpango huu. Kama mtu una mawazo zaidi baada ya kusoma, toa maoni yako. Mpango huu si Msahafu, utabadilika kutokana na maoni ya watu. Kama una mawazo zaidi, toa maoni yako kwa lengo la kujenga, isiwe kazi ya kulaumu tu kuwa mpango una upungufu. Mabadiliko yanafanyika kutokana na mawazo mapya,” amesema.

Amesema maendeleo ya mpira wa miguu ni mchakato mrefu, kwa hiyo unahitaji ushiriki wa watu kutokana na ukweli kuwa uongozi wa mpira wa miguu Tanzania bado ni wa kujitolea. Rais Tenga amesema ahadi ya TFF ni kushirikiana na washirika mbalimbali kuhakikisha kuna maendeleo kwa faida ya mpira wa miguu wenyewe na nchi kwa ujumla.

Amewashukuru wote waliotoa maoni kwa ajili ya mpango huo wenye kurasa 76. Mpango huo ulioandaliwa na Mkufunzi wa FIFA, Henry Tandau, Mkurugenzi wa Ufundi wa TFF, Sunday Kayuni na Ofisa Maendeleo wa TFF, Salum Madadi unapatikana kwenye CD na nakala laini (soft copy).


‘FFU’ wa Ngoma Africa Band Watoka Kambini

$
0
0

Kamanda Ras Makunja aka Field-Marshal(FFU), wa Ngoma Africa Band aka FFU,
katika gwanda za gwaride!

FFU wakiwa na ‘mitutu’ yao

INASEMEKANA kikosi kazi cha Ngoma Africa Band a.k.a FFU ughaibuni, a.k.a wazee wa bongo tambarare ukipenda “Watoto wa Mbwa” chini ya Kamanda Ras Makunja ‘Field-Marshal/King of Anunnaki Empire (pichani)’, wameshatoka kambini na wapo tayari kwa gwaride la mashambulizi.
Kundi hilo linalotamba kwenye majukwaa ya kimataifa, pia inasemekana Kamanda wao amepandishwa cheo kama anavyoonekana pichani sasa katika gwanda! Katika kambi yao FFU Camp at www.ngoma-africa.com pia kumepigwa soup soup na virungu vya muziki kama kazi vinasikika at www.ngoma-africa.com

Ziara ya Rais wa IBF Katika Bara la Afrika

$
0
0

Ngowi akiwa amesimama na Mkurugenzi wa Masoko wa Shirika la Almasi la Botswana DEBTSWANA Bi. Lesedi Rakola katika mkutano huo.


ZIARA ya Rais wa IBF katika bara la Afrika, Ghuba ya Uajemi na Mashariki ya Kati Mtanzania Onesmo Ngowi, imeiweka nchi ya Botswana mahali pazuri kwa kuiingiza kwenye kundi la nchi nane (8) za Afrika zitakazofaidika na programu ya “IBF ya Utalii wa Michezo”.

Akiongea kwenye mkutano wa waandishi wa habari pamoja na wadau wa michezo alipokuwa anahitimisha ziara yake iliyomchukua kwenye majiji ya Francistown na Gaborone, Rais Ngowi aliweka bayana furaha yake kwa jinsi serikali ya Botswana kupitia Baraza la Michezo la Taifa (BNSC) ilivyompa mapokezi mazuri.

Ngowi aliitembelea Botswana kuanzia Machi 31 hadi Aprili 5 ambapo aliweza kutembelea majiji mawili ya Francistown na Gaborone. Aidha, Ngowi aliitembelea pia miji midogo ya Molopolole,Kanye, Kang, Jwaneng na Ghanzi. Katika miji midogo ya Ghanzi na Kanye Ngowi alijionea jinsi Botswana inavyotunza na kuendeleza vivutio vya kitalii na hivyo kuweza kujipatia pesa nyingi za kigeni kutoka kwa watalii wanaotembelea nchi hiyo!

Programu ya “IBF ya Utalii wa Michezo” itaifanya Botswana kufaidika na ujio wa watalii kutoka nchi zaidi ya 144 ambazo ni wanachama wa IBF. Pia kutakuwa na wawekezaji watakaowekeza kwenye vivutio mbalimbali na kuifanya Botswana kuwa moja ya nchi zinazofaidika na “Utalii wa Michezo”(Sports Tourism).

Rais Ngowi aliishauri serikali ya Botswana umuhimu wa kuwekeza kwenye sekta ya michezo hususan mchezo wa ngumi na kutoa mfano wa namna nchi zinavyotumia mabilioni ya dola za Kimarekani kuandaa michezo ya kimataifa kama vile michezo ya Olimpiki na Kombe la Dunia.

Katika hotuba yake rasmi (Key Note Speech) aliyoitoa kwenye ukumbi wa Chama Cha Mpira wa Miguu cha Botswana (BFA), Ngowi alieleza jinsi bondia mmoja anavyoweza kuitangaza nchi kwa kiasi kikubwa na kumtolea mfano bondia wa Botswana Lesley Sekotswe ambaye aliiwakilisha nchi vizuri alipopambana na bondia Immanuel Naidjala wa Namibia hivi karibuni.

Nalo Barala la Michezo la Botswana BNSC limemhakikishia Ngowi kuwa litafanya kila liwezalo kuuendeleza mchezo wa ngumi ambao ndio unaoitangaza vyema Botswana kwenye medani ya kimataifa. Mwenyekiti wa BNSC bwana Solly Reikeletseng pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa BNSC bwana Perscy Raditladi walitoa ahadi ya kushirikiana na IBF katika kuuendeleza mchezo wa ngumi kwa kiwango ha kimataifa.

Ngowi alimaliza ziara yake nchini Botswana jana siku ya Ijumaa na kuelekea nchini Afrika ya Kusini ambako atakuwa na ziara ya siku nne itakayoisha tareeh 9 April. Akiwa nchini Afrika ya Kusini Ngowi atafanya mazungumzo ya serikali ya nchi hiyo hususan serikali ya jimbo la Mpumalanga ambalo limekuwa likidhamini mapambano mengi ya ngumi.

Mwishini mwa April Ngowi atafanya ziara nyingine katika nchi za Ghana, Cameroon, Misri na Tunisia kujenga uwezo wan chi hizo katika kuitumia programu ya “IBF ya Utalii wa Michezo” (IBF Sports Tourism)

Nani Kuibuka Mshindi Jumatano Hii Guinness Football Challenge

$
0
0

Timu nne zitakazochuana katika kipindi cha nne cha Guinness Football Challenge wiki hii. Kuanzia kushoto ni timu kutoka Kenya (wamevaa nyekundu), Tanzania (bluu), Uganda (kijani na nyeusi).

JUMATANO iliyopita kupitia televisheni za ITV na Clouds TV, mashindano ya GUINNESS® FOOTBALL CHALLENGE™ yaliendelea huku kila timu ikionesha ni jinsi gani utulivu unavyosaidia katika mashindano hayo. Timu ya Kenya ilifanikiwa kuzitoa timu nyingine za Tanzania, Uganda na timu nyingine kutoka Kenya.

Kenneth Kamau na Wills Ogutu walishinda katika mikwaju ya penati na kufikia hatua ya mwisho katika ukuta wa pesa wa Guinness ambapo walifanikiwa kulenga matundu manne na kupata fedha za kimarekani dola 5,500. Kwa bahati mbaya walishindwa kulenga tundu la mwisho na hivyo kupelekea kupoteza dola 2,500 na kuondoka na fedha za kimarekani taslimu dola 3,000.

Kenneth na Wills wana nafasi ya kuiwakilisha nchi yao katika mashindano yajayo ya Pan-African ambapo wanaweza kubahatika kujinyakulia kitita cha fedha za kimarekani hadi kufikia dola 250,000. Katika kipindi kijacho cha mashindano haya kinachorushwa na vituo vya televisheni vya ITV na Clouds TV, timu nne mpya zitaingia uwanjani kupambana vikali ili kujua ni nani ataibuka mshindi na kutambulika kama wachezaji na si tu mashabiki,watatakiwa kushinda na kuziwakilisha nchi zao katika mashindano ya Pan-African.

GUINNESS FOOTBALL CHALLENGE, ni kipindi cha runinga kinachotayarishwa na kampuni ya kimataifa ya Endemol. Kipindi hiki kinarushwa kila Jumatano katika televisheni za ITV na clouds TV. Kipindi kitaruhswa na kituo cha ITV kuanzia saa tatu na dakika kumi na tano(3:15) usiku ambapo Clouds TV itarusha kipindi hicho saa mbili na dakika kumi na tano(2:15) usiku .

Katika Episodi ya nne ya mashindano haya yatakayooneshwa na vituo vya televisheni vya ITV na Clouds TV, timu nne ndizo zitakua uwanjani kuchuana vikali, ni timu ipi itakayowapiga chini wengine na kuingia katika hatua ya Pan Africa? Majibu yote yatapatikana Jumatano hii.

Hizi ndizo timu zitakazochuana vikali katika kipindi cha nne wiki hii cha GUINNESS® FOOTBALL CHALLENGE kinachorushwa na televisheni za ITV na Clouds TV.

Timu ya blu-Tanzania:
• Lukwesa Kanakamfunu (18) na Hamza Ziada (20), wote kutoka Dar-es-Salaam wanaojivunia kuwa marafiki japokuwa wanashabikia timu mbili adui yaani Arsenal na Manchester United. Lukwesa ni mwanafunzi na ndiye kichwa cha timu wakati Hamza ndiye atakayekua akionesha uwezo wa kuchezea mpira.

Timu nyekunndu:
• Ephatus Nyambura (24) na Samuel Papa (23) wote kutoka Nairobi watashiriki kuona kama wanaweza kuwa timu ya tatu ya Kenya kupata nafasi ya kufuzu mashindano ya Pan Africa. Empantus meneja wa ujenzi na ndiye kichwa cha timu wakati Samuel ambaye ni mchezaji wa Nakuru Allstars FC ataonesha uwezo wake wa kucheza mpira.

Timu ya kijani-Uganda:
• Andrew Mpanga (30) na Gadafi Mohammed Anguzu (18) wote kutoka Kampala, Andrew ni mshabiki wa Man. Utd wakati Gadafi ni mshabiki wa Man. City. Andrew ni daktari wa meno ambaye atakuwa kichwa cha timu. Gadafi ni mchezaji mpira hivyo ataonesha uchezaji wake.

Timu nyeusi-Uganda:
• Badi Arorwa (25) na Dennis Bogere (30)kutoka Kampala watawakilisha Uganda katika kipindi kijacho cha mashindano. Badii atajibu maswali akiwa kama kichwa cha timu na Dennis ambaye atakayekuwa akichezea mpira kuonesha kipaji chake.

Wapenzi wa kipindi hiki cha Guinness Football Challenge barani Afrika wanakumbushwa kwamba, wanaweza kushiriki kwa kufuatilia kwa karibu. Wanaweza kufanya hivyo kwa kujisajili bure kabisa katika tovuti ya m.guinnessvip.com.

Pia GUINNESS FOOTBALL CHALLENGE ina kurasa ya Facebook ambayo ni www.facebook.com/guinnesskenya, Ili kufuatilia kwa karibu yanayojiri, unatakiwa kufuatilia ukurasa huu ‘like’ na utakuwa unapata habari zote zinazohusu mchezo huu.

GUINNESS FOOTBALL CHALLENGE, ni kipindi cha mchezo wa soka kinachotayarishwa na kampuni ya kimataifa ya Endemol. Usikose kuangalia na kufuatialia kipindi hiki katika runinga yako kupitia televisheni za ITV na Clouds TV kila siku ya Jumatano usiku. Usisahau kuwa na chupa ya bia uipendayo ya Guiness wakati unaangalia kipindi hiki.

*Haiuzwi kwa walio na Umri chini ya miaka kumi na nane. Tafadhali Kunywa kistarabu.

Kambi ya Masumbwi Yahamia Chalinze

$
0
0

Refarii Ibrahimu Kamwe akimnyoosha mkono juu Amour Mzungu kuwa mshindi wa mpambano huo wa kirafiki dhidi ya Josefu Marwa


DIWANI wa Kata ya Bwilingu Chalinze Bagamoyo,Ahmed Karama Nassar amesema yupo tayali kushirikiana na wadau mbalimbali ili kufanikisha ujenzi wa Ukumbi maalumu wa mchezo wa masumbwi Chalinze. Nassar aliyasema hayo mwishoni mwa wiki katika mapambano ya ngumi yaliyopigwa katika ukumbi wa CCM Mwijuma Mwananyamala.

“Natarajia kufikisha mbali mchezo huu kwa kuwa mmenishawishi kuupenda mchezo wa masumbwi mchezo unaopendwa na wengi na kukimbiwa na wadhamini wachache ata hivyo nimeandaa mpambano rasmi utakaochezwa Chalinze kwa ajili ya kuhamasisha mchezo huu siku ya Aprili 21 hivyo nawaomba wadau wote wa ngumi tuamie chalinze kwa mda hili tuweze kuhamasha mchezo huu.

Ambapo siku hiyo kutakuwa na ushindani mkubwa wa mabondia kutoka Dar es Salaam watacheza na mabondia wa Chalinze siku hiyo ata hivyo kwa kuonesha kwamba anajili na anathamini mchezo wa masumbwi ame aidi kutoa gari moja kwa ajili ya mashabiki na mabondia kwenda kushiriki mchezo uho wa Aprili 21.

Mbali na ahadi hiyo Diwani huyo ametoa pesa taslimu shilingi 150,000 kwa ajili ya malipo ya baadhi ya mabondia waliokuwa hawajilipwa na kuanza kudai kabla ya kupanda ulingoni na kuhamua kuchukua jukumu hilo la kuwalipa mabondia hao.

Mmoja ya wadau wa mchezo wa masumbwi nchini Ibrahimu Kamwe amesema kuwa yupo tayali kutoa ushilikiano wa hali na mali kwa kuanzia atachukua baahi ya vijana kwa ajili ya kwenda kucheza mchezo wa masumbwi uliopangwa siku hiyo hivyo tupo pamoja unajua ngumi watu wanapenda kuangalia ili galama zake ni kubwa ata hivyo naona ajabu wadhamini kushindwa kujitokeza kudhamini mchezo huu unaopendwa na vijana wengi na kuwataka wadau wengine kuiga mfano wa Ahmed Karama Nassar kwa kuanza kuunga mkono mchezo wa masumbwi.

SuperSport Afrika Kurusha Mechi Sita Ligi Kuu Tanzania

$
0
0

Super Sport logo

KITUO cha televisheni cha SuperSport cha Afrika Kusini kitaonesha moja kwa moja mechi sita za Ligi Kuu ya Vodacom katika Super Week kati ya Aprili 11 na Mei 18 mwaka huu. Mechi hizo ni kati Azam na African Lyon itakayochezwa Aprili 11 mwaka huu badala ya Aprili 10 mwaka huu kwenye Uwanja wa Azam Complex ulioko Chamazi, Dar es Salaam. Yanga na Oljoro JKT ambayo sasa itachezwa Aprili 13 mwaka huu badala ya Aprili 10 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Azam na Simba itakayochezwa Aprili 14 mwaka huu badala ya Aprili 13 mwaka huu Uwanja wa Taifa, na mechi kati ya Coastal Union na JKT Ruvu itakayochezwa Aprili 16 mwaka huu badala ya Aprili 10 mwaka huu.

Mechi nyingine ya Super Week itakayochezwa Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga ni kati ya Mgambo Shooting na Yanga itakayofanyika Aprili 17 mwaka huu badala ya Aprili 13 mwaka huu. Pia mechi nyingine itakayooneshwa live na SuperSport ni kati ya Yanga na Simba itakayofanyika Mei 18 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Kutokana na mechi za Super Week, mechi kati ya Mtibwa Sugar na Oljoro JKT iliyokuwa ichezwe Aprili 13 mwaka huu sasa itachezwa Aprili 17 mwaka huu Uwanja wa Manungu, Turiani mkoani Morogoro.

TFF YATAKA MAELEZO YA MCHEZAJI KUHUSU RUSHWA

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limemtaka mshambuliaji Nsa Job wa Coastal Union kuwasilisha maelezo yake juu ya madai kuwa alipewa rushwa ya sh. milioni mbili ili asiifunge moja ya timu vigogo vya soka nchini.

Job alikaririwa Aprili 3 mwaka huu na kituo cha redio cha Clouds FM katika kipindi cha Amplifier kuwa alipewa kiasi hicho cha fedha na kiongozi wa timu husika ili asiifunge katika mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom, lakini alipokea fedha hizo na kuifunga timu hiyo.

Baadaye kiongozi huyo alikuwa akimtaka arejeshe fedha hizo. Pia TFF imekiandikia kituo hicho cha redio kutaka nakala ya kipindi hicho ili pamoja na maelezo ya mshambuliaji huyo vipelekwe katika Kamati ya Nidhamu kwa ajili ya hatua za kinidhamu.

TFF itachukua hatua kali dhidi ya Job iwapo hatawasilisha maelezo yake kuhusiana na suala hilo, na imetaka wadau kutoa ushirikiano ili iweze kupambana kikamilifu na vitendo vya rushwa kwenye mpira wa miguu.

TFF Yazipongeza Ashanti United, Mbeya City na Rhino Rangers Kuingia Ligi Kuu

$
0
0

TFF Yazipongeza Ashanti United, Mbeya City na Rhino Rangers Kuingia Ligi Kuu

KAMATI ya Ligi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imezipongeza timu za Ashanti United ya Dar es Salaam, Mbeya City ya Mbeya na Rhino Rangers ya Tabora kwa kupanda Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) msimu ujao (2013/20114).

Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Wallace Karia amezitaka timu hizo kufanya maandalizi ya kutosha ili ziweze kushindana katika VPL ikiwemo kutimiza masharti ya kuwa klabu za Ligi Kuu. Moja ya masharti ya klabu zenye hadhi ya Ligi Kuu ni kuwa na timu ya pili (U20) ambayo itakuwa na inacheza mechi za utangulizi kwenye uwanja wa nyumbani kila timu ya wakubwa inapocheza.

Mbali ya kuthibitisha timu hizo tatu kupanda daraja, pia Kamati ya Ligi imethibitisha rasmi timu tatu zilizoshuka daraja kurudi Ligi ya Mkoa katika mkoa husika. Timu zilizoshuka kutoka Daraja la Kwanza (FDL) ni Small Kids ya Rukwa kutoka kundi A. Kundi B timu iliyoshuka ni Moro United ya Dar es Salaam wakati Morani FC ya Manyara yenyewe imeporomoka kutoka kundi C.

POLISI KUJIULIZA KWA RUVU SHOOTING VPL

Polisi Morogoro inapambana na Ruvu Shooting katika moja kati ya mechi tatu za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) zitakazochezwa kesho (Aprili 10 mwaka huu). Matokeo ya mechi hiyo yanatarajia kutoa mwanga kama Polisi inaweza kubaki kwenye ligi hiyo msimu ujao.

Timu hiyo itakuwa nyumbani Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro katika mechi hiyo itakayochezeshwa na Ibrahim Kidiwa kutoka Tanga akisaidiwa na Godfrey Kihwili na Ephrony Ndissa wa Arusha. Polisi Morogoro inayonolewa na Adolf Rishard inakamata nafasi ya mwisho ikiwa na pointi 18 tu na imebakiza mechi tatu dhidi ya Simba, Kagera Sugar na Coastal Union.

Mechi nyingine za kesho ni kati ya Tanzania Prisons iliyo nafasi ya 12 ikiwa na pointi 20 dhidi ya Mgambo Shooting. Mwamuzi Hashim Abdallah wa Dar es Salaam ndiye atakayechezesha mechi hiyo kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya. Mgambo ina pointi 24 na iko katika nafasi ya tisa.

Mwamuzi Said Ndege wa Dar es Salaam atachezesha mechi kati ya wenyeji Mtibwa Sugar na Toto Africans itakayofanyika Uwanja wa Manungu ulioko Turiani mkoani Morogoro. Toto Africans ya Kocha John Tegete ina pointi 21 ikiwa nafasi ya 11 wakati Mtibwa Sugar iko nafasi ya tano na pointi zake 32.

Ligi hiyo itaendelea keshokutwa (Aprili 11 mwaka huu) kwa mechi moja kati ya Azam na African Lyon itakayofanyika Uwanja wa Azam Complex.

TFF Yaiadhibu Yanga na Kocha wa Toto Africans

$
0
0

Rais wa TFF, Leodger TENGA

KLABU ya Yanga na Kocha Msaidizi wa timu ya Toto Africans, Athuman Bilali wamepigwa faini ya sh. 500,000 kila mmoja kutokana na makosa mbalimbali katika mechi za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) inayoendelea nchini.

Adhabu hizo zimetolewa na Kamati ya Ligi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) iliyokutana Jumapili (Aprili 7 mwaka huu) jijini Dar es Salaam kupitia ripoti za waamuzi na makamishna kwa michezo namba 108 hadi 171.

Yanga imepigwa faini hiyo baada ya kupata kadi tano za njano katika mechi dhidi ya Kagera Sugar iliyochezwa Februari 7 mwaka huu. Vilevile Kagera Sugar imepigwa faini ya sh. 100,000 kwa kuchelewa kufika kwenye kikao cha maandalizi ya mechi (pre match meeting) dhidi ya African Lyon iliyochezwa mjini Bukoba, Februari 23 mwaka huu.

Naye Kocha Bilali amepigwa faini hiyo na kufungiwa mechi tatu za ligi hiyo kwa kumshambulia kwa maneno kocha wa timu pinzani, hali iliyosababisha mwamuzi amtoe kwenye benchi la wachezaji. Alifanya tukio hilo kwenye mechi kati ya Toto Africans na Tanzania Prisons iliyochezwa Aprili 3 mwaka huu jijini Mwanza.

African Lyon na Simba zimepigwa faini ya sh. 500,000 kila moja kwa kushindwa kuchezesha timu zao za U20 kwenye mechi za utangulizi wakati zilipocheza na Oljoro JKT na Coastal Union, Machi mwaka huu kwenye viwanja vya Azam Complex na Uwanja wa Taifa.

Suala la Meneja wa Coastal Union, Akida Manchai kumshambulia kwa maneno yasiyo ya kiungwana Makamu Mwenyekiti wake Steven Mnguto baada ya kwenye mechi kati ya African Lyon na Coastal Union iliyochezwa Machi 30 mwaka huu Uwanja wa Azam Complex limepelekwa Kamati ya Nidhamu kwa ajili ya hatua za kinidhamu.

Adhabu zote zimetolewa kwa mujibu wa Kanuni za Ligi Kuu ya Vodacom.


Guinness Football Challenge; Kenya Wazidi Kufanya Vema

$
0
0

Washindi wa kipindi cha Nne cha Guinness Football Challenge, Enphatus
Nyambura(kushoto) na Samuel Papana (kulia) katika picha ya pamoja na
watangazaji wa kipindi hicho Larry Asego and Flavia Tumsiime jana baada
ya ushindi.

 Aprili 10, 2013, Dar es Salaam;  Katika sehemu ya nne jana usiku kupitia
televisheni za ITV na Clouds TV, mashindano ya GUINNESS® FOOTBALL CHALLENGE™  yalikuwa na ushindani mkubwa  lakini washiriki kutoka Kenya Enphatus
Nyambura na Samuel Papa waliweza kumudu vishindo na kufanikiwa kuwa timu ya
tatu kutoka Kenya kuingia katika hatua ya Pan- Africa. Katika kipindi hiki cha
nne washiriki walijitahidi kufanya vizuri katika kuonesha uwezo wao wa kuchezea
mpira na kujipatia alama nyingi japo walishindwa kujibu maswali kwa
ufasaha.Washiriki kutoka Kenya walifanikiwa kufika katika hatua ya mwisho ya
kulenga  ukuta  wa pesa wa Guinness ambapo walijishindia fedha
za kimarekani dola 1,500.
Enphatus na Samwel wana
nafasi ya kuiwakilisha nchi yao katika mashindano yajayo ya Pan-African ambapo
wanaweza kubahatika kujinyakulia  kitita
cha fedha  za kimarekani hadi kufikia
dola  250,000. Katika
sehemu ya tano ya mashindano
haya, yanayorushwa na vituo vya Televisheni vya ITV na Clouds TV  timu nne mpya zitaingia
uwanjani kupambana vikali ili kujua ni nani ataibuka mshindi na kuendelea na mashindano hata kuingia hatua
ya Pan-African. Je timu nyingine ya Kenya inaweza kushinda?
GUINNESS FOOTBALL
CHALLENGE, ni kipindi cha runinga kinachotayarishwa na kampuni ya kimataifa ya
Endemol.  Kipindi hiki kinarushwa kila
Jumatano katika televisheni za ITV na clouds TV.  Kipindi kitaruhswa na kituo cha ITV kuanzia
saa tatu na dakika kumi na tano(3:15) usiku
ambapo  Clouds TV itarusha kipindi
hicho saa mbili na dakika kumi na tano(2:15) usiku .
Tafadhali kunywa
kistaarabu – Hairuhusiwi kwa wenye umri chini ya miaka 18.

King Kapita Atoa Video ya ‘Kunatatizo Kwani’

$
0
0

Msanii KingKapita



MSANII
King Kapita amebainisha kuwa tayari ametoa video ya nyimbo yake mpya inayojulikana kwa jina la “KUNATATIZO KWANI”. Nyimbo hiyo ambayo aliifanya na msanii GODZILLA kutoka ya DEFATALITY (MESSEN SELEKTA) kwa sasa inapatikana katika mtandao wa Youtube kwa link ya; http://youtu.be/NaJDR38AKE4

King Kapita ana nyimbo kama:
1.MTOTO MLITO
2.MTOTO WA FISADI
3.SHIKAMOO PESA

LINK YA HULKSHARE HII HAPA http://www.hulkshare.com/n8iouqb6fbi8 KWA AJILI YA KUSIKILIZA NA KU DOWNLOAD

Mazoezi ya Mabondia Kambi ya Ilala Kuelekea Mpambano wa Mei Mosi

$
0
0

Bondia Ibrahimu Class ‘King Class Mawe’ kulia akioneshana uwezo wa kutupiana makonde na Ally Masaga wakati wa mazoezi yaliyofanyika katika kambi ya Ilala Amana CCM Dar es Salaam Class anajiandaa na mpambano wake wa Mei Mosi dhidi ya Amos Mwamakula utakaopigwa katika ukumbi wa PTA Saba saba.

Bondia Ibrahimu Class ‘King Class Mawe’ kulia akioneshana uwezo wa kutupiana makonde naIbrahimu Toll wakati wa mazoezi yaliyofanyika katika kambi ya Ilala Amana CCM Dar es Salaam Class anajiandaa na mpambano wake wa Mei Mosi na Amos Mwamakula utakaopigwa katika ukumbi wa PTA Saba saba.

Bondia Ibrahimu Class ‘King Class Mawe’ kulia akioneshana uwezo wa kutupiana makonde na Kasimu Gamboo wakati wa mazoezi yaliyofanyika katika kambi ya Ilala Amana CCM Dar es Salaam Class anajiandaa na mpambano wake wa mei mosi na Amos Mwamakula utakaopigwa katika ukumbi wa PTA Sabasaba (Picha na Super ‘D’ Blog)

SuperSport Yashindwa Kurusha Mechi 5 za Ligi Kuu

$
0
0

Super Sport logo

MECHI tano kati ya sita za Super Week za Ligi Kuu ya Vodacom zilizokuwa zioneshwe moja kwa moja (live) na Kituo cha televisheni cha SuperSport cha Afrika Kusini sasa hazitaoneshwa kutokana na matatizo ya kiufundi.

Kwa mujibu wa Mtayarishaji Mtendaji (Executive Producer) wa SuperSport Kanda ya Afrika, Max Tshunungwa ambaye yuko nchini, wameshindwa kuonesha mechi hizo kutokana na matatizo ya kiufundi katika magari yao ya kurushia matangazo (OB van) yanayohudumia Afrika Mashariki- Kenya, Tanzania na Uganda.

Mechi hizo ni kati ya Azam na African Lyon, Yanga na Oljoro JKT, Azam na Simba, Coastal Union na JKT Ruvu na Mgambo Shooting na Yanga itakayochezwa Aprili 17 mwaka huu jijini Tanga.

Tatizo hilo pia limeathiri mechi za Ligi Kuu ya Kenya (KPL) ambazo hazitaonekana wikiendi hii. SuperSport ndiyo yenye haki za matangazo ya televisheni kwa ligi hiyo ya Kenya.

Tshunungwa amekutana na Sekretarieti ya TFF na Kamati ya Ligi kuelezea tatizo hilo. SuperSport kwa kushirikiana na Kamati ya Ligi na TFF watapanga mechi nyingine za Super Week kabla ya ligi kumalizika msimu huu.

Pia TFF, Kamati ya Ligi na SuperSport watakuwa na mkutano mfupi wa waandishi wa habari wakati wa mapumziko kwenye mechi ya leo kati ya Yanga na Oljoro JKT kwenye Uwanja wa Taifa.

Wakenya Wazidi Kung’ara Guinness Football Challenge

$
0
0

Baadhi ya washiriki wa mashindano ya Guinness Football Challenge, wakiwa katika picha ya pamoja na mastaa wa mchezo wa mpira wa miguu na mabalozi wa Guinness Football Challenge.

APRILI 10, 2013, Dar es Salaam; Katika sehemu ya nne jana usiku kupitia televisheni za ITV na Clouds TV, mashindano ya GUINNESS® FOOTBALL CHALLENGE™ yalikuwa na ushindani mkubwa lakini washiriki kutoka Kenya Enphatus Nyambura na Samuel Papa waliweza kumudu vishindo na kufanikiwa kuwa timu ya tatu kutoka Kenya kuingia katika hatua ya Pan- Africa. Katika kipindi hiki cha nne washiriki walijitahidi kufanya vizuri katika kuonesha uwezo wao wa kuchezea mpira na kujipatia alama nyingi japo walishindwa kujibu maswali kwa ufasaha.Washiriki kutoka Kenya walifanikiwa kufika katika hatua ya mwisho ya kulenga ukuta wa pesa wa Guinness ambapo walijishindia dola kimarekani 1,500.

Enphatus na Samwel wana nafasi ya kuiwakilisha nchi yao katika mashindano yajayo ya Pan-African ambapo wanaweza kubahatika kujinyakulia kitita cha fedha za kimarekani hadi kufikia dola 250,000. Katika sehemu ya tano ya mashindano haya, yanayorushwa na vituo vya Televisheni vya ITV na Clouds TV timu nne mpya zitaingia uwanjani kupambana vikali ili kujua ni nani ataibuka mshindi na kuendelea na mashindano hata kuingia hatua ya Pan-African. Je timu nyingine ya Kenya inaweza kushinda?

GUINNESS FOOTBALL CHALLENGE, ni kipindi cha runinga kinachotayarishwa na kampuni ya kimataifa ya Endemol. Kipindi hiki kinarushwa kila Jumatano katika televisheni za ITV na clouds TV. Kipindi kitaruhswa na kituo cha ITV kuanzia saa tatu na dakika kumi na tano(3:15) usiku ambapo Clouds TV itarusha kipindi hicho saa mbili na dakika kumi na tano(2:15) usiku. Tafadhali kunywa kistaarabu – Hairuhusiwi kwa wenye umri chini ya miaka 18.

Timu Nne Mpya Kuingia Hatua ya Mwisho Mashindano ya Guinness Football Challenge

$
0
0

Timu nne zitakazochuana katika kipindi cha tano cha Guinness Football Challenge wiki hii. Kutoka kushoto ni timu kutoka Kenya(wamevaa nyekundu), Tanzania – bluu, Uganda- kijani na nyeusi.

JUMATANO iliyopita katika sehemu ya nne kupitia televisheni za ITV na Clouds TV, mashindano ya GUINNESS® FOOTBALL CHALLENGE™ yalikuwa na ushindani mkubwa lakini washiriki kutoka Kenya Enphatus Nyambura na Samuel Papa waliweza kumudu vishindo na kufanikiwa kuwa timu ya tatu kutoka Kenya kuingia katika hatua ya Pan- Africa, baada ya kuwapiga chini timu za Tanzania na Uganda.

Katika kipindi hiki cha nne washiriki walijitahidi kufanya vizuri katika kuonesha uwezo wao wa kuchezea mpira na kujipatia alama nyingi japo walishindwa kujibu maswali kwa ufasaha. Washiriki kutoka Kenya walifanikiwa kufika katika hatua ya mwisho ya kulenga ukuta wa pesa wa Guinness ambapo walijishindia dola kimarekani 1,500.
Enphatus na Samwel wana nafasi ya kuiwakilisha nchi yao katika mashindano yajayo ya Pan-African ambapo wanaweza kubahatika kujinyakulia kitita cha fedha za kimarekani hadi kufikia dola 250,000. Washiriki bora watakwenda kukutana uso kwa uso na mashabiki wa soka kutoka nchi za Cameroon, Ghana, Tanzania, Kenya, na Uganda ili atakayeonesha ufahamu na ujuzi zaidi wa soka atavishwa taji la ubingwa wa` Pan-African’.
GUINNESS FOOTBALL CHALLENGE, ni kipindi cha runinga kinachotayarishwa na kampuni ya kimataifa ya Endemol. Kipindi hiki kinarushwa kila Jumatano katika televisheni za ITV na clouds TV. Kipindi kitaruhswa na kituo cha ITV kuanzia saa tatu na dakika kumi na tano(3:15) usiku ambapo Clouds TV itarusha kipindi hicho saa mbili na dakika kumi na tano(2:15) usiku .

Katika kipindi cha tano cha mashindano haya yatakayooneshwa na vituo vya televisheni vya ITV na Clouds TV, timu nne ndizo zitakua uwanjani kuchuana vikali, ni timu ipi itakayowapiga chini wengine na kuingia katika hatua ya Pan Africa? Majibu yote yatapatikana Jumatano hii.

Timu ya blu-Tanzania:
• Khenry Sadallah(26) na Abubakari Mohamed(19) kutoka Dar-es-Salaam watashiriki katika sehemu ijayo. Harry atakuwa kichwa cha timu ambaye ni mshabiki wa AC Milan wakati Abubakari ambaye ni mwanafunzi na mshabiki wa Manchester United ataonesha uwezo wake wa kucheza mpira

Timu nyekundu-Kenya:
• Ken Muturi (26) na Chris Mwamgi (19) wote kutoka Nairobi wanamatumaini makubwa yakuwa timu ya mwisho kuingia kwenye mashindano ya Pan African. Ken ni mfanyabiashara kwa njia ya mtandao, ni mpenzi wa mpira wa miguu ambapo atakuwa kichwa cha timu wakati Chris ambaye ni mchezaji wa Springland FC ataonesha kipaji chake cha mpira wa miguu.

Timu ya kijani-Uganda
• Mfanyabiashara Ian Ford (24) na mwanafunzi wa uchumi Herbet Odipio(23) kutoka Kampala ni mashabiki wa Manchester United watashiriki katika kipindi kijacho cha mashindano Guinness Football Challenge. Ian atakuwa kichwa cha timu wakati Herbet ataonesha uwezo wake wa kusakata kabumbu.

Timu nyeusi-Uganda:
Edward Lyukamuzi (23) na Timothy Nimungu (22) kutoka Kampala ni timu ya pili kutoka Uganda watashiriki kipindi cha 5 cha mashindano haya. Edward ni mtaalamu wa Teknolojia ya mawasiliano ndiye kichwa cha timu wakati Timothy ambaye ni mtaalamu wa masoko atonesha uwezo wake wa kucheza soka.

Wapenzi wa kipindi hiki cha Guinness Football Challenge barani Afrika wanakumbushwa kwamba, wanaweza kushiriki kwa kufuatilia kwa njia ya mtandao. Wanaweza kufanya hivyo kwa kujisajili bure kabisa katika tovuti ya m.guinnessvip.com.

Pia GUINNESS FOOTBALL CHALLENGE ina kurasa ya Facebook ambayo ni www.facebook.com/guinnesskenya, Ili kufuatilia kwa karibu yanayojiri, unatakiwa kufuatilia ukurasa huu ‘like’ na utakuwa unapata habari zote zinazohusu mchezo huu.

GUINNESS FOOTBALL CHALLENGE, ni kipindi cha mchezo wa soka kinachotayarishwa na kampuni ya kimataifa ya Endemol. Usikose kuangalia na kufuatialia kipindi hiki katika runinga yako kupitia televisheni za ITV na Clouds TV kila siku ya Jumatano usiku. Usisahau kuwa na chupa ya bia uipendayo ya Guiness wakati unaangalia kipindi hiki.

*Haiuzwi kwa walio na Umri chini ya miaka kumi na nane. Tafadhali Kunywa kistarabu.

Mabondia Ghana Kuwasha ‘Moto’ Mei 3

$
0
0

Albert Mensah (kulia)

NCHI ya Ghana ambayo ni moja ya nchi zenye vipaji vingi vya wanamichezo mahiri na majina makubwa hususan mchezo wa ngumi, itawaka moto Mei 3, 2013 wakati mabondia mahiri sita watakapo chapana kugombea mataji ya IBF katika ubingwa mbalimbali.

Bondia atakayeanza kupanda ulingoni kufukisha moto huo ni “Mtoto wa Kijiweni” Albert Mensah ambaye amejizolea sifa kemkem za kupambana na mabondia mahiri duniani. Mensah yuko kwenye viwango vya IBF vya dunia na amewekwa namba 7 kwa ubora duniani katika uzito wa Welter.

Mbabe huyu atakumbana na bondia mwenye maringo na “Mtoto wa Mjini” Ben Odamettey ambaye amekulia katika viunga vya Jamestown katika kata ya Bukom jijini Accra, ambayo ni maarufu kwa kutoa mabingwa wengi wa dunia kama kina Azumah Nelson, Ike Quartey, Joseph Agbeko na Poison Kotey. Wawili hawa watapambana kugombania ubingwa wa IBF katika bara la Afrika uzito wa Junior Middleweight.

Mpambano wa pili na unaongojewa kwa hamu kubwa ni ule wa mwanadada na mrembo kutoka Nigeria ambaye anaishi nchini Ghaba, Helen Joseph atakapombana na binti Mfalme kutoka Himaya ya Austrohungrian (Hungary) Marianna Gulyas. Warembo hawa wanagombania mkanda wa IBF wa Mabara wa wanawake katika uzito wa unyoya (Featherweight) na moto mkubwa unategemewa kuwaka kutokana na umahiri wa warembo hawa wa kurusha makonde ulingoni.

Helen atakuwa anarudisha heshina yake baada ya kupoteza pambano la ubingwa wa dunia kwa mwanadada Dahianna Santana wa Dominican Republic mwezi wa Desemba mwaka jana. Hii ni heshima pekee kwa kina mama kutoka bara la Afrika wa kuonyesha umahiri wao kwa binti huyo wa Kifalme kutoka Hungary.

Ndipo litakapokuja pambano la kukata na shoka kati ya mbabe kijana anayeinukia katika ulimwengu wa masumbwi nchini Ghaha na Afrika kwa ujumla bondia Issa Samir kutoka Ghana atakapopambana na mbabe kutoka kwenye jangwa la barafu la Siberia, bondia Robison Omsarashvili kutoka katika nchi ya Georgia ambayo ni moja ya nchi zilizokuwa kwenye Muungano wa Kishoshalisti wa Sovieti ya Urusi (USSR).

Ni nderemo na vifijo kwa Waghana na watu wote wa Afrika wakati mabondia hawa watakapo pambana kugombea mataji haya makubwa kabisa ya IBF na kuliwakilisha bara la Afrika katika ramani ya dunia.

Mapambano haya yanaandaliwa na kampuni ya GoldenMike Boxing Syndicate ya Accra, Ghana chini ya Henry Many-Spain na Michael Tetteh na yatafanyika katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Accra (Accra International Conference Center) na yatasimamiwa na Rais wa IBF katika bara la Afrika, Ghuba ya Uajemi na Mashariki ya Kati Mtanzania Onesmo Ngowi.


Mechi ya Azam, Simba Yaingiza Mil. 66/-, Yanga na Oljoro Mil. 63/-

$
0
0

Simba Sports Club

MECHI ya Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Azam na Simba iliyochezwa Aprili 14 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam imeingiza sh. 66,855,000 kutokana na watazamaji 11,458.

Viingilio katika mechi hiyo namba 155 iliyomalizika kwa timu hizo kutoka sare ya mabao 2-2 vilikuwa sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000 huku kila klabu ikipata mgawo wa sh. 15,587,177.45 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 10,198,220.34.

Mgawo mwingine wa mapato hayo ni asilimia 15 ya uwanja sh. 7,925,683.45, tiketi sh. 3,818,890, gharama za mechi sh. 4,755,410.07, Kamati ya Ligi sh. 4,755,410.07, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 2,377,705.03 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 1,849,326.14.

WATAZAMAJI 11,021 WAZISHUHUDIA YANGA, OLJORO

Watazamaji 11,021 walikata tiketi kushuhudia mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Yanga na Oljoro JKT iliyochezwa Aprili 13 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kuingiza sh. 63,170,000.

Viingilio katika mechi hiyo namba 156 iliyomalizika kwa Yanga kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 vilikuwa sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000 huku kila klabu ikipata mgawo wa sh. 14,853,252.45 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 9,636,101.69.

Mgawo mwingine wa mapato hayo ni asilimia 15 ya uwanja sh. 7,552,501.25, tiketi sh. 3,183,890, gharama za mechi sh. 4,531,500.75, Kamati ya Ligi sh. 4,531,500.75, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 2,265,750.37 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 1,762,250.29.

Boniface Wambura

Ofisa Habari

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

Jerry Silaa Ashiriki Bonanza la Stakishari Veterans

$
0
0

Mgeni rasmi, Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Silaa akikabidhi jezi na mipira kwa baadhi ya timu 17 zilizoshiriki katika Bonanza la Stakishari Veterans.


Picha juu na chini ni Mgeni rasmi, Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, Jerry Silaa akizungumza wananchi pamoja na washiriki wakati wa bonanza la timu ya Stakishari Veterans FC kutimiza miaka 5 ambapo amesema mpira wa soka unawakutanisha watu na kuwasidia kujenga mahusiano pamoja na kujenga afya za miili yao.

 

Picha juu na chini Mgeni rasmi, Mstahiki meya wa Halmashauri ya manispaa ya Ilala, Jerry Silaa akikabidhi jezi na mipira kwa baadhi ya timu 17 zilizoshiriki katika bonanza hilo.

 

Diwani wa Kata ya Kipawa, Bonna Kaluwa akigawa jezi na mipira kwa timu zilizoshiriki Bonanza la Stakishari Veterans kutimiza miaka 5.

Mgeni rasmi, Mstahiki meya wa Halmashauri ya manispaa ya Ilala, Jerry Silaa akijiandaa kupiga penati kuashiria ufunguzi wa Bonanza hilo lililofanyika katika viwanja vya Stakishari kata ya Gongo la Mboto jijini Dar.

Mstahiki Meya Jerry Silaa akionyesha ufundi na kufunga goli wakati akipiga penati ya kuzindua rasmi bonanza la Stakishari Veterans FC kutimiza miaka 5.

Mstahiki Meya Jerry Silaa akipongezwa na Golikipa aliyemfunga goli kwa penati wakati akizundua Bonanza hilo.

Mgeni rasmi Mstahiki Meya Katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa timu ya Stakishari Veterans FC iliyofanya Bonanza la kutimiza miaka 5 Kipawa jijini Dar.

Bonanza likirindima katika viwanja vya Stakishari Kipawa kata ya Gongo la Mboto baada ya kupewa baraka na Mstahiki Meya Jerry Silaa.

Timu zilizoalikwa kushiriki Bonanza la Sitakishari VSC

New Ukonga Veteran – Ukonga

Pugu Kajiungeni Veteran – Pugu

Pugu Kigogo Fresh Veteran -Pugu

Segerea Veteran – Tabata

Kivule Veteran – Kivule

Kipunguni B Veteran – Kipunguni

Kinyerezi Veteran – kinyerezi

Tabata Veteran – Tabata

Bandari Veteran – Kurasini

Mbagala Veteran – Mbagala

Makangarawe Veteran – Mbagala

Airport Veteran – Airport

Kisukulu Veteran – Kisukulu Tabata

Kigamboni Veteran – Kigamboni

Vingunguti veteran – Vingunguti

Wenyeji Sitakishari veteran

 

Bi. Kidude Afariki Dunia, Wajua Historia Yake?

$
0
0

Msanii maarufu na nguli nchini Tanzania Bara na Visiwani, Fatuma binti Baraka au maarufu kwa jina la Bi. Kidude


Na Mwandishi Wetu,

TAARIFA ambazo mtandao huu umezipata ni kwamba msanii maarufu na nguli nchini Tanzania Bara na Visiwani, Fatuma binti Baraka au maarufu kwa jina la Bi. Kidude amefariki dunia leo majira ya saa 4 asubuhi nyumbani kwa mtoto wa kaka yake maeneo ya Bububu leo mjini Zanzibar.

Bi. Kidude ambaye amekuwa akiugua kwa muda mrefu sasa huku mara kadhaa akizushiwa taarifa za kifo chake jambo ambalo limekuwa likizua tafrani kwa wapenzi wengi wa msanii huyo nguli wa miondoko ya taarab ndani na nje ya Tanzania.

Msanii huyo maarufu wa taarab za asili (zamani) na nyimbo za unyago alizaliwa katika Kijiji cha Mfagimaringo, akiwa mmoja wa watoto 7 wa familia ya Mzee Baraka aliyekuwa mfanyabiashara wa nazi, tangu enzi za ukoloni zao ambalo ni la kutumainiwa sana Zanzibar.

Inasadikiwa kwamba mnamo mwaka 1920 tayari nguli huyu wa taarab alikuwa ameanza kuimba katika vikundi vya sanaa kwao. Taarifa zinasema mwaka 1930 Bi. Kidude alijiunga na Egyptian Musical Club ya jijini Dar es Salaam kabla ya kuliacha kundi hilo mwaka 1940 na kurejea Zanzibar.

Hakuna anayepinga kutokana na historia yake, Bi Kidude ni miongoni mwa magwiji wa muziki katika Bara la Afrika. Hakuna anayejua tarahe rasmi ya kuzaliwa nguli huyu wa muziki hadi sasa, japokuwa inakadiriwa kuwa ana umri wa miaka 102.

Kwa mujibu wa taarifa ambazo Bi. Kidude aliwahi kuzitoa, anaeleza kuwa alianza fani hiyo tangu alipokuwa na umri wa miaka 10 na alijifunza kutoka kwa msanii mkongwe na aliyetamba sana enzi hizo Sitti binti Saad. Anasema wageni wengi kutoka sehemu mbalimbali walikuwa wakifika Zanzibar kuja kumwona Sitti, na kwa vile Bi. Kidude na Sitti walikuwa wako karibu basi yeye alikuwa akiwapeleka wageni wale nyumbani kwa Bi. Sitti, wakifika huko wageni walikuwa wakiingia ndani na yeye kubakia nje, kule ndani Bi Sitti alikuwa akiwaimbia wale wageni, na yeye huku nje alikuwa akimsikiliza kwa makini na kumfuatiza jinsi alivyokuwa akiimba. Aliendelea hivyo hadi akawa mahiri sana katika uimbaji.

Taarifa zinaeleza alipokuwa na miaka 13, kwa mara ya kwanza alitoroka nyumbani kwao Zanzibar na kukimbilia Tanzania Bara, baada ya kulazimishwa kuolewa. Lakini alipokuwa kigoli wa kutosha kuolewa aliolewa ingawa ndoa hiyo nayo haikudumu kutokana na manyanyaso aliyokuwa akiyapata, hivyo aliamua kukimbilia kaskazini mwa Misri ikiwa ni katika miaka ya 1930, huko aling’ara sana katika fani yake ya uimbaji na uchezaji ngoma. Lakini ilipofika miaka ya 1940 aliamua kurudi nyumbani Zanzibar ambako aliendelea na shughuli zake uimbaji.

Bi Kidude hakuwa akitegemea kazi moja tu ya kuimba, kwani pia ni mfanyabiashara ya ‘wanja’ na ‘hina’ ambavyo anavitengeneza yeye mwenyewe, pia ni mtaalamu wa matibabu kwa dawa za mitishamba na zaidi ya hayo ni mwalimu mzuri sana wa ‘Unyago’ na ameanzisha chuo chake mwenyewe na anasema katika wanafunzi wake wote hakuna aliyepata talaka kutoka kwa mumewe.

Watu wanasema ‘Utu uzima dawa’ Bi. Kidude alikuwa na upeo mkubwa wa akili kwani pamoja na kukulia katika mazingira yaliyogubikwa na tamaduni za kiarabu ambapo mwanamke anatakiwa wakati wote akiwa hadharani ajifunike, Bi Kidude aliliona hili katika upeo mwingine kwamba ni sheria tu ya kitamaduni toka Uarabuni, hivyo aliamua kuvunja sheria hiyo na kuondoa hijabu mwilini mwake, na kuvaa kama Mtanzania na si kama Mwarabu.

Lakini hakubakia hapo alivunja na miiko mingine zaidi ya kutokunywa na kuvuta, kwani Bi Kidude anakunywa pombe na kuvuta sigara jambo ambalo si kawaida kwa wanawake Zanzibar. Bi Kidude amekwisha tembelea nchi nyingi sana ikiwa ni pamoja na Oman, Ufaransa, Hispania, Ufini, Ujerumani na Uingereza.

Muziki aliyokuwa akiimba ni Bi. Kidude ni mchanganyiko wa muziki toka nchi za Kiarabu na vionjo vya muziki wa Kiafrika umekita sana katika mwambao wa Afrika Mashariki yaani Zanzibar, Mombasa, Lamu na kwingineko.

Bi. Kidude amewahi kushinda na kutunukiwa tuzo mbalimbali: mwaka 2005 alishinda tuzo ya ‘WOMEX’ ikiwa ni kutambua mchango wa mwanamuziki huyo katika tasnia ya muziki na tamaduni za Zanzibar. Amekwisha pata tuzo tena ya Tamasha la Filamu la Nchi za Jahazi (ZIFF) mwaka 1999 tuzo ni ya maisha.

Rais Jakaya Kikwete pia alimtunuku Bi. Kidude Nishani ya Sanaa na Michezo kwa mchango wake katika sanaa nchini mwaka 2012. Bi. Kidude. Baadhi ya nyimbo alizowahi kuimba ni pamoja na Muhogo wa jang’ombe, na anaimba kwa Kiswahili na Kiarabu. Hakuwahi kupata elimu nyingine zaidi ya Kurani.

Habari hii imeandaliwa na www.thehabari.com kwa kushirikiana na mitandao ya kijamii

Onesmo Ngowi Kuongoza Ujumbe Mzito Mkutano wa Shirikisho la Ngumi Kimataifa, Ujerumani

$
0
0

Onesmo Ngowi

MTANZANIA, Onesmo Ngowi ambaye ni Rais wa Shirikisho la Ngumi la Kimataifa Bara la Afrika, Ghuba ya Uajemi na Mashariki ya Kati, ataongoza ujumbe mzito kutoka Bara la Afrika na Ghuba ya Uajemi kwenye Mkutano wa 30 wa Shirikisho la Ngumi la Kimataifa na Chama Cha Ngumi Cha Marekani (IBF/USBA).

Mkutano huo utafanyika katika hotel ya nyota tano ya Concorde Berlin iliyo karibu na Kanisa la kumbukumbu la Kaiser Wilhelm pamoja na taasisi ya Helmut Newton na Jumba la ukumbusho wa Picha jinini Berlin, Ujerumani.

Ujumbe atakaoongoza Ngowi utajumuisha wajumbe kutoka katika nchi za Afrika, Ghuba ya Uajemi na Mashariki ya Kati na mpaka sasa ni nchi 31 zitakazo jumuika katika ujumbe huo ambao utajumuisha viongozi wa mashirika mbalimbali ya kusimamia utalii, biashara na michezo.

Mbali na kuhudhuria mkutano huo utakaofanyika kwa siku sita kuanzia Mei 21 mpaka Mei 26, ujumbe wa Ngowi utafanya pia mazungumzo na viongozi pamoja na taasisi mbalimbali zinazosimamia Utalii, Uwekezaji pamoja na Utalii wa Michezo katika nchi ya Ujerumani na nchi nyingine za Ulaya ambazo zitatembelewa na ujumbe huo.
 
Katika msafara huo ambao utajumuisha pia viongozi wa bodi za Utalii na Michezo kutoka katika nchi za Botswana, Afrika ya Kusini, Ghana, Misri na Falme za nchi za Kiarabu (UAE),ujumbe huo utatembelea pia nchi za Ufaransa, Ubeljiji, Uhispania pamoja na Uholanzi!

Ngowi amewahimiza watanzania juu kuchangamkia fursa za kujitangaza kibiashara nje ya nchi na kuwataka kujituma. “Ni muhimu Watanzania wakafungua macho na wajue kuwa dunia sasa ni kijiji na wasipoangalia watajikuta wanabaki nyuma kila mara” aliema Ngowi ambaye kwa ujumla alionyeha kusikitishwa na muitikio mdogo wa watanzania kwenye masuala ya kujitangaza kibishara nje ya nchi.
 
Ujumbe wa Ngowi utaondoka barani Afrika tarehe 17 Mwezi Mei na kuelekea Dubai ambako ndipo wajumbe wote watakapokutana tayari kwa msafara wa kuelekea jijini Berlin, Ujerumani!
 
Imetolewa na; INTERNATIONAL BOXING FEDERATION AFRIKA (IBF/AFRIKA) DAR ES SALAAM, TANZANIA 

Mashindano ya Ngumi Klabu Bingwa Mkoa wa Temeke Yaendelea Bila Udhamini

$
0
0

Bondia Athumani Yanga wa timu ya Ashanti Boxing ya Ilala akioneshwa mkono juu baada ya kumpiga Yusuph Saidi wa Kokoto wakati wa mashindano ya Klabu bingwa ya wilaya ya temeke yaliyoanza jana Yanga alishinda kwa point na kupereka shagwa katika klabu ya Ashanti

Na Mwandishi Wetu

MASHINDANO ya Klabu Bingwa ya Mkoa wa Temeke yameanza jana jijini, Dar es Salaam huku
yakishirikisha timu 20 na yanatarajiwa kufikia tamati  Aprili 19 mwaka huu. Lengo la mashindano hayo yaliyoanza jana ni kuinua vipaji vya mabondia chipukizi na kupata vipaji bora watakaokuwa chachu ya maendeleo ya mchezo nchini.
 
Kocha wa kimataifa wa mchezo huo nchini Rajabu Mhamila ‘Super D’ alisema vijana wanakaoshiriki mashindano hayo walipima uzito katika Ukumbi wa CCM Kata ya 15, Temeke Dar es Salaam. Super D ambaye pia ni kocha wa timu ya Mkoa wa Ilala ambao ni waalikwa katika michuano hiyo alisema vijana wake kutoka klabu ya Amana na Ashanti watafanya vema katika mashindano hayo.
 
Mkoa wangu umetoa vijana sita ambao naamini watafanya vizuri katika mashindano hayo na kutoa upinzania mkubwa ambao utakuwa chachu ya maendeleo ya mchezo huo nchini. Super D aliwataja baadhi ya mabondia hawo kuwa ni Hussein Mawimbi na Said Hamisi kutoka klabu ya Amana na Athumani Yanga pamoja na Said Mabunda kutoka klabu ya Ashanti.
 
Pia aliwaomba wadau kujitokeza kusaidia mashindano hayo yanayofanyika katika ukumbi wa CCM Kata ya 15, Temeke ili kuhakikisha hamasa ya kuendeleza mchezo huo inapatikana yatakayofanikisha mafanikio ambalo ndilo lengo kubwa. la mashindano hayo

Kocha huyo wa kimataifa wa mchezo wa ngumi nchini, alisema kuwa katika mchezo huo kutakuwa na CD na DVD za mafunzo wa mchezo huo zenye mapambano makubwa ya mabondia wa ndani na nje ya nchi. Aliongeza kuwa baadhi ya mapambano yaliyomo ni katika CD na DVD hizo ni ya Kalama Nyilawila dhidi ya Francis Cheka, Mbwana Matumla na Francis Miyeyusho, Said Mundi na King Class Mawe. na Francis Cheka dhidi ya Japhet Kaseba mapambano yote mawili mbali na hivyo atakuwa akisambaza vifaa vya mchezo wa masumbwi kwa mabondia ambao awana wanaweza kumuona na kujipatia vifaa mbalimbali.

Viewing all 521 articles
Browse latest View live